Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Uganga wa kienyeji na uchawi wote ni WACHAWI, yaani ana uwezo wa kumtibu af mtu anamwambia ni nyama yangu mwache afe unakubali kuacha mtu afe.
Ukiona mganga kakubali mteja wake afe huyo sio mganga ni mamluki anaeendekeza njaa.

Mganga wa kweli lazima amtibie huyo mgonjwa mpaka apone kama huo ugonjwa upo ndani ya uwezo wake hakuna mchawi atakaempa pesa akaikubali kisa tu huyo mgonjwa aache kumtibia ili afe wamle nyama.
 
Inaendelea....SEHEMU YA NNE

Huyu mke wa mganga nae ana majini nae ingawa hajishughulishi sana na mambo ya uganga zaidi ya kutumwa moto na vitu vidogo vidogo tena kwa kufanya kuitwa, ila siku hiyo majini yake yalikuja kwa uchungu baada ya kuona mganga amezidiwa.

Mke wa mganga akasema njia ya kumsaidia kaonyeshwa hivyo akaingia kilingeni na kuchukua dawa kadhaa za maduka ya dawa za asili na kuchanganya na dawa fulani ya kwenye tunguri na kuchanganya na unga wa sembe na kisha kumpaka mume wake baadhi ya sehemu na nyingine kumnywesha.

Baada ya muda akapata nafuu na kunyanyuka na hapo tukaanza kumcheka kuwa kawezwa, na yeye akacheka kidogo na kusema wale wamekuja kiume lakini moto ukokwe arudishe majibu muda huo huo.

Hapo tukafanya haraka kukoka moto na kuuweka katika chungu maalum anachokiita Bukhuri shari, akabadili nguo na kuvaa nyekundu tupu hadi kilemba na kuchukua tunguri yake ambayo ki umbo ni kubwa kuliko zote alizonazo na tunguri hiyo kipindi anaitengeneza nilikuwepo na ni mpya mwenyewe anaiamini sana.

Tunguri hii alipokuwa anaiunda alimchoma bundi aliyeuwawa na makunguru na majivu yake akachanganya unga wa mti uliopigwa na radi, mti wa nyumba ambayo ina maiti ndani, kisiki kinachokwaa watu njiani, mzizi uliokata njia, unga wa kichwa cha nyoka na vitu vingine pamoja na damu ya kuku wawili wa rangi maalum na ule ulimi wa tunguri pia ni miongoni mwa miti yenye siri kubwa kulingana na maelezo yake.

Naam kwa mara ya kwanza nikaona tunguri hiyo imeshikwa kwa jazba huku akiuelekea moto na kusema leo naua kuanzia walioshiriki na mpaka vilivyomo katika nyumba zao! Akaanza na kutia ubani na kusema na Waalim wake! "Enyi majini nimechokozwa kama mlivyoona, hamkunipa uganga nije niteseke...mmeniachisha shughuli zangu za maana mkanitia kichaa ili leo yanikute haya nife? Sasa leo naangamiza watu na kama mnaona huruma na kuona ni kufuru kaeni pembeni, niacheni na wakulungwa wa bara nitende malukazi....

Inaendelea....
Duh, mwamba anayepiga biti hadi majini, hatari sana huyu mwamba

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹
 
Inaendelea.... SEHEMU YA PILI

Baada ya yule bibi kusema hayo akanyamaza akisubiri majibu ya upande wa pili.

Moyoni mwangu nilidhani rabda mganga atamfukuza yule mchawi au hata kugombana nae kutokana na hizo hila zake za kishenzi, ila kinyume chake mganga akatulia kidogo na kisha kumuuliza yule bibi, "unafanya hayo yote ili kuutumikia uchawi! Uchawi una faida gani?

Bibi akatabasamu na kujibu kwa hisia za furaha "baba uchawi una faida kubwa mno mwanangu kuzidi hata huo uganga wenu, mimi hapa nilipo nina pembe inakaa ziwani...inakusanya pesa za biashara za mji mzima kwa njia ya chumaulete, hebu fikiria ni wangapi ambao hawajazindika shughuli zao na wananichumia mimi? Bado sijagusia misekule ambao hunisaidia na kunizalishia mashambani kwangu.

Mganga akauliza tena kwa kama dharau fulani hivi, "sasa kama mna nyenzo hizo mbona mnakufa masikini na kuishi katika nyumba duni, kula yenu tu ni tabu achilia mbali mavazi yenu?

Ndugu msomaji, huyo bibi alikuwa amevaa khanga tofauti kuukuu na chini amekuja na ndala tofauti zilizoshonwa shonwa hivyo yale maongezi yake yalishangaza kidogo.

Safari hii bibi alicheka kwa kama kebehi na kumjibu mganga, "kumbe mwanangu bado wewe ni mtoto mdogo sana hujui kitu! Sisi fahari yetu siyo mchana ila ni usiku! Kwenye mwembe mkubwa kikaoni ndiyo utamjua tajiri ni nani kulingana tu na usafiri na zana za gharama atakazo ingia nazo...wapo wanaingia na ungo, wanaoingia na Fisi, wanaokuja kwa ufagio na ndege ya watu wengi nk na pia kuna watu wana pembe wamenunua zaidi ya milioni ishirini na hiyo ikiwekwa chini huioni na hata ukionyeshwa hutaweza kuinyanyua na uganga wako wote.

Najua nyinyi ufahari wenu ni makazi, mavazi na kula ila sisi raha yetu ipo sehemu tofauti kabisa na nikujuze tu usiku ni raha sana mwanangu na sasa nikipata hiki cheo nauelekea ukubwa sasa na kiti changu kitabebwa juu juu na katika mji nitaheshimika mno.

Maongezi yalifika mpaka muda wa magharibi na adhana ikalia...hapo yule bibi akasema naondoka nawahi kusali lakini ufanye hivyo nilivyokwambia au kama shida ni pesa nikupe mimi hilo fungu ulilopanga akupe bora tu usimuague.

Bibi wakati akisema hayo alifungua fundo kwenye nguo yake na kuonekana noti nyingi ambazo pengine zinaweza fika hata laki mbili au zaidi! Mganga akasema; sihitaji pesa ila nikuulize jambo? Sasa unakwenda kusali ili iweje ilihali wewe ni mchawi? Huoni unazidi kukufuru?

Bibi akasema huku kasimama anataka kuondoka "unapoingia katika uchawi masharti yake inatakiwa uvae kofia mbili, moja ya uchawi na nyingine ya Imani...hapa kwenye imani unaweza kushika dini sana uwe Mkristo, Muislam au dini yeyote na ukishindwa hilo basi kuwa na imani ya kupenda watu sana na kujitoa...hii inasaidia hata akitokea mtu mmoja akisema wewe ni mchawi, watatokea kumi watakao pingana nae na kuwa upande wako.

Mganga akasema kwa hasira; tafadhali ondoka usije ukadhurika, mimi ni mganga wa majini hivyo sirubuniwi na yeyote bali nawafuata wao walionipa uganga...ondoka haraka kabla sijachoma ubani ukapigwa na chini sasa hivi maana hawataki mambo machafu na ya kipumbavu namna hiyo!!!


NAENDELEA KUANDIKA HIVI NDUGU ZANGU...
Huyu ndie real mganga
 
Jamani mganga wa kweli ni mungu tu.. ukisali kwa moyo wote hakuna mchawi anaeweza kukugusa. Na sio lazima uende kanisani.. Mimi nina mwaka wa pili sasa siujui mlango wa kanisa. Ila huwa naamka saa tisa usiku nina tubu na kusali namuomba Mungu mahitaji yangu. Namuomba anilinde pia. Hakika mambo yangu yanaenda vizuri kabisa. Wachawi wenyewe wananiogopa. Tusali sana jamani mungu yupo na anajibu maombi tukimuomba kwa moyo wote.
 
Jamani nina miaka mingi sijalog in huwa nasomaga tu ila huu uzi umenifanya nimelia sana acheni tu hii dunia.itoshe tu kusema nateseka lakini maombi yamenifunilia yalio sirini naonyeshwa kabisa anayenitesa. Ukiniona huwezi jua mateso nayopitishwa hapa nalia nitahadithia nikitulia
Pole Sana, itoshe kusema tumtangulize Mungu kwa kila hatua tunayopiga hawa waliokaribu yetu ndio wanaotumaliza sababu wanatujua undani mtu mbaya hatoki mbali na wewe...Dada yangu aliyumba mpaka kuamua kuachika bila shurti sababu ya hizi mambo mbaya zaidi iliathiri familia karibu yote sababu ya hivihivi kujuana machimbuko ya Koo na familia ila Mungu mwaminifu kajikabidhi kwake ndie anayemfunulia mengi kila iitwayo siku
 
134 Reactions
Reply
Back
Top Bottom