Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,550
- Thread starter
- #41
FJM, PPR sio non profit, ni production house hizo kazi zote inazofanya inalipwa. Na inafanya kazi kwa client yoyote kama alivyo dereva taxi hawezi kuchagua abiria wake.Pascal nashukuru kwa ufafanuzi. Naomba niweke sawa mambo, nilitaja jina la Hawa Ghasia kama waziri mwenye dhamana wizara ya Utumishi. Pia naomba niwe wazi, I DO NOT BELIEVE IN THE CONCEPT OF NON-PROFIT. It is a farce, big time, hasa Bongo.
If PPR is some sort of a non-profit then that raises more questions.Yaani hawa watanzania watagharamia production costs for nothing? Like Mother Theresa? Ndugu usije kutumbukiza JF kwenye zogo la kumpigia mtu debe? Hapa tunaona wadau wakiwapigia wapambe wao upatu kupitia signature zao.
Hebu hii hoja tuiweke hivi,
Pascal Mayalla ni dereva taxi inaitwa PPR, taxi inapaki kituo cha Mwenge, na kila siku taxi hiyo inakodiwa kwenda mjini kupitia Bagamoyo Rd kuwapeleka wateja mjini na kurudi ikiwa tupu. Kila siku inaporudi, humuona Mkuu Maxi, akitembea kwa miguu kurudi Mwenge, na nipomuuliza Maxi kwa nini anatembea kwa miguu, akaniambia ni kwa sababu daladala zinajaa sana, hivyo anapoteza muda mrefu kugoja dala dala na amegundua, akitembea, anafika mapema, na pia amajikuta anafanya mazoezi kuji keep fit na zoezi la kutembea.
Ndipo mimi nampa offer Max, kwa vile taxi yangu hurudi tupu muda ule ule Max anapotoka, nampa offer ya kumpa lift, free of charge, kumuwahisha Mwenge, hivyo kuokoa ule muda atakaoutumia kutembea, na kama ni mazoezi, basi atapata muda wa kuingia kabisa gym. Max ana uhuru wa kukuikubali hiyo lift, ama kuikataa kwa vile ameshazoea kufanya mazoezi, ama anaweza kuikataa hiyo offer kwa vile wapanda taxi wengine wanalipia, hivyo isije kuwa bure ni mwanzo tuu baadae akadaiwa. Au ameshazoea akitembea, anakuwa huru kupita pale kwa Mwajuma na Fatuma, sasa akipata lifti, kutamnyima uhuru wake, hivyo anaamua kuikataa hiyo offer hata kama ni bure.
PPR inaandaa vipindi vya wateja na inalipwa, nimeamua kuamndaa baadhi ya vipindi vya bure, sio lazima vya jf. Lakini kwa vile humu jf kuna michangu mizuri sana ya baadhi ya members ikiwafikia wengi zaidi italeta maana zaidi ya humu jf, ndio maana nimeomba mawazo yenu, jee tutoke nje ya jf, au tuendelee kujifungia humu humu jf. Kama hiyo lift ya PPR ita compromise uhuru wa jf, tutaiambia tuu hiyo PPR, asante kwa offer yako, endelea na fafari yako tuachie jf yetu kama ilivyo, then nitaendelea na program zangu without jf imput.
Naomba kusisitiza, nimeitoa hii offer in good faith, kama ni kupandisha vipindi, with, or without jf imput, program itapanda, nikiweka jf imput program itakuwa bora zaidi kwa diversed ideas toka ma great thinkers wa humu jf, nikiikosa jf input, program inaruka na watu wa mtaani, japo haitakuwa juu, ila mimi itakuwa nimetimiza wajibu wangu wa kuwatumikia Watanzania.