Visa na Vibweka vya Sumbawanga. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa na Vibweka vya Sumbawanga.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bujibuji, Jun 23, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Hizi ni stori za Sumbawanga, tumekuwa tukizisikia sana lakini hatujazithibitisha.
  Miongoni mwa stori hzi ni kwamba kuna mkuu mmoja wa mkoa aliteuliwa enzi za Nyerere. Alipoenda kujitambulisha kwa wazee kwenye mkutano ulio fanyika kwenye ukumbi wa almashauri ya mji, akashangaa wazee wana tundika makoti yao hewani na hayaanguki.
  Jamaa aka resign ndani ya masaa 24
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kuna mizimu ya Katabi na Katavi watu wamekutana nayo sana kwenye mbuga ya Katavi ati Sumbawanga na Mpanda. Ukikutana na mizimu hii unaweza kuwehuka au kufa kabisa.
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  jamaa mwenyewe aliyeteuliwa na Nyerere ni huyu
  [​IMG]
   
 4. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hizi story nilikuwa nazisikia sana kama;

  1.Jamaa aliamua kuwekeza sumbawanga mjini, akaamua kujenga, akanunua tofali,mbali na site, alikodi vijana wambebee matofali ya kuchoma kupeleka site, kesho kuamka anajikuta kaamkia site, hoi mchafu kishenzi kumbe yeye mwenyewe kabeba tofali.

  2.Nyingine jamaa alikataa mimba ya binti ikawa kizaa zaa.

  Nadhani story nyingi zilikuwa ni za kutunga, maana toka kuwe na mawasiliano ya uhakika hatusikii tena hizi legend. Nyingi zilikuwa za zamani na zilikuzwa zilipokuwa zinahadithiwa, kwani nyingi zinafanana ila zinatofaitiana kwa masimulizi
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  WENGI wetu tukisikia jina Sumbawanga ni
  wazi kuwa fikra zinakwenda moja kwa
  moja kuwa ni uchawi, ushirikina na pengine
  kifo. Ukweli ni kwamba ni jina lililotoholewa
  kwenye neno Sumbu wanga, likiwa na
  maana ya tupa uchawi , na lilianzishwa na
  mtawala mmoja wa zamani wa eneo hilo
  aliyeitwa Mwene Ngalu.
  Sumbawanga ni makao makuu ya mkoani
  Rukwa, uliopo Nyanda za Juu Kusini
  Magharibi mwa Tanzania. Mkoa huu
  unapakana na nchi za Jamhuri ya
  Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Zambia,
  Burundi na mikoa ya Tabora na Mbeya na
  una jumla ya watu milioni 1.5, kwa mujibu
  wa sensa ya mwaka 2002. Ulianzishwa
  rasmi mwaka 1972.
  Mkoa huo una makabila mbalimbali ila kabila
  kubwa na la asili ni Wafipa ambao ndiyo asili
  ya jina Sumbawanga, mji ulioanzishwa
  mwaka 1803, chini ya chifu wa kwanza wa
  Ufipa aliyeitwa Kapufi ambaye alitawala
  miaka ya 1885. Chifu Kapufi wa Kwanza
  alianza milki yake ndani ya Ufipa yote na
  makao yake makuu yalikuwa Kijiji cha
  Kisumba nje kidogo ya mji wa Sumbawanga.
  Mke wake aliitwa Mwene Wakulosi ambaye
  walijaliwa kupata watoto watatu, wa
  kwanza wa kiume na wawili waliofuata wa
  kike ambao ni Mwene Kiatu wa pili aliitwa
  ‘Mwene Ngalu Chisichaafipa’ (jina la utawala)
  na wa tatu aliitwa Mwene Mwati.
  Baada ya kifo cha Chifu Kapufi wa Kwanza,
  milki ilitawazwa kwa mwanae wa kwanza,
  Mwene Kiatu ambaye alihamia kijiji cha
  Lwiche ambako kwa mila na desturi za
  kiutawala, ukitawazwa kuwa chifu ni lazima
  uhame na kwenda kuanzisha kijiji chako
  kama alivyofanya Mwene Kiatu.
  Katika kipindi chake cha utawala wa eneo la
  ufipa, chifu Mwene Kiatu hakujaliwa kupata
  watoto na alipokufa, milki ilichukuliwa na
  dada yake, Mwene Ngalu ambaye ndiye
  mwanzilishi wa Sumbawanga.
  Chifu Mwene Ngalu alikuwa mtu mwenye
  upendo na hakupenda uchafu wa aina
  yoyote ukiwamo uchawi, hivyo kabla ya
  kuingia kijiji cha Sumbawanga
  alichokianzisha, aliwataka wananchi
  waliomfuata watupe uchafu wote kwenye
  mto Lwiche pamoja na uchawi kisha
  waingie wakiwa safi.
  Kutokana na imani hiyo watu walitupa
  uchawi wote na taka nyingine kisha
  wakaingia kijiji cha Sumbawanga wakiwa
  wasafi. Aliyekiuka amri hiyo na kuvuka mto
  Lwiche kutaka kuingia kijiji kipya cha
  Sumbawanga alikufa katika mto huo.
  Hapo ndipo ikawa asili ya Sumbawanga na
  kijiji kikawa na watu walio wasafi na
  hakukuwa na matatizo na utawala wa
  Mwene Ngalu. Alipendwa na kila ilipotokea
  ishara ya matatizo ndani ya ufipa ilikuwa
  rahisi kutatuliwa kwa kuwa Chifu Mwene
  Ngalu aliomba na majibu yalipatikana
  haraka, hasa kwa imani ya usafi waliokuwa
  nao.
  Hata hivyo Chifu Mwene Ngalu alijaliwa
  kupata watoto saba ambao wote aliwazalia
  katika nyumba yake ya utawala iliyojengwa
  kwa kipindi cha miaka miwili katika mwaka
  1918 hadi 1920 chini ya usimamizi wa
  Mabruda wa dhehebu la Roma yaani
  wakatoliki ambao walikuwa Wajerumani.
  Nyumba hiyo hivi sasa imebomoka na
  limebaki gofu ambalo kwa nje kuna sehemu
  ya makaburi yanayotumika kuzika kizazi cha
  utawala huo, na jambo la ajabu kwenye
  gofu hilo wapo nyuki waliojenga kwenye
  pango na wapo kwa muda mrefu tangu
  kipindi cha uhai wa baadhi ya watawala wa
  kizazi hicho.
  Watoto wa Mwene Ngalu ni Maria wa Ngao,
  Joseph Kapufi wa Ngao, Thadeo wa Ngao,
  Teresia wa Ngao, Jacob wa Ngao, Victoria
  wa Ngao na Antony wa Ngao, ambao baada
  ya kifo cha mama yao, mtoto wa kwanza
  Joseph wa Ngao alitawazwa kuwa Chifu wa
  kizazi hicho na kupewa jina la Joseph wa
  Ngao-Kapufi wa Pili.
  Chifu huyo aliyejaliwa watoto wanne, ambao
  ni Olanda Joseph, Adolf Joseph, Veneranda
  Joseph na Yovita Joseph na alipofariki dunia
  nduguye ambaye ni mdogo wake wa
  mwisho, Antony wa Ngao alitawazwa
  mwaka 1989, kuwa Chifu wa Ufipa na
  kupewa jina la Kapufi wa Tatu.
  Kapufi huyo wa tatu, Antony wa Ngao,
  alitawala ufipa tangu mwaka 1989 hadi
  Desemba 6 mwaka jana alipofariki dunia na
  kuzikwa kwenye eneo la makaburi ya kizazi
  cha utawala huo, karibu na jengo la Mwene
  Ngalu ambalo hivi sasa limebaki gufo tu.
  Katika kipindi cha utawala wake, Chifu
  Kapufi wa Tatu, alijaliwa kupata watoto
  watatu ambako mkewe wa kwanza alijaliwa
  kupata mtoto mmoja wa kike aliyeitwa Ntalu
  na mke mdogo alijaliwa kupata watoto
  wawili wa kiume ambao ni Oscar na
  Apolinary. Hata hivyo baada ya kifo cha
  Kapufi wa Tatu, hivi sasa ukoo huo wa
  kichifu uko kwenye mchakato wa kutafiti
  mrithi wa kiti hicho.
  Msemaji wa familia ya akina Kapufi Adolf
  Joseph (61), ambaye ni mtoto wa Chifu
  Joseph wa Ngao wa Pili, anasema jinsi ya
  kumpata mrithi huyo ni kwa njia ya
  kuwashirikisha wazee wa mji huo (wa
  zamani) walio hai hivi sasa pamoja na wale
  wa vijiji vya karibu kisha kuteua majina
  kadhaa na kuyachambua kupata
  anayestahili.
  Anasema jina la mrithi likipatikana sherehe
  za kumsimika kuwa Chifu wa kabila hilo
  huanza kufanyiwa maandalizi, na kwa
  kawaida hufanywa nje ya mji kwa
  kutengeneza sehemu maalumu ya
  kumpitishia ambayo huiita mzingo. Pia
  huvuka mto Lwiche kwa imani kuwa ni
  moja ya hatua za kudhihirisha kiwango cha
  usafi wake kabla ya chifu mtarajiwa
  kutawazwa.
  Baada ya sehemu hiyo kukamilika
  kutengenezwa chifu mtarajiwa hupitishwa
  kwa nyuma kuingia kwenye mzingo huo
  huku akipuliza filimbi tatu, ya kwanza
  ikikataa kulia hupewa ya pili nayo ikigoma
  hupewa ya tatu ambayo nayo ikigoma ni
  dalili kuwa hafai kuwa chifu, hivyo
  huenguliwa na kutafutwa mwingine.
  Adolf anasema ikiwa filimbi moja au mbili
  zikilia na moja kugoma watampa utawala
  wa muda huku wakijiandaa kumtafuta chifu
  mwingine, kwa imani kuwa filimbi zote
  lazima zilie kwa sababu ni ishara ya sifa
  njema za utawala za kiongozi anazopaswa
  kuwa nazo ndipo apewe mamlaka.
  Wakati mchakato huo ukiendelea, wa
  kumpata mrithi wa kiti hicho, mavazi ya
  Chifu Kapufi wa Tatu, Antony wa Ngao
  amepewa Vicent Kafumu ambaye ni mjukuu
  wa Chifu Mwene Ngalu kwa mzaliwa wake
  wa kwanza aliyeitwa Maria wa Ngao.
  Pamoja na hayo yote pia enzi za utawala wa
  viongozi hao walitumia silaha mbalimbali
  ambazo hadi leo baadhi yake zimehifadhiwa
  ili mtawala ajaye akabidhiwe kwa ajili ya
  kudumisha mila. Zana hizo ni upinde
  (ulapwa), mishale (ncheto), fimbo (wasi),
  mkuki (ilawa) na chombo cha kubebea
  mishale (untontowaancheto). Silaha
  nyingine ni shanga (inkasi) zinazovaliwa
  mikononi na shingoni kwa chifu, kiti cha
  miguu mitatu (kisumbi) na vazi la kujifunga
  kiunoni na mabegani (seketa) ambayo
  husukwa kwa pamba.
  Anasema mabadiliko ya dunia na teknolijia
  na mapinduzi ya kilimo kwa kiasi kikubwa
  zilibadilisha mtazamo na fikra za wakazi wa
  Sumbawanga ambako muingiliano wa watu
  ulipoanza imani ya uchawi na ushirikina
  zilipungua na watu wakaingia katika
  shughuli za uzalishaji mali ingawa baadhi
  yao wanaendelea na ushirikina kama zilivyo
  sehemu nyingine nchini.
  Mabadiliko hayo pia yalipunguza nguvu ya
  kuabudu mizimu iliyokuwapo hapo awali
  kwa kuwa misitu mingi ilifyekwa kwa ajili ya
  shughuli za kilimo na ufugaji hivyo, imani ya
  kuwapo mizimu iliondoka kwa asilimia
  kubwa na watu wakabakia kuabudu katika
  nyumba za ibada kufuatana na imani ya dini
  zao, anasema Adolf.
  Hata hivyo bado kuna sehemu au vijiji
  vyenye kuendelea kuamini mizimu na
  ushirikina kama vile kijiji cha Chipu kilicho
  kilomita kama 30 kutoka Sumbawanga mjini
  na vijiji vya Milanzi na Kalambo ambavyo
  bado imani ya uchawi na vitendo vya
  kishirikina vinaendelea kwa baadhi ya
  wakazi wake.
  Kwa kijiji cha Milanzi baadhi ya wakazi wake
  hutumia mapango yaliyo kwenye mlima
  uitwao Itwelele kwa kufanya matambiko na
  mambo mengine ya kishirikina kwa imani
  kuwa mizimu iliyopo huko huwasaidia
  kutekeleza mahitaji yao na kumdhuru mtu
  au watu waliotenda makosa na kuyakana.
  Adolf anasema hilo siyo tatizo kubwa kwa
  sababu hakuna anayemdhuru mgeni
  anayeingia mkoani hapo kwa kufanya
  shughuli zake kama vile biashara au kilimo.
  Ila kwa wale ambao hawajafika
  Sumbawanga hudhani kuwa huo ni uchawi
  na ushirikina tu, dhana ambayo si ya kweli
  kwa kuwa maendeleo yanayopatikana
  katika karibu makabila yote nchini hivi sasa
  yapo pia Sumbawanga
   
 6. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Makala ndefu lakini nzuri, nimeipenda na asante kwa kutujulisha historia ya Sumbawanga na watawala wake wa jadi.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Kama uliamini wachawi na wazee vikongwe,
  Simbeye atayabadili mawazo yako. Anasema
  uchawi aliurithi kutoka kwa babu yake, na
  akiwa na miaka kumi na nne alikuwa
  mchawi maarufu mjini Sumbawanga
  alikozaliwa mwaka 1961. Msikie: " Hata
  masomo yangu yalikatizwa na safari za kila
  mara kwenda kuzimu na kurudi duniani"
  Pengine hiyo ni nzito kwako kama
  ilivyokuwa kwa mwandishi wa habari hizi
  alipotembelewa na Simbeye katika Ofisi za
  GTV Nairobi Kenya. Tulipotaka kujua
  kwamba Kuzimu alikuwa akienda kwa
  usafiri upi? Yeye alijibu: "Mimi unayeniona
  hapa, nilikuwa na uwezo wa kujibadili kuwa
  chochote. Ningeweza kujibadili niwe Nyoka
  ama mbuzi ili mradi niwe mwepesi kwenda
  kuzimu bila Mke wangu Mrs. Medhodia
  Muzare kujua." "Wao wangeona mbuzi ya
  jirani shambani, na wakijaribu kuifukuza
  inapotea bila wao kujua imeelekea wapi."
  Kwangu safari ya Kuzimu ilikuwa imeanza."
  Maneno ya kuzimu hayakunivutia sana kama
  pale aliposema kwamba wateja wake
  walikuwa wengi ni Wahubiri. "Kazi yangu ya
  uchawi sikuwa naifanya kinjaa njaa."
  "Wateja wangu walianzia mawaziri
  wabunge na hata wahubiri walitaka nguvu
  kutoka kuzimu ziwasaidie kujaza makanisa
  yao." Hata mimi nilishawishika kama wewe
  kuuliza anitajie wahubiri hao. Alisema: "Japo
  sasa nimeokoka na kujiunga na mhubiri wa
  kike Joyce Wairimu Maina, haitakuwa busara
  kwangu kuwataja wateja wangu wa
  zamani, lakini wengi walikuwa wakija
  niwasaidie uchawi wa kuangusha watu
  wanapoombewa ionekane kwamba ni
  nguvu za Mungu."Kwa Simbeye anaedai
  Kaokoka, Tena chini ya Mchungaji Joyce
  Wairimu Maina wa Kericho ambaye kanisa
  lake limefurika watu wanaotaka kumuona
  Mchawi kutoka Tanzania, Halafu uangalie
  ibada kanisani hapo inapoendeshwa,
  Mambo yote aliyokuwa akiyafanya wakati
  akiwa mganga wa kienyeji, sasa
  ameyageuzia kwa Yesu, utashawishika
  kusema bado Uganga wa kienyeji
  umehamishiwa kanisani. Lakini mwenyewe
  anadai:"Hii tunayoifanya kanisani kwa Mama
  Joyce Maina ni tofauti na ile inayofanywa na
  wachungaji niliokuwa nikiwauzia uchawi."
  Tena wahubiri waliokuwa wakija kununua
  uchawi kwangu ni wale walioajiriwa na
  Wanawake Matajiri walioacha mabwana zao
  na kuanza mradi wa kuhubiri. Hao ndio
  hununuliwa dawa za kusababisha miujiza
  na wanaifanya hiyo kama kazi nyingine."
  "Isitoshe Wamama hao matajiri hununua
  dawa za kuwafanya wahubiri vijana
  wakubali kuwaoa." "Kuna vijana wengi
  walioolewa na wamama hao na sasa
  huduma zao zimetekwa nyara na wamama
  hao na huwatumikisha kama watumwa.'
  "Asubuhi mchana na jioni lazima wahubiri
  na kufanya miujiza FEKI ili waumini watoe
  pesa ambazo huchukuliwa na wamama hao.
  ' Wahubiri hulipwa kidogo, na kununuliwa
  mavazi ya kuvutia washirika.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mizimu hiyo ni Katabi na mkewe Wamwelu, inasemekana mpaka sasa huwa wanaonekana katika mbuga ya Katavi.
   
 9. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  source???
   
 10. senator

  senator JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Visa na vibweka vya sumbawanga!!
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sumbawanga si kwa Pinda?
   
 12. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sumbawanga si kwao Pinda?
   
 13. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Alienda mkuu mwingine,yeye kidogo alikuwa njema,akiwa mkutanoni walimfanyia mchezo huo huo wa kutundika makoti hewani naye akajibu mapigo kwa kutundika lake pia hewani.Baada ya kikao,wale wazee walichukua makoti yao lakini yule mkuu alipotaka kuchukua koti lake akagundua limeliwa na mchwa!
   
 14. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33

  nakumbuka miaka ya 2005 mwishoni iliwahi kutangazwa kuwa HUKO SUMBAWANGA mwewe alionekana angani akiwa amenyakua ng'ombe KAMA ANAVYOWANYAKUA VIFARANGA! SIKUFUATIKIA ZAIDI KUTOKANA NA UKWELI KUWA NILIKUWA SHULE NJIA ZA HABARI ILIKUWA ADIMU KIDOGO NA MUDA ULIKABA! KAMA KUNA MTU ALISHAWAHI KULISIKIA HILO ATUJUZE ZAIDI
   
 15. Mpendwa

  Mpendwa Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana shida gani?? kikao kikiisha anapata posho zake!!!!!Pia siku hii alikuwa akimuwakilisha waziri mkuu kwa maana waziri mkuu hakuwepo siku hiyo ya tarehe 21 bungeni!!Mwamsheni mumuulize swali la pupa kwa pupa (papo kwa papo) ujionee majibu yakeMf. Mbona unalala bungeni? Jibu la kwanza mimi sijalala, nasikuliza wachangiaji kwa umakini sana, kwanza nani kukwambia unipige picha? mara kofi, ngumi, mara umeliwa sikio!!!!!!!!!This is Mr Tyson bwana!!!!
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  chilli or tomato? Utapenda ipi?
   
Loading...