Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Redio TBC1 ya saa mbili usiku huu(kwa saa za Afrika Mashariki), Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda imefuta leseni zote za waganga wa jadi. Hii ni katika vita dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi(albino) ambayo imepamba moto.
Suala la kuangalia hapa ni je serikali inamamlaka ya kuweza kufuta hizo leseni? Je waganga wa jadi wanaweza kwenda kupinga amri hii ya serkali ukichukulia kama jambo hili laweza kuwa limefanyika zaidi 'sentimentally' Kuliko kuangalia sheria inasemaje.