TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,868
- 5,753
Sasa mambo ni hadharani. ILE vita ya Urais wa 2015 iliyokuwa ikipiganwa kati ya Viongozi Wakuu wa Vyama vya siasa nchini vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi, maarufu kwa jina la UKAWA, sasa imehamia kwa MAFAHALI wakuu wawili ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mwenyekiti wa chama hicho , FREEMAN MBOWE anataka kugombea Urais wa 2015 kwa tiketi ya chama chake kwa udi na uvumba.
Uamuzi wa MBOWE na Wapambe wake kutaka kumuweka kando Dr. SLAA umejengwa katika misingi mitatu:
1. Ujana wa MBOWE ukilinganisha na Dr. SLAA
2. DHEHEBU lake la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT
3. Uzee na hali ya afya ya Dr. SLAA ambayo inaelezwa kudorora siku hadi siku kadri siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 zinavyokaribia.
Tayari vyama viwili kati ya vinne vinavyounda UKAWA , CUF na NCCR-MAGEUZI vimekwisha kumtangaza mgombea wake wa Urais ambapo CUF wamemtangaza Prof. IBRAHIMU HARUNA LIPUMBA na NCCR-MAGEUZI wamemtangaza Dr. GEORGE KAHANGWA ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hadi sasa CHADEMA na NLD bado hawajawatangaza wagombea wao tayari kuingia kwenye KAPU la UKAWA na wale wa CUF na NCCR ili kumpata mgombea mmoja atakayeshindana na mgombea wa CCM.
Taarifa zaidi zinasema shinikizo la kumtaka Mbowe agombee kupitia MBOWE linatoka katika makundi makuu mawili ambayo ni
1. Waumini wa KKKT
2.Wafanyabiashara wanaotoka Ukanda wa Kaskazini wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa kawaida jamii ya Mkoa wa Kilimanjaro imekuwa ikiishi katika matabaka mawili yenye misimamo isiyoingiliana kuanzia kwenye mila , desturi na tamaduni zao.
Kwa mjibu wa Mbunge mmoja wa Chadema, matabaka hayo ni ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wanaoishi Ukanda wa kaskazini kwa upande mmoja ambao unatamabulika zaidi kwa jina la CHAGALAND, na wananchi wanaoishi ukanda wa chini au wa kusini , ambao ni jamii ya WAPARE.
IMEELEZWA kwamba wafuasi wengi wa Chadema katika Ukanda huo wa kaskazini , ambao wengi wao ni waumini wenza wa MBOWE katika dhehebu la KKKT , wangependa kuona safari hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokana na Kanisa hilo.
Kundi la pili la Wafanyabiashara walioko nyuma ya Urais wa Mbowe , ambao wana asili ya Ukanda wa Kasakzini mwa Mkoa wa Kilimanjaro inasemekana wamekuwa ni chachu ya Nguvu ya ksiasa iliyonayo CHADEMA kwa sasa kutokana na michango ya ufadhili wa hali na mali kitoka katika jamii hiyo.
Hivyo wafanyabiashara hao wa kutokea ukanda wa Kaskazini mwa Mkoa wa Kiliamnjaro wangependa kuona Juhudi zao za kukifhadhili chama zinazaa matunda kwa kumuwezesha Mh. MBOWE kuwa mgombea urais hasa ukizingatia kuwa ni mtu kutokakatika UKANDA ambao wanatokea.
Chanzo: TAZAMA Tanzania.