Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!

Nitonye, kwanza sitaweza kuchukua maoni yote au ya wote. Pili ni lazima nitachagua yale ambayo ni fit for public consuption ndio nitayatumia. Hata yawe mazito vipi nitayatoa ila lazima nichague kwa makini kwa sababu kwenye broadcast media, nikiweka madudu wenye TV na Redio zao hawatarusha.
 
Ni wazo zuri sana mkuu, nikweli kabisa humu ndani kuna mambo ambayo ukiyaona na jinsi yalivyo na tija utagundua upo umuhimu wa kuwafikia wananchi. Wana jamii wenzangu tukumbuke kuwa michango yetu imekuwa ni muhimu sana na inahitajika kuwafikia wanajamii wengine ambao hawajui kusoma na kuandika, hivyo mawazo yetu yatafika mbali sana iwapo yatawafikia watu wengi zaidi kama zitatumika njia mbadala maana pia itasaidia kuitangaza jf kwa watu wasioijua. Kuhusu usiri hilo sio tatizo maana kuna member wengi ambao kwasasa wanatumia ID halisi hivyo itakuwa ni matakwa ya mtu binafsi kama atatumia jina lake au JF ID. NAUNGA MKONO HOJA.
 
Wazo zuri lakini tunahofia michango mizuri itakuwa inaminywa
TIQO, ni kweli sio kila michango itatumika ni baadhi tuu, ila hiyo ambayo haitatumika haina maana imeminywa, itakuwa haukuchaliwa tuu. Kwa uzoefu wangu humu Jukwaani hoja nyingi kali na moto ni hoja za kisiasa zaidi, program yangu sio ya siasa ni ya issues za kiutendaji zaidi kwa maslahi ya taifa.
 

Huyu Huwa anaongea kama serikali, Kama waziri Mkuu, fatilia issue ya Madaktari na ile summary dismisal yake, Issue ya Mwakyembe na sumu, TANESCO na Dowans. Leo aje kuzuga na TV show, Nionyesheni wapi aliisha kuwa kinyume ama kumpinga Mbunge wa Monduli? I can not buy this idea. Huyu Mzee wa bahasha leo awe mwema na pen NAMES? Acheni JF iwe kama ilivyo sasa otherwise JF ije na TV yake. Nina mwamini sana Maxence Melo na wengine wa JF kuliko huyu bwana na Idea isiyo na kichwa wala miguu...Pascal ni mjuaji kila kitu yeye anadhani yuko top of the game. Hapa anatafuta cheap popularity, Great thinkers kuweni makini na hili chaka Pasco anakotaka waingiza.

I dont support this at all......

Zee la Pombe
 
Bro Pascal!

Wazo lako ni zuri tuu ila kwanza linahitaji muda kwa wadau wengine ambao ni JF members kuweza kujipanga na hasa kufanya risk assessments ili kuweza kuanisha faida na hasara zake, tusije tukakurupuka kuanzisha kitu ambacho kitawasaidia wabaya wa JF kulimaliza jukwaa letu hili au kuwaadhibu wana JF kwa namna yoyote ile.

Chonde chonde, ebu vuta subira kidogo kwani kuanza ku record na kukirusha hewani hicho kipindi by next week kabla wengi wetu hatujafaham faida na hasara zake kunaweza kututokea puani.
 

Nakubaliana na hoja yako ya kutaka maoni zaidi toka kwa wadau. Lakini wasiwasi wangu bado uko kwenye implications. Watu wakishahisi hawako huru kutoa michango yao JF itazama. Hili litakuwa jambo la kushikitisha sana kama litatokea. Na depending on the topic tunaweza kujikuta tunawindana.

Tukumbuke Tanzania ki-mfumo hatuko very open na hii ni kutokana na historia ya nchi zetu. Habari nyingi toka kwenye mawizara ni za kuiba na wakati mwingine zinazua zogo kwa wakubwa. Pia institutions zilizopo hazionekani kulinda usalama wa raia zaidi ya kufanya kazi za wakubwa. Sasa kama mwanaJF ndiye chanzo cha sensitive topic/mchango kwenye talk show itakuwaje wakianza kumska? Nani atakuwa responsible? Na ikitokea hivyo future ya JF itakuwaje?

Lakini kuna kitu bado sijaelewa Pascal labda ungefafanua. Unasema hivi "Ownership ya program itakuwa ni PPR kwa sababu ndio ata foot production costs" Kwa uelewa wangu PPR iko chini ya wizara ya utumishi - Mama Hawa Ghasia. Sasa Mama Ghasia anata kulipia mjadala ya JF? Tukubaliane Pascal hapa kuna kigugumizi maana JF imekuwa na hoja ambazo mara nyingi hutafsiriwa kama ni critical. Sasa serikali hiyo hiyo ilipie mijadala inawayowa-critisize?

Naamini unafahamu sheria (walau kwa kiasi fulani) sasa unaposema 'Ownership' nini tafsiri yake? Na mgao wa mapato yatokanayo na hizo talk show utahusisha JF? Maana contents ni za wana-JF, wizara ya utumishi wao watalipia gharama za kutengeneza/kuweka pamoja hiyo michango. JF kama JF wanapata nini? na kama hawapati ni kwanini? Ni vizuri tuweke bayana mambo mapema ili kuzuia sintofahamu mbele ya safari.
 
mkuu bonge la idea ila mkuu ilikuaje kuhusu kile kipindi chako cha Kitimoto nilikua nakipenda sana
Maishapopote, 'Kiti Moto' kilikula rungu la utawala wa Mkapa, jamaa hakupenda critique, ndio maana nimeamua kuiepuka siasa, rungu lile lile lisije likanishukia.

Kusema ukweli, baada ya Kiti Moto kufa, wakati huo nikiwa mtoto wa Ilala, niliishia zangu Italy kutafuta maisha, na huko sio tuu nilikwama bali pia nilipigika na nikapata maswahibu fulani nikaishia hospital, Mfanyakazi fulani wa Ubolozi wetu akiitwa Mchemwa, aliniokoa, habari zikaeneo hapo mjini Rome, Mtanzania mtangazaji wa Kiti Moto amelazwa hospitali fulani, ndipo Balozi Prof. Mahalu na Edward Lowassa wakaja hospital ndipo Lowassa akakiri yeye binafsi kusikitishwa na kufungwa kwa kipindi kile. Hii inamaana japo bosi wake alikerwa na kiti moto, baasdhi ya mawaziri wake walikikubali.

Kwa utawala wa sasa wa JK, umefungua zaidi milango ya uhuru wa habari, hivyo kikianzishwa kipindi kama Kiti Moto, this time kita survive. Acha nianze kuingiza mguu kidogo kidogo kwa talk shows ambazo sio za kisiasa, zikiota mizizi, nitapenyeza hoja muhimu kama mjadala wa katiba kidogo kidoga na kipindi kikisimama, kitu kama kiti moto kitarudi hewani!
 
Nimeandaa barua kwenda kwenye TV stations zote kuomba free airtime. Kwenye TV nitajitambulisha mimi kama mimi na sio jf ili nisije nikafungiwa milango kabla!. Nilisha zungumza na baadhi ya wamiliki walionyesha kuwa positive as long as sio politics.

great idea pascal...

lakini hapo kwenye nyekundu...mbona sasa ni kama unawapa "desa" wafanye hicho unachokihofu??
 
Kama unataka uhuru wa kutosha nashauri uombe airtime Citizen tv ya kenya uwe unatuma recorded programme na tukajadili yote mpaka siasa! Sikuhizi mpaka mawilayani watu wanatumia Cable tv hivyo utapata watu wengi zaidi then utakirudisha kwenye local stations kikishakuwa maarufu sana! Tuipeleke JF kama ilivyo kwenye Tv! Pale Citizen utakuwa huru kabisa! Maoni yangu mengine naya reserve kwa muda ila ni lengo zuri!
 
FJM, PPR, ni independent production house owned na Watanzania ambayo huwa inashinda tenda za kurusha matangazo ya baadhi ya matukio. Mojawapo ya tenda hizo, ni tenda ya kupublisize Wiki ya Utumishi wa Umma, hivyo wakaandaa vipindi 10 vya "Wiki ya Utumishi na PPR", lakini PPR sio ya Utumishi na haina uhusiano wowote na Hawa Ghasia.

PPR pia huwa inapata baadhi ya tenda za maonyesho ya saba saba hivyo hutoka na "Saba Saba na PPR", nane nane vivyo hivyo kwa "Nane Nane na PPR". pia kulikuwa na series za "Wiki ya Mawasiano na PPR" na series ya vipindi 20 vya "Miaka 50 ya Uhuru na PPR"

Hiki kipindi ni non profit na ni cha bure, PPR haitengezezi faida kupitia kipindi hiki bali ni kazi ya kujitolea, kama kazi ya kanisa kuwatumikia Watanzania. Ownership in this sense, ni umiliki wa kipindi na liabilities, nikimaanisha maoni ya kipindi yatakuwa ni maoni yangu na sio ya jf, hata kama nitapata mawazo na michango ya jf.

Matumizi ya maoni na michango hiyo ya jf kwenye program yangu, ni kama magazeti wanavyotumia contents za jf na hawasemi, kwa upande wangu nikitumia any content ya jf, kwanza ni lazima nimnotify mwenye content husika to seek his/her consent, ndipo nitumie. Tofauti pekee na wenye magazeti, mimi nitatoa attribution, kwa mwenye content na kwa jf.
 
Aminia, ucije ukachanganya siasa ukajiua mwenyewe

Sielewi kwa vipi hiyo talk show itakwepa siasa? Sukari ni siasa, daraja la kigamboni ni siasa, maji ni siasa,elimu ni siasa, na hata mgomo wa madaktari ni siasa. Unapongea kuhusu mgomo wa madaktari unagusa siasa moja kwa moja kwa sababu wenye wajibu wa kusimamia huduma za afya ni viongozi wa serikali inayotakana na chama cha siasa. Na kwa sasa serikali iliyo madarakani inatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivyo huduma za afya zinatolewa kufuatana na ilani ya CCM. Whether wametimiza kila walichoandika kwenye ilani au la hayo ni mambo mengine, lakini wasimamizi ni wanasiasa. Kwani Pinda na Ponda ni nani? ni manabii? au ni comedians?

Ni muhumu tukawa na intellectual debate about this talk show ili kama itakafanyika basi iwe kwenye viwango vinavyotakiwa na vya kuleta manufaa. Kama wamiliki wameshaanza kuweka masharti ya aina za topics then sioni umuhimu wa hii talk show. Kwanza unafadhiliwa na serikali, pili wamiliki wanaweka masharti!
 
Zee la pombe, naona umenichanganya mimi Pascal Mayalla na Pasco wa jf, sisi ni watu wawili tofauti in terms of contents, Pasco wa jf yeye ni mtuu wa kwenye jukwaa la jf tuu, he is not real, mimi ni Pascal Mayalla mwenyewe, the real one.

Mawazo yako ni muhimu ndio maana nimeomba mawazo yetu hili lifanyike au laa.

Kama uliusoma utangulizi wangu, hiyo kazi ya production kwangu ni part time, huwa nafanya programs kibao, kuhusu issue nyingi tuu tofauti, hivyo hata mawazo ya wengi yakishinda kuwa jf, tubaki hivi hivi tulivyo, nitaheshimu mawazo ya wengi, ukifungua hiyo attachment ya script ya kipindi, utaweza kuona kuwa kipindi kinaweza kufanyika with, or without jf input!.
 


Pascal nashukuru kwa ufafanuzi. Naomba niweke sawa mambo, nilitaja jina la Hawa Ghasia kama waziri mwenye dhamana wizara ya Utumishi. Pia naomba niwe wazi, I DO NOT BELIEVE IN THE CONCEPT OF NON-PROFIT. It is a farce, big time, hasa Bongo.

If PPR is some sort of a non-profit then that raises more questions.Yaani hawa watanzania watagharamia production costs for nothing? Like Mother Theresa? Ndugu usije kutumbukiza JF kwenye zogo la kumpigia mtu debe? Hapa tunaona wadau wakiwapigia wapambe wao upatu kupitia signature zao.
 
FJM, Tanzania ni secular state, haina dini, ila Watanzania wana dini zao, na dini ni imani, Watanzania hawa hawa wenye dini zao, hufanya maamuzi kibao kwa mujibu wa imani zao, bila kuchanganya dini na maamuzi yao japo ni imani ya dini zao, imewachochea kufanya maamuzi fulani kwa nchi ambayo haina dini.

Dini ni imani na sio siasa, na haturuhusiwi kuchanganya dini na siasa, lakini kila siku tunayasikia mahubiri kwenye nyumba zetu za Ibada. Wakristu wanaomwamini Kristu, wakitoa waraka wa kuhimiza waumini wake wamchague kiongozi "mcha Mungu", anaelewa fiki ni kiongozi wa imani gani atafit kwenye mcha Mungu kwa Wakristu!. Waislamu wakisema ni dhambi kwa Muslam kumchagua Kafir!, japo kafiri ni mtu asiye na dini, kwa imani ya Kiislamu Dini ya kweli ni moja tuu, hivyo wahubiri wa kiislamu wakisema usimchague kafir, utaelewa ni nani wanamlenga. Kila kitu ni siasa!.

Hata mimi katika hiyo program ziwezi kukwepa siasa 100 kwa mia, bali nitachagua topic za non political issues zaidi ya Siasa. Mwakiyembe akirudi, tunaweza kuuzungumzia ugonjwa wake kama ugonjwa desease bila kuzungumzia dhana za sumu ambazo ni pure politics.

Naweza kuzungumza na Lowassa kuhusu his role kwenye Richmond, na kwanini alijiuzulu kwa kauli "nawapeni mlichotaka" if he had no hand. Tunaweza kuzungumzia The constitutionalism of our constitutition bila kuzungumzia party politics or the role of CCM or Chadema kwenye the making of our new costitution.

Bado tunaweza kujadili issue muhimu kwa mustakabali wa taifa letu bila kujadili U CCM, UChadema au UCUF, hivyo tutakuwa tumejadili issue bila siasa zake.

Lazima nikiri the deviding line nini ni siasa na nini sio siasa is very thin, kinachofanya issue moja ionekane ni siasa au sio ni the motive behind!.

Mfano naweza kumjadili rais JK kuwa IQ yake ni low ndio maana alipata GPA ya 2.1 na hata kumuita ni kilaza kama bintiye Mwanaasha, nikimjadili kihivyo nitakuwa kama nimemtusi kwa kwa sababu viongozi wengi wazee wetu walikuwa na busara na hawakwenda hata shule wala hawakusoma hata darasa moja, hivyo IQ, GPA na DV IV doesent matter kinachomater ni ku deliver. Lakini kama nikichukua baalthi ya maamuzi ya rais, na chama cha Mapinduzi, nikaonyesha ni jinsi gani uamuzi huo ni mbovu with comparison, nikafikia conclusion JK ni rais mbovu, nitaionyesha ubovu huu bila kuonyesha nimemtusi rais.

Hivyo issue ikizama kisiasa, itajadiliwa bila partisan politices in good faith, with objectivity na impartiality ili program isije kugeuka ni piga debe la chama fulani.
 
Na mengi ya kudadisi ila kwa leo ningesema kwenye angle moja tu..kuna kitu kizuri kitatokea ambacho pengine tusikione wengi.Kwa muda mrefu baadhi ya member humu wamekuwa wakilalamikia wenzao juu ya michango yao iliyojaa matusi,kejeli n.k hasa kwa watu wanaotofautiana mawazo (ndo maana ajabu kwenye Jf yenye maneno home of great thinkers kuna jukwaa pekee la great thinkers).

Naamini watu wengi watajitahidi kufikiri na kutoa maoni au hoja zilizoshiba ingawa kwa viwango tofauti..ni ukweli pia kwamba kipindi kitafuatiliwa na wana -JF wengi tu wanaokipinga na wanaokipenda, kama ambavyo viongozi wasioipenda JF wanavyopita humu kuchukua mawazo na ushauri.Nani amabaye hatapata faraja kusikia hoja zake makini zikiungwa mkono na watanzania ambao hata hawajawahi kushika computer...Hii itachochea mijadala makini pia bila shaka

Nyongeza: dah naona itakuwa pia fursa yako ya kuwa moderator..nisikilizie watu watakavyokula ban...halafu kabla sijasahu kama kitarushwa kwenye TV sijui nitampaje mtu like.Tv yangu haina access ya hiyo kitu!!!
 

Samahani kwa kuchelewa kutoa maoni haya.LAkini nasema hivi chonde chonde tusiruhusu pascal akafanya mchezo huo, kwani ni mnazi mkubwa wa CCM.Nimekuwa nikimfuatilia mara nyingi kwenye vile vipindi vyake.Hana la maana zaidi ya kusifia Rais na CCM hata kama hutasema moja kwa moja.Siungi mkono hoja yake.Chunguzeni vizuri mtakuta kuwa katumwa ili kuua jukwaa hili lisilo na upendeleo wa hoja.JF itarudi kama gazeti au tv ambayo habari inahaririwa kwanza kabla ya kutoka.SIungi mkono wana JF
 


Pascal unaweza kuzungumzia mgomo wa madaktari au kupanda kwa bei ya sukari bila kugusa (hata kwa chembe moja) imani ya mtu. Lakini huwezi kuongelea mgogoro wa madaktari au kupanda kwa bei za bidhaa bila kugusa siasa. Ukielewa connection kati ya policy, political decision/manifesto na maisha ya kila siku utaona ninachosema. Bei, uchumi, huduma za afya etc hivi vitu vinagusa POLICY, policy ambazo zimewekwa na wanasiasa kwa uegemeo wa wanasiasa hao. Hakuna imani yoyote inayotokana na policy (wanasiasa). very simple!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…