EATV haipo kwenye StarTimes. Kwanini tv za Bongo zinakosa matangazo?

Kigger

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
805
710
Kwa pitapita zangu nimeona tv za bongo zimechoka, zimekosa ubunifu ikilinganisha na miaka iliyopita.

Nimejaribu kupitia tv za Kenya hata zile tv kaunti zina matangazo lukuki kila kipindi kikiwa na mdhamini zaidi ya mmoja, ambapo hapa kwetu kuna baadhi ya tv kubwa unaweza kutizama zaidi ya saa 3 ukokasa tangazo lolote mfano EATV NA STAR TV.

Inakuaje tv kongwe kama hizi zikose wadhamini wa vipindi? Nawaza jinsi watajiendesha vipi bila matangazo na hali hii sio kwa tv hadi radio.
 
TV karibuni zote zimefanana nyingi hazina vipindi vya maana mapenzi na udaku, wanaona gharama kuwalipa watangazaji waliosomea na kuokoteza okoteza watu
 
hao eatv hata radio yao haina matangazo kabisa sijui watu wanalipwa vipi? Hii ni sababu watu wanakimbi hii radio kila kukicha!
 
hao eatv hata radio yao haina matangazo kabisa sijui watu wanalipwa vipi? Hii ni sababu watu wanakimbi hii radio kila kukicha!
Nafikiri ea ubunifu hamna tv zote zilizo kataa wazo ya kibunifu zimekwisha
 
TV karibuni zote zimefanana nyingi hazina vipindi vya maana mapenzi na udaku, wanaona gharama kuwalipa watangazaji waliosomea na kuokoteza okoteza watu
Ni ajabu nilikua natizama tv ya kenya hadi kipindi cha reggae kina wadhamini 3
 
Halafu zimekaa kizee mnoo,muonekano wake hauna mvuto hata kidogo..hawana wataalamu wa graphics?
 
Back
Top Bottom