Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya: JamiiForums na wanachama wake wanaongoza!. Lets Be More Proactive!

paskali nikuulize kidogo (don't take it personal) unaamini kabisa kwa roho safi pasina shaka kwamba huyo mkuu wa mkoa na huyo mwigulu wapo na nia ya dhati kupambana vita ya madawa kulevya? kuweka wasanii wawili watatu kina wema sepetu detention ndio kunakuaminisha hilo?
Kuna ma don ya unga yamekaa kinondoni,magomeni ,mbezi

Yeye anafuata celebrities tu

Hayupo serious na kwangu mimi naona ni kick tu
 
paskali nikuulize kidogo (don't take it personal) unaamini kabisa kwa roho safi pasina shaka kwamba huyo mkuu wa mkoa na huyo mwigulu wapo na nia ya dhati kupambana vita ya madawa kulevya? kuweka wasanii wawili watatu kina wema sepetu detention ndio kunakuaminisha hilo?
Safari ni hatua na dalili njema huonekana asubuhi.

Hii ni dalili njema, let's give them time.
Paskali
 
Wanabodi,
Kwenye hii vita ya madawa ya kulevya iliyopamba moto baada ya kupata chachu mpya toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda , nimepata fursa kupitia mabandiko ya wana JF wengi.

Kama serikali ingekuwa inatoa tuzo kwa taasisi mbalimbali zilizo mstari wa mbele katika vita hii, ni pamoja na Mtandao huu wa JamiiForums, umeweka thread maalum kupiga vita madawa ya kulevya, na kuifanya sticky.

JamiiForums most of the times JF tumekuwa very active as a passive whistle Blower, sasa tuwe more proactive kwa wana JF kujitokeza kumsaidia Makonda, Mwigulu na Jeshi letu la Polisi kusaidia any info we have kupitia michango ya wana JF humu. I don't know how we can achieve this, bali tusiishie kusema tuu, kama tunaweza kutenda, pia tutende no matter how little it might be, but let's do something.

Mfano hata tuki print tuu mabandiko kuhusu Madawa ya kulevya na kutoa Hard Copy 10 tuu, it's not nothing, it is something.

Hizo Copy 10 za kwanza zitue Kwenye meza za hawa wafuatao
1.Rais wa JMT
2.VP
3.PM
4.Waziri wa Mambo ya Ndani.
5.IGP
6.Director wa TISS
7.Director wa Immigration
8.Director wa PCCB
9.Director wa Tume ya Madawa
10. Paul Makonda.

Hongera sana, Mike, Max na wana JF wengine wote mnaochangia vita hii, let's keep fighting hata kama mchango wetu hauonekani, ila tunajiwekea akiba nzuri sana ya good karma ambayo ina thamani kubwa kuliko tuzo yoyote.

Nawatakia Jumapili Njema.
Paskali.

NB: Usisahau kupitia hii thread=>Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Pascal Mayalla Said;
Nikiwa mwandishi wa newsroom wakati huo nikiishi Ilala, nikapangwa kusafiri na Mkapa Sweden, US na UK, three days kabla ya safari majira ya saa 3:00 nikatembelewa na ugeni wa jamaa wawili, mwanamke na mwanaume. Wakajitambulisha na kunieleza nía ya ugeni wao.

Kiukweli nilishangaa jinsi walivyojua niko kwenye msafara, ndipo wakanijulisha mizigo yetu yote inapelekwa Ikulu siku moja kabla ya safari na haikaguliwi inasafirishwa under a diplomatic bag. Wakaniomba niwabebe parcel yao, kuwa ndiyo the safest way na kila siku ndio zao! . Fungu nililotajiwa sikuamini. Kiukweli roho ilinidunda, bulungutu limetolewa na kuwekwa mezani ni mshahara wa zaidi ya miaka 10 ya kiwango changu!.

Kiukweli niliogopa, what if itajulikana?!. Wakanihakikishia its never na wengine wote wanabeba! . Kiukweli niliogopa nikawaambia siwezi! . Jamaa walinishawishi sana mwisho wakakasirika na kuondoka kwa hasira huku wakinilaani nitakufa masikini!. Pia walinionya nikisema popote hata kwa mke wangu, wao watajua na kitakachonifika sitaweza kusimulia! .

Nikasafiri na msafara na kweli a day kabla ya safari mizigo ni Ikulu na siku ya kurudi inakabidhiwa hotelini unakuja kuipokelea Ikulu a day baada ya kurudi.

Kiukweli tukiwa huko majuu ndipo nikashangaa wenzetu wanavyofanya mi shopping ya nguvu, umasikini wa Tanzania unajulikana, mishahara ya serikali ya enzi hizo inatilisha huruma, lakini maofisa wadogo wadogo tuu wana má jumbo suitcases mawili matatu yamejaa vitu vya thamani, nikahisi usikute ni kweli! ,hivyo kuna umasikini wa baadhi yetu ni umasikini wa kujitakia. Safari zilizofuata nikataka kushawishika, roho ikakataa, bora kuwa masikini wa kutupwa with peace of mind luliko kuwa tajiri mwenye mashaka.

That was then, ndio maana kulipoibuka tuhuma hii kuhusu China, niliuliza swali hili.
Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!
Paskali


KWAHIYO MZEE WANGU PASKALI, INA MAANA ZILE SAFARI ZA JK ZOTE NJE YA NCHI, WASAIDIZI WAKE PALE TISS WALIKUWA WANAFANYA MAMBO, SASA NIMEGUNDUA KWA YULE BOSS WA TISS ALIYEUWAWA PALE AIPORT YA DSM NA WENZAKE WA TISS, SABABU ULIKUWA NI NINI?
JPM, UKISAFIRI SAFARI ZA NJE NA WASHIRIKA WAKO, KUWA MAKINI MH. JPM....!
 
Kuna uzi mmoja niliandika comment nilisema usalama wa taifa na polisi wanahusika na kuuza na kusafirisha madawa, kuna lijamaa lilinikomalia na kusema nitaishia segerea kwa kuwasingizia. Juzi Makonda kawataja polisi 12 pia kuna muuza ngada mmoja anamtumia mpaka mkubwa mmoja wa polisi na kumwambia kijana wako flani mpeleke sehemu flani anifanyie kazi yangu vizuri. Yupo rafiki yangu kaishia south afrika alikamatwa na yule dada mwenye makalio makubwa, Na yule aliekamatwa China (Jack) nilijua ataisha tu nilipomuona na kuna rafiki yangu mmoja muuza ngada mkubwa na lina mahela hatareee.

OMARY SANGA, MFANYABIASHARA JARIAKOO NI NANI HASA????
 
JamiiForums Ipo juu sana kwa kila jambo.

Cha ajabu na hovyo kabisa serikali hii ya ccm haitaki whistleblowers.

Badala source hizi serikali izitumie kufikia malengo MUJARABU wao nikutisha nakufunga midomo

Bwana mkubwa aachie watu waseme yeye afanyie kazi taarifa sio kutufunga na kututishia.

Mwigulu....mzigo huo hapo juu....natimu yako fanyia kazi acha kufungafunga Cdm na Cuf ....nikujipotezea weledi.
Wengi wenu mnataarifa za uongo, mnatanguliza majungu na fitna, kwa kuwa ww huna, yeyote aliyenacho kwako ni muuza dawa.
 
Ni kweli watu tupaze sauti, enough is enough, alafu watu waache siasa kwenye issue sensitive kama hizi ambazo zinahusu mustakabali wa vijana wa taifa hili. Tunamuomba muheshimiwa Mwigulu Nchemba na yeye ndiyo awe front kwenye hii vita, siyo anagwaya gwaya, wazalendo wa nchi hii wako nyuma yake.
 
JamiiForums Ipo juu sana kwa kila jambo.

Cha ajabu na hovyo kabisa serikali hii ya ccm haitaki whistleblowers.

Badala source hizi serikali izitumie kufikia malengo MUJARABU wao nikutisha nakufunga midomo

Bwana mkubwa aachie watu waseme yeye afanyie kazi taarifa sio kutufunga na kututishia.

Mwigulu....mzigo huo hapo juu....natimu yako fanyia kazi acha kufungafunga Cdm na Cuf ....nikujipotezea weledi.
Wanataka kuifungia JF,


Sadly!
 
Leo ndiyo itakuwa ushaamini kutokana na Kauli aliyeitoa jpm

Ova
Mimi naamini hii vita ina baraka za JPM, mimi naamini combination ya JPM, Mwigulu na Makonda mbona kitaeleweka tu!!

Madawa ya Kulevya yanawafanya watumiaji wawe kama mazombi!. hapana aisee, hayakubariki hata kidogo, lazima hii vita ipiganwe!!!

Napendekeza sheria itungwe, mtumiaji na msambazaji wote wapigwe risasi, hiyo itapunguza sana!!
 
Back
Top Bottom