TUJIKUMBUSHE: Kwanini walengwa wakuu kwenye mauaji ya Kibiti walikuwa viongozi wa chama na Serikali pamoja na wanachama wa CCM tu?

yvegenc prymacov

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
1,529
1,921
Habari,

Ukiwa unajua ulikotoka ni rahisi pia kujua unakoenda. Taifa letu limewahi kukumbwa na mauaji ya kukusudia, walengwa wakuu wakiwa ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wenyeviti wa vijiji, makatibu wa CCM, madiwani wa CCM pamoja na taasisi za kiserikali.

Je, lengo hasa la mauji hayo dhidi ya viongozi wa chama na serikali tu ilikuwa ni nini? Nani alikuwa mfadhili wa hayo mauaji? Nani alikuwa nyuma ya hayo mauaji?

Nauliza hivyo kwa sababu;

1. Mauaji yalitokea baada tu ya uchaguzi mkuu 2015, je, yalikuwa na uhusiano na huo uchaguzi?

2. Walengwa wa hayo mauaji wengi walikuwa ni wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi, viongozi na watumishi serikali ya Chama Cha Mapinduzi, je, wauaji pia nao walikuwa na mrengo wa kisiasa?

3. Kupotea kwa Azory Gwanda, kulikuwa na uhusiano gani na hayo mauaji ya Kibiti?

4. Kesi ya Mbowe ya ugaidi, ushahidi uliotolewa na vyombo vya usalama, wanajeshi pamoja na raia wakiambatanisha vielelezo vyote kama; sauti ya Mbowe, picha zake na ushahidi wa mazingira na vielelezo, mpaka Mahakama ikamkuta na kesi ya kujibu. Je, kesi hiyo ilikuwa na uhusiano wowote na mauaji ya kigaidi ya Kibiti?

Nauliza hayo lengo langu ni kupata elimu, kwani JF kuna hazina kubwa ya wajuvi.
 
Kesi ya Mbowe ya ugaidi, ushahidi uliotolewa na vyombo vya usalama, wanajeshi pamoja na raia wakiambatanisha vielelezo vyote kama; sauti ya Mbowe, picha zake na ushahidi wa mazingira na vielelezo, mpaka Mahakama ikamkuta na kesi ya kujibu. Je, kesi hiyo ilikuwa na uhusiano wowote na mauaji ya kigaidi ya Kibiti?
Umeuliza ujinga hivyo unastahili kujibiwa kijinga pia!
 
Waulize waliozima mjadala ule usijadiliwe bungeni. Kwenye kesi ya Mbowe pale ndio udhaifu wa mahakama zetu kutumika kwenye siasa chafu ulidhihirika.

Hakuna wakati ushahidi wa kipuuzi kama ule ulitamalaki mahakamani hadi ikawa aibu kuwa vyombo vya dola kuwa havijui muongozo wa kazi zake.

Inshort ule usemi wa kuwa hii ni shithole country ulidhihirika.
 
Wewe, kama hujawahi kuambiwa, kwa vyovyote una tatizo la akili. Hata uambiwe mara ngap, inaonekana kutokana na udogo wa akili, huna uwezo wa kuelewa.

Unakumbuka hata kauli moja kuhusiana na matukio ya mkuranga na Kibiti?

Maana kama hata kuelewa tu matukio hayo yalianza lini (unasema yalianza mara baada ya uchaguzi, wakati matukio hayo yalianza wakati wa utawala wa Kikwete, kabla hata ya uchaguzi wa 2015, kwa kuvamia vituo vya polisi, na kupora silaha) huelewi, sasa wewe unadhani una akili hata ya kuelewa au kukumbuka chochote?
 
Back
Top Bottom