Virusi ya corona: Afrika huenda ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa corona - yaonya WHO

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Afrika huenda ikawa kitovu kipya cha mlipuko wa virusi vya corona, Shirika la Afya duniani WHO limeonya.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la visa vya ugonjwa huo wiki iliopita.

Kumekuwa na zaidi ya visa 1000 na zaidi ya maambukizi 18,000 kote barani Afrika kufikia sasa , ijapokuwa viwango hivyo viko chini zaidi ya vile vinavyoonekana katika baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani.

Shirika la Afya Duniani WHO linasema kwamba virusi hivyo vinaonekana kusambaa katika maeneo ya mashambani.

Pia limesema kwamba bara hilo halina ,mashine za kutosha za kuwasaidi wagonjwa kupumua ili kukabiliana na mlipuko huo.


Mkurugunzi wa shirika hilo barani Afrika Dkt Matchidizo Moeti, aliambia BBC kwamba shirika hilo limeshuhudia kuenea kwa virusi hivyo kutoka miji mikuu hadi mashambani katika mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria, Ivory Coast , Cameroon na Ghana.

Amesema kwamba kwa sasa wanaangazia kuzuia badala ya kutibu virusi hivyo kwasababu mataifa ya Afrika hayana uwezo kuwatibu wagonjwa wengi wa virusi vya corona.

''Tunataka kupunguza kiwango cha watu ambao wanafikia kiwango cha kuhitaji mashine za kuwasaidia kupumua katika chumba cha wagonjwa maututi , kwasababu tunajua kwamba vifaa hivi ni vichache kwa kiwango chochote miongoni mwa mataifa mengi ya Afrika'', alisema.

Nataka kusema kwamba suala la mashine za kusaidia watu kupumua ni mojawapo ya changamoto kubwa ambazo mataifa hayo yanakabiliana nayo.

Kwa wagonjwa walio katika hali mabaya zaidi wakiugua ugonjwa wa corona, upatikanaji wa mashine za kuwasaidia kupumua kunaweza kuwa changamoto kubwa

Mashine hizo zinasaidia mapafu kupumua na kutoa hewa chafu ya kaboni mwilini wakati mtu ni mgonjwa sana hali ya kwamba hawezi kujisadia kupumua.

Mojawapo ya vifo vilivyorekodiwa kutokana na virusi vya corona barani Afrika ni mwandishi wa Zimbabwe Zororo Makamba mwezi Machi.

Baraza la mji mji mkuu wa Harare limesema kwamba halina vipumuzi kumtibu na kuna hofu kwamba ugonjwa huo unaweza kusambaa haraka katika maeneo ya watu wengi ambapo mtu hawezi kufuata agizo la kutokaribiana na watu wengine ambapo wengi hawana uwezo wa kupata maji safi na sabuni.

Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 17 Aprili 2020

Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.

BBC
 
Nashauri Dar iweke lockdown. Watu wasitoke wala kuingia Dar na Zanzibar ili isienee sehemu nyingi.
Tusisubiri sana kuona watu wengi wanaugua.
Tusipuize jamani ndugu zanguni.

2020
 
Hivi ile mashine ya kupima joto ni bei sana? Kwa nini usiwekwe kila mpk Wa mkoa ili wanao ingia mkoa au kutoka mkoa moja kwenda mwingine wapimwe ili kuzui kuamisha virusi
 
Hivi ile mashine ya kupima joto ni bei sana? Kwa nini usiwekwe kila mpk Wa mkoa ili wanao ingia mkoa au kutoka mkoa moja kwenda mwingine wapimwe ili kuzui kuamisha virusi
Ile inapima joto, kwahiyo utaweza tu kumtambua mtu ambaye ameshaanza kuonesha dalili za kuumwa (homa)
Kwahiyo mtu anaweza kuwa na virus na bado hajaanza kupata homa, kipima joto kinaonesha kuwa ni mzima kumbe siyo.
Nahapo anaendelea kuambukiza wengine.

Wanasema inachukua siku 14 hadi 30 kuweza kuanza kuumwa tangu mtu aambukizwe.
 
Mkuu habari za hivi karibuni ni kuwa ndani ya Siku 2 hadi 5 dalili zishaanza kuonekana Na wanadai usiende hospital kama hujaambiwa kama ulipiga simu
Ile inapima joto, kwahiyo utaweza tu kumtambua mtu ambaye ameshaanza kuonesha dalili za kuumwa (homa)
Kwahiyo mtu anaweza kuwa na virus na bado hajaanza kupata homa, kipima joto kinaonesha kuwa ni mzima kumbe siyo.
Nahapo anaendelea kuambukiza wengine.

Wanasema inachukua siku 14 hadi 30 kuweza kuanza kuumwa tangu mtu aambukizwe.
 
Hivi kwanini WHO inawekeza nguvu kubwa corona kusambaa africa kuliko kitj kingine aah inaboa sana hali hii
 
Corona yetu Afrika ni njaa, ajali, utapiamlo, Malaria, HIV/AIDS, na magonjwa ya kitropikia

Kwa nini wazungu wanailazimisha Dunia nzima ilie kilio chao na wakati na sisi tuna vilio vyetu ambavyo huwa hawatusaidii

Covid-19 kwa Afrika inakuzwa na hofu ya vyombo vya habari

Vyombo vya habari huwa ni kansa ya kueneza mitazamo hasi

Tunaambiwa subirini wiki mbili zijazo mtaona lakini siku zinaenda mambo ni Yale yale
 
hata mimi nahisi hivyo.. corona sio hatari kwa africa kulinganisha na njaa, ukimwi, ajali za barabarani au vita za kuuana wenyewe kwa wenyewe

corona ina mwezi mzima tanzania vifo havifiki hata 10.. na kelele nyingi za media.. huku ajali za barabarani juzi tu kibiti zimeua watu 15.. na boda boda zinaua watu kila siku, ukimwi kila siku unaua watu.. bado vibaka wanaua watu kila siku kwenye uporaji
 
Hao hao ndio walisema wiki hii maambukizi Afrika yataishangaza dunia sasa mbona sio hivyo.
Wanataka watuchanye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu mnaotoa comment za namna hii huwa natamani sana korona ianze kufyeka familia yenu.

WHO sio watabiri wa nyota au mitume wa uongo mliozoea. Wao wanafanya projection kwa data na kutoa observation. Kwakuwa nia yao sio kuona walichopredict kinatokea, ndyo maana wanatoa na suggestions nini kifanyike.

Sijui waafrika tuliumbwa na Mungu gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata mimi nahisi hivyo.. corona sio hatari kwa africa kulinganisha na njaa, ukimwi, ajali za barabarani au vita za kuuana wenyewe kwa wenyewe

corona ina mwezi mzima tanzania vifo havifiki hata 10.. na kelele nyingi za media.. huku ajali za barabarani juzi tu kibiti zimeua watu 15.. na boda boda zinaua watu kila siku, ukimwi kila siku unaua watu.. bado vibaka wanaua watu kila siku kwenye uporaji
Endeleeni kupuuza tu. Ila cha moto mtakiona.

Huu upuuzaji mtashangaa wenzetu wanarecover mapema then wanaendelea na biashara zao. Sasa kwa uzembe wetu watatuppiga pin africa yana hakuna kitu wala mtu kutoka wala kuingia africa. Apo ndyo utaona uchumi utakavyoumia huku tukipambana na ugonjwa tuliopuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom