Vipindi vya Television.

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
Habari za weekend ndugu zangu natumai mko salama, ehee ni weekend tayari.
Twende kwenye mjadala
Tanzania iko katika biashara ya vingamuzi kwasababu tulitoka uko kwenye analog na sasa tuko digital lakini ni kama atutumii fursa hii vizuri.
Nafikiri mna weza kukubaliana na mimi kama umewahi kutumia DSTV utakutana na vitu vingi sana ambavyo hutachoka kutazama kwenye stesheni zake. vipindi vingi venye kuchekesha na kukutoa stress za dunia hii lakini ukija kwetu ni kama vingamuzi vinalega lega katika kubuni na kuchagua stesheni za kuweka kwenye vingamuzi vyao unaweza kulipia kifurushi cha juu kabisaa lakini wakati mwingine ukakosa kipindi kizuri cha kutazama pamoja na familia na wote mkafurahi bila mmoja kuona kama kipindi kinaboa.
Twende kwenye lengo la maneno yote hayo
Leo nimekutana na video flani kama muinavyo hapo , ni fun video mimi nikawaza huu si unaweza kuwa mchezo kabisaa ukaratibiwa vizuri na watu wanaohitaji kushiriki wakatuma maombi wakachaguliwa kadhaa randomly wakapimwa afya wakashiriki na atakaeumudu akala 100k or 150k.
kwa mliki wa kingamuzi kikawa kipindi kinaluka kila week labda , Chenye challanges kama hizi tofauti tofautii zinazoendana na tamaduni zetu bila kuathiri sheria za nchi na sio lazima tuige challanges za nchi zilizoendelea tunaweza kuwa na challanges tulizobuni wenyewe zinazoendana na budget na mazingira yetu.
Kikawa kipindi kinawapa burudani watazamaji wa rika zote lakini pia kinatoa fursa ya kuingiza pesa kwa ajili ya matangazo kwa sababu naamini kitaangaliwa tu kikiluka kwenye muda sahihi na kikiratibiwa na kupromotiwa vizuri ,tena kitaangaliwa kuliko vipindi vingi tu vya hapa bongo, lakini pia kikawa chanzo cha pesa kwa waliopata bahati ya kushiriki.
Vipindi vya aina hii vimekuwa chanzo cha pesa nyingi tu katika nchi za wenzetu sisi sjui tunashindwa wapi, Tuna vipindi vya ajabu ajabu sana ata avina mvuto sjui nyie mnaonaje...
 

Attachments

  • 255653889056_status_e3f409d8b2ed4087b1ff46c3942603f0.mp4
    3.2 MB

Similar Discussions

Back
Top Bottom