Vita Rashid Mfaume Kawawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita Rashid Mfaume Kawawa

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Yo Yo, Oct 20, 2008.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Huyu ndio mbunge wa jimbo la Namtumbo na ufuatao ndio wasifu wake kwa mujibu wa tovuti ya Bunge

  Kazaliwa Mwaka 1964
  Elimu yake ni kama ifuatavyo

  Shule ya msingi Turian:1972-78

  Sekondari Agakhan Mzizima :1979-82

  Elimu ya juu College of Business Education:Advanced Diploma in Business Administration:1988-89 and Certificate in Computer Data Processing mwaka huu huu 1988 mpaka 1989

  Pia kahudhuria

  The City and Guilds of London Institute na kutunukiwa The City and Guilds of London Institute mwaka 1996
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...That's all???????????!!!!!!!!!!!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  KWani ana issue gani zaidii?labda haja update CV yake......adv dip sio elimu tosha jamani?au lazima awe na MBA ndio awe Mbunge?au mimi sijaelewa mnaongelea nini....nihabarisheni
   
 4. Mama Subi

  Mama Subi Member

  #4
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Sasa Yo-yo, hii post inamaanisha nini? Labda tunge elimishana masharti ya kuwa mbunge wa jumuiya ya muungano wa Tanzania ni yapi ili tuweze kuelewa una maanisha nini kwasababu hivi sasa inaonekana kama unamuonea huyu mheshimiwa kwasababu kuna wengi wenye elimu na experience ndogo kuliko yakwake.
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  ...sasa vita inaonesha kasoma sekondari ..1979 hadi 1982 ..ni miaka minne.....kwa hiyo ameishia form four ....hata kama alijisomesha hadi form six kupata sifa ya kujiunga adv dip...as private candidate haijasema pia...

  Hailezi mwaka 1982 hadi 1988 alipojiunga na advance dip...alikuwa akifanya nini....

  Inajulikana wazi kuwa course ya adba ni ya miaka mitatu lakini inaonyesha kuwa vita aliisoma kwa mwaka mmoja tu ....hakuna kozi kama hiyo labda ya certificate.....

  Je mleta hoja anataka tufanye utafiti kama vita kawawa ni kihiyo mwingine?? Au vita amefoji vyeti na cv.....

  Itabidi tuwekewe cv kamili ya vita ..kwani hii haijatulia...

  ..
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa wadhifa alionao, elimu yake inamtosha sana na anawazidi wabunge na wanasiasa wengi, including viongozi wa juu kama Mh. Mbowe. Let's leave him alone unless there is an issue with his work/perfomance.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Is that all??????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Hiyo miaka ya advanced diploma mbona inatisha, yaani kamaliza advanced dipolma within a year. Kweli ni kipanga sana huyo, ingekuwa sasa hivi tungempeleka special schools!!!! tehe tehe tehe!!!

  A level alisoma wapi??? Kwanza waliosoma naye alipata div gani form iv????

  Ili aweze kusoma advanced dipoloma ni sheria awe na certificate au awe amemaliza form six na kufaulu!!!!!!!!! Sasa kwenye hii CV sioni miaka amesoma certificate!!!!!

  Na huko the City and Guilds of London Institute alisomea nini na alitunukiwa cheti gani????

  Jamani itafika mahali sasa tufanye scrutiny ya vyeti hata kwenye Siasa!!!!!!!

  Halafu kule NECTA waanze kufanyia Scrutiny vyetu vyote vya waajiriwa au basi iundwe taasisi ya kufanya kazi hiyo na ianzie kwa viongozi wetu.

  Nasikitika watu wamefauli kiukweli na vyeti halali lakini hawana post nzuri kwa kuwa tu kijana wa fulani kafoji cheti na kwa kuwa ana mtu wa kumkingia kifua anapata kazi nzuri na mwenye haki anasota. Yaani nakuambia zoezi la kuhakiki vyeti likipita halafu wahusika wanakuwa publicized then watu tutapata kazi za maana ile mbaya maana nafasi nyingi za sasa zita fall vacant!!!! Du Tanzania usanii mwingi mno kila mahali!!!!
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ndio wasi wasi wangu unapoanzia hapo......sijawahi kuona au kusikia ADBA ya CBE ni ya mwaka mmoja......nina wasiwasi na hii either Cv yake imekosewa na wawekaje kwenye tovuti ya bunge au hiyo sio ADBA ni certificate
  Ndio haswaa
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Niambieni kifuatacho,

  Hivi vyeti ni vyake kweli, na haja vi misrepresent. Full stop.

  Kama hilo la juu ni kweli, mwacheni. Kwani kuna educational qualification ya kuwa mbunge ambayo hajaifikia?

  Kama mnataka kuleta issue ya kuwa amekuwa mbunge kwa sababu mtoto wa Kawawa semeni, lakini hamuwezi kumsema mtu kama huyu, nshomile mpaka "London City Guild" si mchezo ati!

  Huyu kampita hata Cisco Mtiro ati na Cisco alikuwa positioned kuwa Mkuu wa Itifaki.Not that I am for anti intellectuallism, but come on people, lets not gloat with elitism.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,976
  Trophy Points: 280
  Yoyo,

  ..advanced diploma ya mwaka mmoja makes sense kwasababu alichukua diploma hapo hapo CBE.


  ..mimi ni kati ya wale tunaoamini kwamba Tanzania ianzishe mfumo utakaowezesha wanafunzi ku-transfer credits frm one higher institution to another.

  ..sidhani kama mwanafunzi mwenye diploma anapaswa kusoma miaka yote mitatu ili kupanda ngazi kupata 1st degree ktk vyuo vyetu vikuu. anachopaswa kufanya ni kusoma vile vipindi ambavyo hakusoma ktk diploma yake.

  NB:

  ..masters degree ktk University za UK na Scotland huchukua mwaka mmoja kuhitimu.
   
 12. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Masters kusomwa kwa mwaka mmoja ni sawa, lakini siyo kwa degree ya kwanza! Advanced Diploma ya CBE ni miaka mitatu. Kama alisoma mwaka mmoja na akashindwa kuendelea na masomo kwa sababu yoyote ile (ikiwemo ku-disco) basi hatakiwa kuweka hiyo hapo!
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,976
  Trophy Points: 280
  Masaki,

  ..kweli kabisa advanced diploma ya CBE ni mwaka miaka 3. kozi hiyo ilianzishwa miaka mingi baada ya chuo kuwa kinatoa diploma ya miaka 2.

  ..hebu ongeza wigo wa mjadala kidogo. kuna wanafunzi waliosoma diploma ya CBE, halafu wakaenda makazini. je, wakitaka kupata cheti cha advanced diploma ya CBE lazima wachukue miaka mitatu sawa na wale wenye vyeti vya sekondari?

  ..kuna ulazima gani wa mwanafunzi aliyehitimu Diploma miaka 2 ya CBE, kulazimika kusoma miaka mingine mitatu, ili ahitimu na advanced diploma ya CBE? yaani mwanafunzi achukue jumla ya miaka 5 kuhitimu advanced diploma?
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  nakubali ilikuwepo zamani hata katika chuo kama Ushirika moshi.......lakini sijaona Vita alichukua diploma lini kama unafahamu alichukua diploma lini basi tuambie
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo panapohitaji marekebisho ya mitaala ya chuo husika. Lakini naamini kwamba dozi ya Diploma ya masomo ya miaka miwili ni ndogo ukilinganisha na dozi ya Advanced Diploma. KWa hiyo kuongeza mwaka mmoja ili mtu apewe Adv Diploma inakuwa haina maana.

  Wanachoweza kufanya ni kusomesha certificate ya mwaka mmoja yenye mitaala inayoweza kumwandaa mwanafunzi kuweza kusoma Advanced Diploma ya miaka mitatu bila ya kuhitaji kusoma tena ile Diploma ya miaka miwili. Mzumbe ndio wameanzisha utaratibu huo kwa sasa!
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Oct 21, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  jamani ni Mzee Kawawa mnamzungumzia au nani? ... Amezaliwa 1964?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  MwanaJamii; si mzee Kawawa ni Vita ni mtoto wa wa mzee kawawa ndiye anazungumziwa hapa.
  Inaelekea cv yake bungeni inawalakini.
  Waliona habari kamiri endeleeni kutu habarisha.
  :D:D:D:D:D:D:D:D
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Vingine havikai kwenye CV jamani.......

  Tanzanianjema
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu unafahamu maana ya CV?
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,335
  Trophy Points: 280
  Elimu ya juu hapa bongo is unfair. Zamani mtu aliyesoma diploma ya Journalism alienda Cardif kuchukua Masters. Leo hata kama una diploma inabidi usote miaka 3 kupata advanced diploma. Miaka 3 mingine kupata degree. Kumeletwa post graduate diploma mwenye diploma hakubaliwi kujoin mpaka uwe na 1st degree. Is it fair?.
  Kupata degree ya sheria LL.B ya UDSM unaisotea miaka 4. Unajumlisha mwaka 1 wa law school, jumla miaka 5. Kusoma sheria hiyo hiyo Mzumbe ama Tumaini ni miaka 3 tuu! Usawa uko wapi?.

  Namalizia kuhusu Mhe, Vita Kawawa. Jamaa is humble and down to earth. Anaheshimu watu wa aina zote, hana kujisikia wala majisifu na anajichanganya na watu wa aina zote.

  Sifa ya ziada ya .he huyu ni extra ordinary support kwenye shughuli za kifamilia. Nilimuona kwenye TV akimsadia Mzee Kawawa kilimo cha uyoga na pia nimewahi kumshuhudia akisaidia kuhudumia wageni kwenye catering ambayo ni moja ya biashara za mkewe.

  Elimu yake mbona safi tuu. Kuna wabunge naomba usisikie, mmoja namjua aliishia darasa la 8 tuu na hukujiendeleza chochote.
   
Loading...