Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!

Samahani sana P Mayalla na wakuu wengine wa JF,

Siungi mkono hii hoja na huo ni uamuzi wangu unaotokana na baadhi ya mambo ambayo yananishawishi kufikia hitimisho hili,

1. P Mayalla aliwahi kuwa na kipindi cha kiti moto..Hicho kipindi kilitoweka ghalfa na hadi leo hajawahi kutueleza kilichomfanya asitishe kipindi chake...

Kama alifikia hatua hiyo bila kuwataarifu watazamaji wake, atashindwaje kufanya kitu kama hicho tena?

2. Taarifa za JF zinaonesha kuwa ndugu P Mayalla amekuwa mwanachama wa JF tokea 2/11/2009. Lakini ihadi leo ameweka mabandiko 74 tu ikiwemo yale aliyobandika leo....Kwa miaka yote hiyo alikuwa wapi? Kimemtokea nini hadi anakuja na wazo lake la kupeleka JF kwenye TV?

3. Kama kweli ni ubunifu na amejua leo baada ya kujificha kwa miaka 4 (akiwa member wa JF), kwa nini asianzishe mtandao wake tukampa maoni huko huko?

4. Amependekeza kuanza na suala la mogomo wa madakatari, anaweza kutupa uhakika msimamo wake kama mtu binafsi ulikuwa upi katika hili suala?

Haya ni baadhi tu ya mambo, hata hivyo nasisitza kuwa siungi mkono pendekezo la Pascal na ikibidi kutumia mawazo ya watu wa JF basi naweka objection ili asitumie mawazo yangu hata siku moja.

DC!
 
Utakuwa unatumia media ipi ktk kusoma?
Ni TV program sio kusoma, bali kuonyesha.Kusoma ni habari, matangazo na salama kwa redio, kwa tv ni kuonyesha.
Nimejipanga kutumia vituo 10 vya TV vilivyoka Dar es Salaam na redio zaidi 10 za jijini.. Nachofanya nimeandika barua kuomba free airtime kwenye TV zote za hapa jijini, TBC-1, TBC-2, ITV, EATV, Channel Ten, Star TV, Mlimani, TV Tumaini, Agape na TVZ. Nimeanza na hizi TV za Dar ndio kila kitu, nikimaliza nitapeleka TV za mikoani kama Aboud ya Morogoro, Sibuuka ya Shinyanga, Barmeda ya Tanga na ABC tv ya Arusha.
 
Wanabodi,
Salaam.
Hapa jf tuko wanachama wengi wenye shughuli mbalimbali. Kikubwa tunachokifanya ni kujadili tuu issues na kuishia kutoa maoni ambayo japo mengi huishia kutekelezwa mengi ya maoni mazuri ya humu huishia humu humu bila kufanyiwa chochote kwa vile mwisho wa uwezo wetu ni kujadili.

Mimi mwanachama mwenzenu wa jf, mbali ya shughuli zangu za kawaida kuniendeshea maisha yangu full time, mimi pia ni part time freelance producer wa vipindi vya Redio na Televisheni.

Asante.

Pascal Mayalla.

Mkuu Pascal mayalla

Sikubaliani na hoja yako hata kidogo maana wewe hapa JF sio mtu mzuri
tunajua undumila kuwili wako HEBU ANGALIA HAPO CHINI KWA MATUMIZI YA NENO "WANABODI"
HUU NDO UANDISHI WAKO

Wanabodi,
Hili ni opinion question yangu kuwa jee, serikali inajipanga kuwafukuza kazi madaktari wote waliogoma kwa 'summary dismissal" kwa kutumia kipengele cha "insubordination"?. Lengo likiwa ni kuzuia mgomo huu usisambae nchi nzima hivyo ku paralyse sekta nzima ya Tanzania?.

Opinion hii inafuatia majibu ya kimitego mitego yanayotolewa na viongozi wakuu wa seriali na sekta ya afya nchini!
1. Juzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, alisema yuko tayari kukutana na madaktari hao wakati wowote ila concern yake kubwa kwanza ni maisha ya watu yanayopotea!, hivyo akawataka kwanza warejee kazini ndipo mazungumzo yafuatie.
2. Jana Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda, alipanga kukutana nao, lakini badala ya kuwafuata pale wanapokutania, serikali ikatafuta ukumbi mwingine wenye usalama zaidi ili kumwezesha Waziri Mkuu Pinda, kwenda kuwaangukia!, Madaktari hao wagomaji wakataa kwenda pengine popote zaidi ya hapo walipo!.

Pasco (wa jf)
Update:
Nimeona news clip ya ITV. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda amewafuata madaktari walipo akiwa ameandamana na Waziri wa Utumishi, Hawa Ghasia na Naibu Waziri wa Afya Dr. Lucy Nkya.

Waziri wa Afya amepokea malalamiko yao ambayo wameyaelekeza kwa Waziri Mkuu. Pia amewasilisha ombi la serikali kuwa kesho warudi kazini wakati serikali ikishughulikia madai yao.

Hizi kauli za shinikizo la kuendelea kugoma, ni kweli umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini katika umoja huo tangulizeni maslahi ya taifa mbele, mkiendelea kutunisha misuli ni kweli mtakuwa fired, na ni kweli kuna baadhi yenu watagain kwa kwenda kupata kazi nje ya nchi, lakini kuna wengine wata loose na to be rendered jobless overnight!.

Kesho asubuhi ripotini kazini hata kama sio lazima mtibu, then endelezeni go slow mpaka kilio chenu kijibiwe!

Wanabodi,

Hili ni swali linaloibuka from opinion, jee kunauwezekano jf ni wachochezi?.

Swali hili linafuatia kinachoendelea sasa kwenye huu mgomo wa madaktari, does jf take side?.

Hapa nazungumzia matukia yanayoendelea baada ya serikali hapo jana kuwaamuru madaktari warejee kazini, huku madaktari wenyewe wakishikilia msimamo kuwa leo harejei mtu.

Pasco (wa jf)
Maslahi ya Taifa Mbele!.

HAPA NI GREAT THINKER HUDANGANYI MTU
 
Mungu akubariki Pasco....umeamua kupanda mlima mrefu sana. na lazima utambue kutumia hoja na majadiliano ya JF itakuwa kama ni msumari wa moto vile kwenye miguu ya baadhi ya watu.
 
Mkuu Pascal mayalla

Sikubaliani na hoja yako hata kidogo maana wewe hapa JF sio mtu mzuri
tunajua undumila kuwili wako HEBU ANGALIA HAPO CHINI KWA MATUMIZI YA NENO "WANABODI"
HUU NDO UANDISHI WAKO

HAPA NI GREAT THINKER HUDANGANYI MTU

Binafsi nimejaribu kujiaminisha kuwa Pasco ni tafauti na Pascal Mayalla...Hata hivyo naweza kusema kuwa Pasco anafahamika vizuri hapa JF kwa michango na misimamo yake kuliko Pascal.

Sasa kama Pascal hafahamiki vizuri katika anga za JF, tutamuamini vipi na kumpa nafasi ya kutumia mawazo yetu kwenye vipindi vyake?

DC!
 
DC your genius ! kacha wewe ni mjanja

Pasco hatukutaki na mambo yako

Kama Pasco hanitaki basi Pascal ananitaka na ndiyo maana kaleta hoja yake hapa JF!!!

Halafu jambo la kusikitisha ni kwamba Pascal hakuleta hapa wazo (idea) bali kaleta kitu ambacho keshakiweka kwenye utekelezaji (implementation)!!

I have smelt evil and I swear to ....Hii ni kitu hatari sana!!

DC!
 
Mkuu Paschal,

Wazo lako si baya ni katika kupata mawazo mbivu kutoka sehemu zote duniani.

Lakini usisahau kutumia mtandao unapokuwa unarekodi kipindi chako na pia ujijenge kwa kukaribisha mawazo kutoka mitandao mingine kama Facebook na Twitter.

Uzuri wa kuwa "online" unapoendesha kipindi hicho utapata mawazo si tu kutoka JF bali hadi kusoma na text messages na tweets.

Kwa mfano unapokuwa ukiwauliza maswali wahusika fulani unaweza kuongeze maswali mengine kutoka online.

Ukifanza hivyo basi utakuwa moja wa presenters wa kutisha.
 
FJM, Tanzania ni secular state, haina dini, ila Watanzania wana dini zao, na dini ni imani, Watanzania hawa hawa wenye dini zao, hufanya maamuzi kibao kwa mujibu wa imani zao, bila kuchanganya dini na maamuzi yao japo ni imani ya dini zao, imewachochea kufanya maamuzi fulani kwa nchi ambayo haina dini.

Dini ni imani na sio siasa, na haturuhusiwi kuchanganya dini na siasa, lakini kila siku tunayasikia mahubiri kwenye nyumba zetu za Ibada. Wakristu wanaomwamini Kristu, wakitoa waraka wa kuhimiza waumini wake wamchague kiongozi "mcha Mungu", anaelewa fiki ni kiongozi wa imani gani atafit kwenye mcha Mungu kwa Wakristu!. Waislamu wakisema ni dhambi kwa Muslam kumchagua Kafir!, japo kafiri ni mtu asiye na dini, kwa imani ya Kiislamu Dini ya kweli ni moja tuu, hivyo wahubiri wa kiislamu wakisema usimchague kafir, utaelewa ni nani wanamlenga. Kila kitu ni siasa!.

Hata mimi katika hiyo program ziwezi kukwepa siasa 100 kwa mia, bali nitachagua topic za non political issues zaidi ya Siasa. Mwakiyembe akirudi, tunaweza kuuzungumzia ugonjwa wake kama ugonjwa desease bila kuzungumzia dhana za sumu ambazo ni pure politics.

Naweza kuzungumza na Lowassa kuhusu his role kwenye Richmond, na kwanini alijiuzulu kwa kauli "nawapeni mlichotaka" if he had no hand. Tunaweza kuzungumzia The constitutionalism of our constitutition bila kuzungumzia party politics or the role of CCM or Chadema kwenye the making of our new costitution.

Bado tunaweza kujadili issue muhimu kwa mustakabali wa taifa letu bila kujadili U CCM, UChadema au UCUF, hivyo tutakuwa tumejadili issue bila siasa zake.

Lazima nikiri the deviding line nini ni siasa na nini sio siasa is very thin, kinachofanya issue moja ionekane ni siasa au sio ni the motive behind!.

Mfano naweza kumjadili rais JK kuwa IQ yake ni low ndio maana alipata GPA ya 2.1 na hata kumuita ni kilaza kama bintiye Mwanaasha, nikimjadili kihivyo nitakuwa kama nimemtusi kwa kwa sababu viongozi wengi wazee wetu walikuwa na busara na hawakwenda hata shule wala hawakusoma hata darasa moja, hivyo IQ, GPA na DV IV doesent matter kinachomater ni ku deliver. Lakini kama nikichukua baalthi ya maamuzi ya rais, na chama cha Mapinduzi, nikaonyesha ni jinsi gani uamuzi huo ni mbovu with comparison, nikafikia conclusion JK ni rais mbovu, nitaionyesha ubovu huu bila kuonyesha nimemtusi rais.

Hivyo issue ikizama kisiasa, itajadiliwa bila partisan politices in good faith, with objectivity na impartiality ili program isije kugeuka ni piga debe la chama fulani.

Pasco wa JF my boy,

I must admit now, kwa hiyo paragraph yako ya pili kutoka mwisho mimi umenifurahisha sana, and for that one naunga mkono hoja yako by 100%.

By the way, i got a GPA of 3.4 in B.com Finance, University of Dar es salaam (1999), thats why i do call myself what i've got to.
 
Mkuu Paschal,

Wazo lako si baya ni katika kupata mawazo mbivu kutoka sehemu zote duniani.

Lakini usisahau kutumia mtandao unapokuwa unarekodi kipindi chako na pia ujijenge kwa kukaribisha mawazo kutoka mitandao mingine kama Facebook na Twitter.

Uzuri wa kuwa "online" unapoendesha kipindi hicho utapata mawazo si tu kutoka JF bali hadi kusoma na text messages na tweets.

Kwa mfano unapokuwa ukiwauliza maswali wahusika fulani unaweza kuongeze maswali mengine kutoka online.

Ukifanza hivyo basi utakuwa moja wa presenters wa kutisha.

TV gani ya Tanzania inaweza kumruhusu mtu kusoma maoni ya watu live, tena kutoka kwenye mitandao ambayo ni ngumu kuwa-trace?

Umesahau kile kipindi cha JK ambacho tuliingizwa mkenge?

Bado sana, siamini kama hiki kitu kinaweza kufanyika Bongo na kisizue mitafaruku ya kisiasa!!

DC
 
Samahani sana P Mayalla na wakuu wengine wa JF,

Siungi mkono hii hoja na huo ni uamuzi wangu unaotokana na baadhi ya mambo ambayo yananishawishi kufikia hitimisho hili,

1. P Mayalla aliwahi kuwa na kipindi cha kiti moto..Hicho kipindi kilitoweka ghalfa na hadi leo hajawahi kutueleza kilichomfanya asitishe kipindi chake...

Kama alifikia hatua hiyo bila kuwataarifu watazamaji wake, atashindwaje kufanya kitu kama hicho tena?
Asante Dark City, kwa vile ni kweli, niliendesha kipindi cha 'KitiMoto' na ni kweli kilisitishwa na ni kweli sikuwahi kusema kilichonifanya hadi nisitishe kipindi kile, hivyo pia inaweza kuwa ni kweli nitaendesha kipindi hiki, na ni kweli kinawezxa kusitishwa na ni kweli kabisa sitasema kwanini kimesitishwa.

Kwa wasio jua, walifikiri labda mimi ndiye ninaye rusha kipindi hewani, mimi ndie ninayemiliki hizo stesheni, na mimi ndiye ninaamua nirushe kipindi au nisirushe!. Kwa taarifa tuu, kazi yangu mimi ni kuandaa tuu kipindi na kupeleka kwenye vituo vya TV ambao wao ndio huamua ama warushe, ama wasirushe. Kwa waliosoma attachment nimeeleza majukumu yangu ni kuandaa tuu na sio kurusha. Ili kipindi kirushwe, lazima niwaombe, na watarusha wale tuu watakao kubali. Kunauwezekano wote wasikubali hivyo kipindi hakitarushwa. Watakapo kataa kukirusha, wanaweza kukueleza sababu kwa kwanini wamekataa, ama wanaweza kukataa tuu bila kukueleza sababu. Kiti Moto kilipokufa tulieleza sababu loud and clear, wenye TV zao walikataa kukirusha na hawakutuambia sababu. Hata hiki kipindi kipya kinaweza kurushwa na baadae kikakataliwa kurushwa bila mimi kuambiwa sababu!.Hivyo sababu yako ya kukataa kuniunga mkono kwa sababu hii ni valid!, na kwa sababu kila kipindi kikisimamishwa huwa watazamaji lazima muambiwe!. Funga macho kumbuka vipindi vingapi viliwahi kuwepo na viliposimamishwa kama uliambiwa sababu!.

2. Taarifa za JF zinaonesha kuwa ndugu P Mayalla amekuwa mwanachama wa JF tokea 2/11/2009. Lakini ihadi leo ameweka mabandiko 74 tu ikiwemo yale aliyobandika leo....Kwa miaka yote hiyo alikuwa wapi? Kimemtokea nini hadi anakuja na wazo lake la kupeleka JF kwenye TV?
Kama kuna sheria ya jf kuwa ukishajiunga, lazima upost mabandika kadhaa kwa interval ya siku kadhaa, na baada ya kipindi fulani kupita lazima angalau uwe umefikisha mabadiko kadhaa, hapo naikubali kuwa hii ni sababu valid, kwa nini usiniunge mkono, na pia mwana jf akiadimika, anawajibika kueleza alikuwa wapi, mbona tangu nimejiunga nimekuwa nikiposti from time time, labda mnisaidie na mimi hizo rules ili nizifuate nisije kukosa uungwaji mkono wa Dark City maana michango yako ndio muhimu kweli, ukikataa wewe tuu, baas, kipindi hakiwezekani bila michango yako!.
3. Kama kweli ni ubunifu na amejua leo baada ya kujificha kwa miaka 4 (akiwa member wa JF), kwa nini asianzishe mtandao wake tukampa maoni huko huko?
, kumbe issue ni kuanzisha mtandao wangu?, kusema kweli hili ndilo haswa lengo langu, yaani kuanzisha mtandao wangu, halafu niitumie michango ya watakaochangia mtandao wangu ndio nitumie mawazo yao kwenye hiyo programu yangu, kama utaweza kunisaidia kwa hilo nitakushukuru, hata kunianzishia page tuu kwenye fesibuku, watu watachangia na mimi nitawataja, si unajua tena nilivyo mtupu, hivyo mimi nikiwa mwenyewe, siwezi kutangaza kitu ndio maana nikatafuta humu jf, hivyo kama utanisaidia kuanzisha mtandao wangu, utakuwa umenisaidia sana, please help!.

4. Amependekeza kuanza na suala la mogomo wa madakatari, anaweza kutupa uhakika msimamo wake kama mtu binafsi ulikuwa upi katika hili suala?
Kwenye program one hiyo ya mgomo wa madaktari, nimeweka pale script, hata ukiipitia utaona wazi, bila michango ya jf, sitaweza kufanya hivyo program, nisaidieni jamani, niko chini ya miguu yenu!. Tena naombeni niwape siri, nafanya hivi vipindi ili nipate pesa, si nitalipwa na naninihii.. nisaidieni mwenzenu nisife njaa!.

Haya ni baadhi tu ya mambo, hata hivyo nasisitza kuwa siungi mkono pendekezo la Pascal na ikibidi kutumia mawazo ya watu wa JF basi naweka objection ili asitumie mawazo yangu hata siku moja.
DC!
Kusema kweli Dark City, nakuomba ukubali, yaani hata wana jf wengine wote wakikubali na wewe ukataa, then siwezi kutengeneza program bila wewe maana maoni yako ndio yananiletea pesa nyingi!. Ila pia nitauheshimu msimamo wako!.
 
TV gani ya Tanzania inaweza kumruhusu mtu kusoma maoni ya watu live, tena kutoka kwenye mitandao ambayo ni ngumu kuwa-trace?

Umesahau kile kipindi cha JK ambacho tuliingizwa mkenge?

Bado sana, siamini kama hiki kitu kinaweza kufanyika Bongo na kisizue mitafaruku ya kisiasa!!

DC

Ni kweli kabisa.
 
Mkuu Pascal mayalla

Sikubaliani na hoja yako hata kidogo maana wewe hapa JF sio mtu mzuri
tunajua undumila kuwili wako HEBU ANGALIA HAPO CHINI KWA MATUMIZI YA NENO "WANABODI"
HUU NDO UANDISHI WAKO

HAPA NI GREAT THINKER HUDANGANYI MTU
Kachanchabuseta, naomba tujadili hoja, tusijadili watu!
 
Mkuu Paschal,

Wazo lako si baya ni katika kupata mawazo mbivu kutoka sehemu zote duniani.

Lakini usisahau kutumia mtandao unapokuwa unarekodi kipindi chako na pia ujijenge kwa kukaribisha mawazo kutoka mitandao mingine kama Facebook na Twitter.

Uzuri wa kuwa "online" unapoendesha kipindi hicho utapata mawazo si tu kutoka JF bali hadi kusoma na text messages na tweets.

Kwa mfano unapokuwa ukiwauliza maswali wahusika fulani unaweza kuongeze maswali mengine kutoka online.

Ukifanza hivyo basi utakuwa moja wa presenters wa kutisha.
Mkuu Richard, asante kwa wazo lako, hiyo program itakuwa recorded. Mimi ni outsider, kupata live program ni ngumu, isitoshe hiyo ni program ya bure, hivyo live ni next to imposible!.
 
Miongoni mwa mikakati ya kudhoofisha JF kabla ya 2015.

Safi sana Pasco naona unafuata hadidu rejea kwa kiwango kilekile.

Kazi nzuri, JF wakibana, then programme inarudshwa WITHOUT THEM, na mawazo yao yanatumika na bila credit yoyote, kama watu wa magazeti wanavyofanya.

Twende kazi..lolz..
 
Pasco ni identical twins wa Pascal Mayalla
Mwanamtama, huku sio kunitendea haki!. hata tuwe tunafanana vipi na Pasco, Mimi ni Pascal Mayalla na yeye ni Pasco wa jf, hata videle viwili vya mkono havifanani, sembuse twins!,

Mimi nimeshasema, na nitaendelea kusema, na kusema tena na tena,
Pascal Mayalla ndio mimi, na Pasco wa jf ni mwana jf pia!. JF tunanawalia na sheria, taratibu na kanuni tulizojiwekea, membe atatambulika kwa jina alilojitambulisha nalo, anatakiwa aheshimike hivyo, mfano wewe Mwanamtama, ukiamua kujitambulisha kama Mwanaulezi, Mwanamahindi, au Mwanakunde, hata kama mimi nakutambua wewe mwanakunde, ndie mwanamtama, siruhusiwi kusema Mwanakunde ndie mwanamtama etc, hii ni name calling!.Nawaombeni tujadili mada, tusijadili watu!.
 
Sawa mkuu,

Lakini sasa inakuwaje tena unasema wewe ni outsider wakati wewe ni mtayarishaji na mtamgazaji wa PPR?.
PPR ni independent production house, tunaandaa vipindi mbalimbali (recorded) vya radio na tv from outside na kuvipelekwa kurushwa na vituo mbalimbali vya radio na TV.
 
Back
Top Bottom