Vita Dhidi ya Mauaji ya Maalbino-Serikali yafuta leseni zote za waganga wa jadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita Dhidi ya Mauaji ya Maalbino-Serikali yafuta leseni zote za waganga wa jadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Jan 23, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Redio TBC1 ya saa mbili usiku huu(kwa saa za Afrika Mashariki), Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda imefuta leseni zote za waganga wa jadi. Hii ni katika vita dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi(albino) ambayo imepamba moto.

  Suala la kuangalia hapa ni je serikali inamamlaka ya kuweza kufuta hizo leseni? Je waganga wa jadi wanaweza kwenda kupinga amri hii ya serkali ukichukulia kama jambo hili laweza kuwa limefanyika zaidi 'sentimentally' Kuliko kuangalia sheria inasemaje.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kama ni kweli hapa serikali itakuwa on the otherside of the law, kwa sababu nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria in the first place pamoja na mengi mengine ilikuwa ni kuepukana na hizi generalizations, yaani kwa mfano majambazi walipozidi wakati fulani hapa bongo, sasa dawa ni kuwafukuza polisi wote maana wengi wanashirkiana na majambazi? That is nonesense!

  - Serikali inatakiwa kuwakamata waganga wanaojihusisha na Albino na inaweza kuwakamata kwa kuwatuma makachero wake kwa waganga hao, lakini kuwanyima leseni wote wka sababu ya isolated ishus za waganga wachache sio haki kabisaa, hapa serikali inajaribu ku-ride on short term popular political ishu, badala ya kukamata mafisadi wote ambao ushidi upo wazi sasa wao wanataka kuonea wanyonge tu mpaka lini?
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  KUFUTA LESENI ZA WAGANGA WA JADI SI KUFUTA USHIRIKINA.
  Exaud J. Makyao
   
 4. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwanza labda tukubaliane, hatujui kilichosemwa na serikali hapa. Inawezekana wanafuta hizi leseni ili kutunga taratibu mpya zitakazoweka wazi mipaka ya nani mganga nani mwanga, na nani Shekhe Yahya, na nani kigagula, nani mwana mazingaombwe. Hakuna anaejua kinachoendelea, (hatuna press, hili linajulikana).

  Lakini kuhusu nguvu ya serikali kufinyangafinyanga sheria bila kuwa na idhini ya bunge ni kwamba sheria za Tanzania zimeandikwa kijanja janja sana, zinaipa serikali nguvu ya kuzibadilisha, kutia chumvi, kuzifuta bila kuogopa mahakama wala bunge. Angalia hapa:

  Kwa mtaji huo, kwa silaha ya sheria hii, waziri husika anaesimamia hii "council" na "commitee" ya kuandikisha waganga ana maguvu ya kufuta na kuchokonoachonoa sheria anavyotaka kwa kisingizio cha ku-regulate kazi za hiki chombo.

  Kibaya ni kwamba hakuna wananchi wanaoenda mahakamani kupinga misapplications za sheria za nchi. Kwamba haki ya kutangua na kutunga sheria hawezi kupewa waziri kwa mlango wa uani wa regulation. Hili jambo marehemu Lugakingira alilia nalo sana, yani serikali ikisema imesema, imetoka.
   
 5. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Kuhani, asante kwa mchango wako.

  Kuhani, Lets give it a benefit of doubt kwamba hicho ndio kilichosemwa;

  Katika administrative law, utawala wa kisheria unamtaka yule mwenye madaraka ya kusimamia huduma fulani mfano hapa mtoa leseni za huduma za waganga wa asili hawezi kuamka usiku na kusema tunafuta leseni lakini anaweza kusema kwamba leseni hizo zikiisha muda wake hazitafanywa kuwa mpya(renew) mpaka masharti mapya yamekidhiwa.

  Pili, mamlaka yoyote inapaswa kwa mjibu wa sheria kumsikiliza yule anayetaka kunyang'anywa leseni kabla ya kutoa maamuzi; pili mwomba leseni au mwenye leseni lazima apewe sababu za yeye kunyang'anywa leseni hiyo na zaidi ya hapo anatakiwa aambiwe ni wapi anaweza kwenda kukata rufaa yake.

  Tukirudi kwenye suala la kanuni ndogondogo(regulations) zinaweza kupingwa katika mahakama ya kawaida kama haziendani na sheria mama( an Act of Parliament). Na kumbuka mamlaka (serikali)haina uwezi wa kufuta au kubadilisha sheria yoyote iliyopitishwa na bunge. Tatizo wengi ulizika na maamuzi ya wakubwa(Nidhamu ya uoga) yale yale ya mfalme aliyesimama mbele ya wasaidizi wake uchi na hakuna aliyesubutu kumsema kwamba yuko uchi( Naongelea wasaidizi wa huyu mkuu waaoshindwa 'kumwambia" bosi wao kwamba "anachemka"

  Ni aibu kwa viongozi wetu kutoa kauli hiz za ajabu ajabu ambazo mwananchi wa kawaida anaweza kuzitumia kuvunja amani; Pili, viongozi wajifunze kufanya 'homework' zao kabla ya kutoa matamshi ya ajabu ajabu kwani kizazi cha sasa cha Kitanzania si cha mwaka 47
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli SAFI SANAAA
  Na tena serikali iongezee kifungu hapo atakayeonekana anaenda sijuwi kwa mganga Apigwe mijiledi na kifungo juu.
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu, Mkama;

  Lengo la waziri mkuu ni sahihi ila walakini hupo katika hizo taratibu alizotumia kufanya hayo maamuzi ndo wasiwasi wangu ulipo hapo.
   
 8. A

  Aluta Member

  #8
  Jan 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimesoma habari hii sikumbuki wapi ila nimeona kuwa Waziri Mkuu aliwasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali na kumuuliza kwanza kama kuna uwezekano wa kufuta vibali vyote vya Waganga wa jadi. Na jibu likawa Inawezekana. Sasa basi tusielekeze mashambulizi kwa waziri mkuu bali kwa Mwanasheria Mkuu. Serikali haijaamua yenyewe swala hili. Japo la pili ni kuwa kama serikali imetoa vibali hivyo kwa nini isiwe na uwezo wa kuvifuta. Kama kuna waganga halali wa mitishamba basi watatakiwa kujisajili tena na dawa zao za jadi lazima zihakikiwe na Hospitali ya Muhimbili kama zaweza tumika kama alternative, pindi tu ugonjwa unaposhindakana hospitali na mgonjwa lazima apate cheti toka hospitali kuwa anaweza pata tiba mbadala. Kumbukeni lengo ni kuwaokoa hawa malaghai wanaopoteza maisha ya wenzetu wasio na hatia kwa malengo yao binafasi. Na kuwaondoa wachawi na wanga wote wanaowajaza watu upumbavu na kusababisha maafa haya!Namuunga mkono Pinda asilimia 100%!
   
  Last edited: Jan 25, 2009
 9. B

  Balingilaki Member

  #9
  Jan 24, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We unapotosha maana nzima ya majadiliano haya mtu ana haki ya kutoa mawazo lakini sio kama yako yaliyojaa ushabiki na chumvi kama za siri kali na ninakumbuka katika R v.Kajuna ilisemwa ijapo kwa kimombo 'our people believe, are believing and will still believe in witchcraft whether we like it or not even if the universe became literate tomorrow morning' serikali ilitakiwa kuangalia namna ya kuelimisha kwanza yhat is 'create morality among tanzanians' ili waone binadamu wote ni sawa na kila mtu anatakiwa kulinda maisha ya mwenzake

  Sasa kuna uwezekano mkubwa kuwa mauaji yakaendelea kwa kasi ya ajabu maana jamii imeishaona 'tija' katika watu kama maalbino.
   
 10. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Hii imenipa flashback ya enzi zile za Mzee wa Kiraracha alipokuwa akiwapa watu siku saba kwa maamuzi yake ya kukurupuka!
  It will be very interesting kuona ni waganga wangapi wa kienyeji watakamatwa kwa ku operate bila leseni, ninachofahamu mimi wengi wao hii ndio kazi yao na wanaitegemea kwa kipato!
  Tukumbuke pia viongozi wetu wanavyohusudu 'ndumba' na uchaguzi ndio huo unajongea, wao ninavyojua ndio wapo mstari wa mbele kwa ushirikina sasa sijui utekelezaji wa hili suala utakuwaje! Am sure tutatendelea kuona mashangingi yakielekea mlingotini nyakati za usiku kama kawaida.
  Vilevile hii naona ni kuwatafutia watu matatizo tu, itakuwa rahisi kwa mganga wa jadi kumshusha busha mgambo aliyepewa maagizo akamkamate badala ya kupimga kipapai aliyetoa decision.
  Yangu macho.............................
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama leseni wanatoa bure wanaweza kuzifuta lakini kama kuna ulaji sidhani kama itakuwa jambo zuri kwa upande wao.
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  we fiedmashal ni mteja wa waganga ehee, mbona umeumia kufutwa kwao vibali? waganga ni watu wa shetani na hatuwataki hapa bongo. pamoja na kwamba sina uhakika kama selikali kweli imedhamiria kwasababu viongozi wote selikalini ni wateja wakubwa wa waganga. wamechanja chale hadi sehem zisizochanjika, wamejizindika kwa uchawi kama shetani. sasa sijui kama watakuwa serious au ni changa la macho.
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ni vigumu lakini kuamini kuwa mu wa sumbawanga anaweza kufuta vibali vya waganga au anaweza kupinga uganga. vilevile ni vigumu kuamini kuwa mtu aliyezaliwa bagamoyo kama jk, anaweza kuwa serous na kufuta uganga tz hapa. inahitaji moyo. rais wa bagamoyo, waziri mkuu wa sumbawanga,kazi kwelikweli.

  alitamba kuwa ataweka kura ya maoni watz wote wapige kura, hadi leo naona kimyaaaaa, sasa sijui kama kweli alikuwa serious. mtu wa bagamoyo huyo. tena anasali dini ya wasoma nyota na watabiri.
   
 14. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mi nilishasema siku nyingi sana! tutatunga sheria, tutatoa maagizo, amri marufuku za aina zote lakini NANI MSIMAMIZI?

  Si ni wiki hizi tumeambiwa kuna kura za Wauaji? ziko wapi? aliyesema ni mkuu zaidi. Sasa yanakuja ya waganga kwani ndo wanahitaji utajili na madaraka ya kisiasa?

  Niliuliza hivi Huyo Waziri wa mambo ya ndani yuko wapi?? nilisema hafai kuliko mifuko ya plastiki. Eti nikaambiwa kuzuia mauaji ni jukumu letu wote. Wapi huko? yaani hata hao wauaji ni jukumu lao. Hakuna wajibu kama kazi ni ya kila mtu.

  Waziri nasikia yuko mitaa ya Dar na ma-miss tu!! hatumusikii, hana initiative yoyote kwake yeye yote gawiza na lipstick.

  Na sasa limekuja la kutafuta watoto wenye viganja sijui vya aina gani na gani.

  HII NI SERIKALI!
   
Loading...