Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Shida iko wapi hata kama atajipatia kopato kwa kazi yake?
Kama unaona hivyo acha kusoma, sisi tutachangia tu kama ataamua hivyo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Fact, ameamua kupoteza muda wake hata Kama ni uwongo ni sawa tu, hata Kama atataka tuchangie vocha pia ni sawa, sion Kama kuna sehem kavunja sheria.Kama funzadume utaona hapa sio mahala pako pita kimyakimya,Sio mbaya mtu akijiingizia kipato kupitia JF mana hajamwibia mtu tunachanga kwa hiyari.
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia. Itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia.
 
Wachawi ni viumbe wa kuogopa kuna jamaa mwalim madrasa amefungwa jela miaka thelathini michongo wametoa wachawi wametengeza kesi ili ili aonekane kabaka tena wamemfanyia hayo baada ya kuwakatalia wachawi lengo lao yule ostadh akubali kila mwaka jamaa wapate kijana mmoja chanika hiyo
Hiii ilimtokea Mganga mmoja hivi kijijini kwetu ambaye alikua anatoa siri za wachawi pale kijijini

Alivyotangaza kuwa kesho nitaanza kutoa viumbe vya ajabu kwenye majumba ya watu hivyo kama kuna mtu ndugu yako alikufa na mkamzika mtamuona

Basi wachawi walivyosikia hivyo wakamtengenezea kesi ya mauaji cha ajabu askari walivyomfunga pingu zikawa zinakatika

Hadi jamaa anaachiwa uganga wake ukaishiwa nguvu na pale kijijini akahama kijiji kikapoa sana, asee wachawi watu wabaya sana.
 
Habari ndugu zangu,

Kwa kuwa leo nimetulia ngoja niwaeleze visa nilivyowahi kuviona katika safari yangu ya mwisho wa mwaka nilipomtembelea ndugu yangu ambae ni mganga.

Kwanza kabisa mimi tangu awali siamini mambo ya uchawi wala sina imani juu ya ulozi na uwepo wake hivyo ndugu yangu pamoja na kufanya shughuli hizo na kuendesha maisha yake lakini nilijua ni vitu ambavyo havipo.

Siku moja alfajiri alijiwa na ugeni wa bibi kizee na mjukuu wake msichana wa kama miaka 28 hivi kilingeni kwake, pamoja na kwamba siamini ushirikina lakini sikuonyesha wazi nilipokuwa pale ili niwe karibu nipate kujua undani wa haya mambo hivyo nikawa naingia kilingeni kwake kwa utiifu kuona utendaji na matokeo.

Na pia ni vigumu kumdharau kwa sababu amewekeza kuliko mimi msomi

Basi ndugu zangu, yule msichana alikuwa amedhoofu sana ishara kuwa ni mgonjwa wa muda mrefu, ramli ikaangaliwa na wakaambiwa mengi ambayo walikubaliana nayo mfano kama vile siku yalipoanza maradhi, namna anavyojisikia na chanzo cha maradhi.

Wakaandikiwa vifaa na kuondoka ili wakavitafute, cha ajabu ilipofika saa kumi jioni yule bibi akarudi peke yake na kumuuliza mganga kama anamkumbuka? Akajibiwa "Naaam si ulikuja asubuhi na mgonjwa, vipi maendeleo yake? Bibi akajibu sikuletwa na maendeleo yake ila nimekuja kukuomba akija usimuague na kwa kuwa ulimpa namba basi akikupigia mwambie umesafiri na kuhamisha kilinge kabisa!

Mganga akasema "kama hutaki aaguliwe ulimletea nini kwangu? Bibi akasema "kama nisingemleta ingewezekana vipi nije tuongee kama hivi mwanangu? Nimemleta nipajue na tujuane ili nije tuongee kama hivi, maana nisingemleta angekuja mwenyewe tu maana si unajua ameshasifiwa kwako".

Mganga akauliza nini lengo lako na ikiwa yule ni mjukuu wako kama ulivyosema asubuhi na kunisisitiza mbele yake nimuague apone kwani mmemaliza tiba zote na haponi?

Ajabu hapo yule bibi akavuta pumzi ndevu na kutabasamu huku akimsogelea kidogo karibu mganga na kusema "Enheee sasa hapo umeuliza swali la kiutu uzima, najua ki umri wewe ni mdogo sana kwangu ila kwa kuwa umeingia kwenye kazi hii basi wewe ni mtu mzima mwenzetu. Mimi nipo kwenye ngoma zetu hizi za utu uzima za usiku, unanielewa?
Mganga akajibu kifupi "endelea tu..

Bibi akaendelea..."yule ni mjukuu wangu kabisa na mama yake nilimtafuna mwaka tisini na mbili na nikapata daraja nzuri tu kwa kuanzia, ila sasa huyu binti ile ni kazi yangu mimi hivyo muda si mrefu nitaimaliza naomba usinirudishe nyuma! Kwani akifa leo yule basi mimi nitakuwa katika daraja nzuri sana na kilemba cha ngazi sita, nitakuwa na mimi nakaa kwenye kiti cha enzi na kutoa hukumu mbali mbali nimechoka kudharauliwa na watoto wadogo!

ITAENDELEA NGOJA NIPATE CHAKULA KWANZA...

NB: Hapa naeleza niliyoyaona kwa macho yangu na hakuna tangazo la uganga na sitahusika na hayo na pia sipo kuaminisha watu imani ya giza hivyo tujikite katika mikasa pekee.
Daaah noma
 
Wachawi ni viumbe wa kuogopa kuna jamaa mwalim madrasa amefungwa jela miaka thelathini michongo wametoa wachawi wametengeza kesi ili ili aonekane kabaka tena wamemfanyia hayo baada ya kuwakatalia wachawi lengo lao yule ostadh akubali kila mwaka jamaa wapate kijana mmoja chanika hiyo
Duh
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia.itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia
Pole sana mkuu tuna kusubiri
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia.itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia
Pole Mpendwa.. Zidisha Maombi Mungu yu pamoja nawe atakupigania..
 
Nilimuuliza swali hili hili, akanijibu angemtibia angekuwa kaanzisha vita kubwa wangeitana jeshi kupambana naye, naye hakuwa na sababu ya kupambana vita isiyomhusu. Akanipa kisa kilichomtokea miaka miwili kabla, aliletewa mgonjwa yani mke alimleta mume akiwa mgonjwa sana jamaa anadai akakaa pale anamtibia. Anasema kuna siku akaamka kama anaumwa yani kama kachanganyikiwa anagawa gawa nguo anatoa wosia kwa watoto wake, ilikuwa ijumaa. Anasema baadaye akaja kijana akamwambia anaitwa na mzee yuko kwenye gari kule chini. Alipoenda akaambiwa aingie kwenye gari, mzee kuingia akamkuta mzee flani.
Eti akamuuliza kwanini unataka kuniharibia kazi yangu, huyo ni mwanangu na mimi ndiye nataka kumtoa kwa ajili ya biashara zangu. Jamaa akamwambia ashakula pesa lazima amalize kazi, mzee akatoa chupa na glass nyuma ya kiti cha gari akamwekea maji akamwambia kunywa nijue kama unataka pambana nami au utaachana naye.
Jamaa akanywa nusu glass kumaanisha kuwa hataki shari, wakaachana, alivyofika kwake akamwambia yule mama na mme wake kuwa ugonjwa umemshinda hawezi kuutibu. baadaye akakusikia yule jamaa alifariki.
Asee haya mambo yapo dunian kumbe?
 
Back
Top Bottom