Proud Patriot
JF-Expert Member
- Oct 13, 2010
- 224
- 10
visasi ni tabia ya kikwete, unajua waliko walio ingia kwenye ligi ya urais naye kutoka ccm??? Ni mwandosya tu yupo lakini baada ya kuonywa huko mbeya!!!!. Waulize akina sumaye, salim ahmed salim. Je waliowaunga mkono sumaye na salim? Nina ushahidi wa kada mmoja aitwaye nicodemus banduka alikuwa mkuu wa mkoa wa lindi 2005.
Banduka alimuunga mkono sumaye kilichompata akisimulia machozi yanatiririka. Nilikuwepo wakati kikwete alipokataa kumpa hata mkono mkuu wa mkoa wakati aliporudi lindi kushukuru. Nilikuwepo wakati anawaadressi mwenyekiti ccm mkoa, wilaya, wakuu wa wilaya na kumwacha mkuu wa mkoa.
Ninakumbuka alivyomleta sadick meck sadick kama mkuu wa mkoa bila kumpa taarifa banduka. Banduka alinyang'anywa gari njiani. Afisa usalama wa mkoa alimtoa kwenye nyumba ghafla.
Banduka alitoroka usiku kuepuka aibu ya ghafla.
Hata mitandao iliyopo ni kwa ajili ya kikwete. Mtandao wake ni kwa ajili ya kuendelea kuwaadhibu wabaya wake tena walio katika chama chake. Kauli za uv ccm bagamoyo na kwingine na matusi kwa wazee wa chama chanzo ni visasi vyake
hafai uongozi wowote hata katibu kata = kikwete ni mtu hatari.
umenishtua aisee, bora mungu amgeuze trekta tu wakamlimie mashambani huko!