Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Feb 24, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Salaam.

  Hapa jf tuko wanachama wengi wenye shughuli mbalimbali. Kikubwa tunachokifanya ni kujadili tuu issues na kuishia kutoa maoni ambayo japo mengi huishia kutekelezwa mengi ya maoni mazuri ya humu huishia humu humu bila kufanyiwa chochote kwa vile mwisho wa uwezo wetu ni kujadili.

  Mimi mwanachama mwenzenu wa jf, mbali ya shughuli zangu za kawaida kuniendeshea maisha yangu full time, mimi pia ni part time freelance producer wa vipindi vya Redio na Televisheni.

  Nimejikuta ninaguswa sana na baadhi ya hoja zinazojadiliwa humu hivyo nimeona niutumie muda wangu wa ziada kuwatumikia Watanzania kwa kujitolea kuandaa vipindi vya Redio na TV vya Elimu kwa Umma kuhusu mada mbalimbali.

  Kufuatia maoni mengi ya maana yanayotolewa na wanabodi kuhusu hoja mbalimbali nimeamua kujitolea to walk an extra mile kwa kuyatumia baadhi ya maoni/hoja katika vipindi maalum, series za talk shows kuhusu haya tunayojadili humu.

  Kwa ruhusa ya invisible, na ruhusa yenu, nitaomba kutumia quote za baadhi ya members wa jf na nitatumia majina yenu haya haya ya jf, mara moja moja nitatoa number ya kupokea sauti kuhusu very specific issues na mara moja moja nitawaalika baadhi ya wana jf ambao hawatamaind expose ili kuchambua baadhi ya issues kwa maslahi ya taifa.

  Ownership ya program itakuwa ni PPR kwa sababu ndio atafoot production costs na mwendeshaji wa kipindi nitakuwa ni mimi. Kwa kuanzia nitaanza na kipindi kimoja kwa mwezi, kikigain momentum kina kuwa by weekly, then weekly.

  Main benefisharies wa program hizi ni Watanzania kwa ujumla ambao watakuwa more informed hivyo utakapo fikia muda wa kufanya maamuzi fulani, watafanya more informed decisions. Jf nayo itabenefit kwa ku feature more predominantly na baadhi ya mawazo ya hawa ma great thinkees wetu humu jf kama kina Mzee Mwanakijiji, Waberoya, Nguruvi 3 etc yatawafikia watu wengi zaidi.

  Kwa kuanzia nitawaomba wanabodi, kunikubalia kuiepuka siasa na kufuatia kukijua ni nini kilikikuta kile kipindi cha "Kiti Moto". Hivyo nitachagua mada kwa uangalifu sana, nitapenda kujikita kwenye mada za kijamii na za kimaendeleo na sio za kisiasa.

  Kwa kuanzia
  Prog1. Itahusu mgomo wa madaktari uliomalizika hivi karibuni.

  Nimeatach draft script naomba wenye nafasi muipitie na kunipa mawazo yenu.

  Nimepanga kuanza recording next week hivyo program itakwenda hewani in the next few weeks.

  Natanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.

  Asante.

  Pascal Mayalla.
   

  Attached Files:

 2. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mkuu ahsante kwa habari njema hiyo ila hicho kipindi kitakuwa kinarushwa kupitia tv zipi?
   
 3. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru mkuu, ila kumbuka tuko makini na wewe uwe makini mkuu. Wacha tupitie script kwanza.......
   
 4. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  mkuu bonge la idea ila mkuu ilikuaje kuhusu kile kipindi chako cha Kitimoto nilikua nakipenda sana
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Nimeandaa barua kwenda kwenye TV stations zote kuomba free airtime. Kwenye TV nitajitambulisha mimi kama mimi na sio jf ili nisije nikafungiwa milango kabla!. Nilisha zungumza na baadhi ya wamiliki walionyesha kuwa positive as long as sio politics.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Pascal sio wazo baya lakini implications zake may prove fatal kwa ustawi wa JF. Kinachoifanya JF iwe chachu ya mijadala mizito ni ule UHURU na anonymity anayopata mchangaiji. Watu wanaeleza mambo mazito humu kwa uhuru kabisa.

  Sasa, idea yako ya kutumia majina ya JF kwenye talk shows zako mimi inanipa mashaka. Utaua hii platform inayotoa fursa hadimu kwa watanzania kueleza kero za msingi kwa taifa hili kwa uhuru zaidi kuliko ambavyo wangefanya kama wangetumia mainstream media i.e TV.

  Pia ningependa niamini kuwa viongozi wengi, tena wazito wanapata points nyingi sana humu. Kama ulimsikiliza vema Waziri wakati wa zogo la madaktari pale Muhimbili alitamka wazi kuwa watu wamekuwa wanatoa tuhuma kwenye mitandao.

  Binafsi ningeshauri tufikirie zaidi namna ya kuifanya JF iwafikie watanzania wengi (pengine watumie simu) kwani uhuru (msisitizo) wa kutoa mawazo ndani ya JF ni wa kulinda!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Bukanga, kwa vile jf ina michango makini na michango ya ovyo, tutachagua ile makini tuu na ile ya ovyo tutaachana nayo. Kwa vile program hizi sio za kisiasa hivyo pia niko aware na maoni extreme yatakajifungamanisha na sera za vyama vya kisiasa.
   
 8. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  Inabidi uchunge ulimi maana wakati mwingine huwa yanakutoka yasiyotakiwa kutoka (wrong time and place)
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Utupe kituo cha TV kitakacho rusha haya mawazo yetu,mimi nashauri iwe ni TV ambayo coverage yake ni kubwa...isije ikawa ni Mlimani TV..otherwise for me it is a good idea and I appreciate.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  NI wazo zuri sana Pasco ila ni vyema pia kujua dhamira yako hasa ni ipi!! nauliza hili swali kwasababu kama ulikua biased wakati wa mgomo, then your views will never be balanced and you as a moderator, you may choose what to present

  I LIKE THE IDEA, I LIKE IT A LOT,, BUT I DONT LIKE THE FIRST TOPIC
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  FJM, hoja yako hii ni ya msingi sana, hata mimi nikiifikiria sana, kwa vile wengi wa members humu wanatumia pen names ili wasitambulike mathalan kwenye program yangu nikisema tusikilize maoni ya FJM, naweka maandishi ya quote yako ulichosema kuhusu mada fulani, then who will give a dam who FJM is?.

  Ila pia ninaconcern uhuru wa watu kujinwaga ukawa jeopardized na knowledge kuwa wanaweza kuwa quoted.

  Ndio maana nimeomba maoni yenu, kwa mfano mtu kama Mzee Mwanakijiji yeye tayari anatoa maoni yake kwenye magazeti mbalimbali hivyo sidhani kama atatatizwa na kuwa quoted as long as hautabadili kile alichokusudia.

  Naomba maoni zaidi kwenye hili.
   
 12. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  pascal mayalla

  sikubaliani na hoja yako kamwe kwa sababu inawezekana umeshachukua kibahasha.yaani umeshaandaa andiko la kipindi ndo unakuja kuomba?huu ni unafiki tu.mimi naamini huu mfumo unaoendelea jf ni mzuri,ingawa wewe Pascal huoni kwamba jf inaleta impact kwa jamii.leo hii hakuna mkoa au ofisi ambayo utamkosa mwanajf,isitoshe magazeti na vyombo vingine vya habari wanachukua news kutoka jf.huu urembo unaotaka kuuleta unaweza kutuondolea ladha ya jf.kwenye hiyo script yako unasema mgomo wa madaktari umeisha rasmi!!are u sure!acha porojo zako Pascal!!
   
 13. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ufafanuzi wako, ila kama unavyojua JF maoni yake ya member wake ni mazito, je utaweza kuyasoma yote bila woga wowote au ndio utakuwa unatoa yale mepesi? Na je kwenye hicho kipindi chako utakuwa unaalika watu wa aina gani? achilia wale wa JF.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  MTM, huyu sasa ni Pascal Mayalla, the real one. Pasco ni Pasco ana mawazo yake na bias zake na mimi Pascal Mayalla ni mtumishi wa watu, kipindi ni cha kuwatumikia watu, ukipitia script utaona nimejaribu ku strike the balance kati ya wadau mbalimbali.
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280

  Mimi binafsi nakuunga mkono kwa asilimia zote. Ni kweli kuna mawazo mazuri sana humu ambayo yanaishia humu kwani si watu wote wanaojua huu mtandao. Ni kweli viongozi hasa wabunge kuna baadhi ni wanachama na wengine wanapita njia tu humu kupata kinachochangiwa.

  Hivyo kwa uamuzi wako wa kutumia baadhi ya mada zenye mtazamo wa kijamii, mimi nakuunga mkono. na kama ulivyotoa tahadhari kuhusiana na siasa, hapo ni wewe wa kuchuja kipi kizuri kweli humu tunakosoa sana serikali ingawa wanaona kama sisi ni wapinga Serikali kumbe sisi tunatoa mawazo yetu. Hili ni kama Bunge kwani kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo na kukosoa, mbona hata Bungeni wanakosoana!!!!!!!!

  Isipokuwa sisi huwa tunaingia kwa undani zaidi kuliko hata Bungeni, na mara nyingi hoja zetu huwa zinakuwana evidency hivyo siyo za kugushi kinachosemwa hapa ni kweli kipo nakama viongozi wa Serikali wangelikuwa wafuatiliaji wa kinachosemwa hapa ina maana nchi yetu ingellikuwa na maendeleo sana. Hapa tunapeana habari mpya za matukio ambazo hata vyombo vya habari wnyewe bado kuzipata sisi tumeshapata.

  Mfano mimi hata kuangalia TV na magazeti huwa nimepoteza upenzi kwani hapa napata habari ambayo jioni nitasikia katika TV / Redio au kesho itaandikwa katika magazeti, sasa sioni umuhimu wa magazeti na TV/radio. Mimi kwangu JF ni chanzo cha habari tosha kabisa.

  Pia naunga mkono wazo lako kwani nakumbuka kulikuwa na mtandao ambao kipindi cha nyuma "bcstimes.com" lakini naona siku hizi hakunahuenda viongozi wetu wa siasa wameshaupiga pini. Huu mtandao kutokana na mawazo mazuri tuliyokuwa tunayatoa uongozi waliamua kuchukua baadhi ya maoni yetu nakuyachapisha kama yalivyo katika GAZETI LA MAJIRA. yaani tulikuwa na ukurasa mzima kwa ajili yetu kwa wiki.

  Inasaidia sana kufikisha ujumbe huu kwajamii ya Kitanzania na kuleta maendeleo.


  Nakupongeza sana P. Mayalla kwa uamuzi wako huo na ninaomba wanachama wote JF tumuunge mkono.

  naomba kutoa hoja:


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ningekupa like lakini kitufe kimepotea
   
 17. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wazo zuri mkuu
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Jackbauer, mimi ni Pascal Mayalla mwenyewe. Pasco ni Pasco na mimi Pascal Mayalla ni Pascal Mayalla. Kumfananisha member yoyote wa jf na member mwingine ni kosa la name calling!.
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri lakini tunahofia michango mizuri itakuwa inaminywa
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nashukuru kwa ufafanuzi
   
Loading...