Vipimo vya acre na hekta vikoje?

Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
11,796
Points
2,000
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
11,796 2,000
kwa wale wajasiriaardhi inatakiwa kujua hii mamboi ili kuepuka kuibiwa.
ekari moja ni sawa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba elfu nne (4000m[SUP]2[/SUP]) mfano.viwanja vingi vya mpira huwa na urefu wa mita tisini 90m na upana wa mita arobaini na tano 45m. ukichukua 45x90 unapata mita za mraba 4050m[SUP]2. [/SUP]kwa hiyo tunaweza sema ekari moja ni sawa na uwanja wa mpira wenye vipimo standard. kama shamba unalonunua haliko na pembe nne unaweza omba msaada kwa mtaalamu akusaidie kupima eneo. kumbuka hapa hatuongelei vipimo kuwa 45x90 bali eneo lazima liwe 4000m[SUP]2[/SUP] kwa hiyo kama shamba lako lina urefu na upana wa 50x80m basi ni eka sababu litakuwa na eneo la 4000m[SUP]2
[/SUP]hekta moja ni sawa na ekari mbili na nusu. ni eneo lenye ukubwa wa 10,000m[SUP]2 [/SUP]au sawa na eneo la 100mx100m au 250mx40m au 500mx20m
wenu katika ujasiriamali,
Red Giant.
 
T

Tuliwonda

Senior Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
121
Points
195
T

Tuliwonda

Senior Member
Joined Jun 29, 2012
121 195
Somo zuri mkuu! Ingawa naona kuna makosa kidogo hapo kwenye 50x40 ni 2000 na siyo 4000. Ina maana ni nusu ekali! Zaidi ya hapo pamoja sana mkuu, maana na mm nilikuwa najinunulia tu vijishamba kule buhongwa. Angalau nimejuwa kumbe havifikagi hata nusu ekali.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,527
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,527 2,000
kwa wale wajasiriaardhi inatakiwa kujua hii mamboi ili kuepuka kuibiwa.
ekari moja ni sawa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba elfu nne (4000m[SUP]2[/SUP]) mfano.viwanja vingi vya mpira huwa na urefu wa mita tisini 90m na upana wa mita arobaini na tano 45m. ukichukua 45x90 unapata mita za mraba 4050m[SUP]2. [/SUP]kwa hiyo tunaweza sema ekari moja ni sawa na uwanja wa mpira wenye vipimo standard. kama shamba unalonunua haliko na pembe nne unaweza omba msaada kwa mtaalamu akusaidie kupima eneo. kumbuka hapa hatuongelei vipimo kuwa 45x90 bali eneo lazima liwe 4000m[SUP]2[/SUP] kwa hiyo kama shamba lako lina urefu na upana wa 50x40m basi ni eka sababu litakuwa na eneo la 4000m[SUP]2
[/SUP]hekta moja ni sawa na ekari mbili na nusu. ni eneo lenye ukubwa wa 10,000m[SUP]2 [/SUP]au sawa na eneo la 100mx100m au 250mx40m au 500mx20m
wenu katika ujasiriamali,
Red Giant.
Samahani mkuu, na hii ya 70m x 70m ambayo ndio maarufu sana imetoka wapi? Mara nyingi sana hii ya 4900sq meters inatumika kama unit ya acre moja.
 
Kilimo

Kilimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Messages
779
Points
225
Kilimo

Kilimo

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2011
779 225
Samahani mkuu, na hii ya 70m x 70m ambayo ndio maarufu sana imetoka wapi? Mara nyingi sana hii ya 4900sq meters inatumika kama unit ya acre moja.

Ni kweli mkuu ekari1 ni 70mx70m kwahiyo eneo la ekari1 ni mita za eneo au square metres4900 hata kama hilo eneo ni mstatili,pembetatu,trapeza au msambamba au vinginevyo!
 
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
11,796
Points
2,000
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
11,796 2,000
wakuu mkiingia hata wikipedia imeeainishwa kwamba 1 international acre ni sawa na 4047m square na kwa kurahisisha huwa wanachukua 4000m square. hiyo 70x70 imetokana na watu kuhesabu hatua. wanaamini ukihesabu hatua 70 huku na sabini kule basi eneo lakatikati litakuwa sawa na ekari moja.
 
P

PUNJE

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2008
Messages
349
Points
225
P

PUNJE

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2008
349 225
..70 X 70 imetokana na vipimo vya YADI; katika vipimo hivyo eka ilihesabika ni yadi 70 kwa yadi 70; na hatua moja ya mtu mzima ililinganishwa na yadi moja. Yadi moja ni sawa na futi tatu kama ninakumbuka vizuri. hivyo eka moja nisawa na yadi 4,900 za mraba; 4,900 yd[SUP]2[/SUP]. kwa ufahamu zaidi YADI 1 NI SAWA NA MITA 0.9144; AU MITA 1 NI SAWA NA YADI 1.093613298337708. NIDHANIITAWASIDIA WENGI.
 
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
533
Points
250
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
533 250
..70 X 70 imetokana na vipimo vya YADI; katika vipimo hivyo eka ilihesabika ni yadi 70 kwa yadi 70; na hatua moja ya mtu mzima ililinganishwa na yadi moja. Yadi moja ni sawa na futi tatu kama ninakumbuka vizuri. hivyo eka moja nisawa na yadi 4,900 za mraba; 4,900 yd[SUP]2[/SUP]. kwa ufahamu zaidi YADI 1 NI SAWA NA MITA 0.9144; AU MITA 1 NI SAWA NA YADI 1.093613298337708. NIDHANIITAWASIDIA WENGI.
Punje, hapo umemaliza na hasa ulivyoeleza source ya huu mchanganyo wa 70 x 70!!

Amini amini nawaambia taarifa nyingi hapa Tz hasa kutoka kwa wataalam wasiokuwa makini ni zenye ubora wa chini sana na hazina usahihi kabisa! Taarifa hizo zinaweza kukupoteza ukadhani mambo ni mazuri au mabaya kumbe ni kinyume chake! Mkulima anaulizwa unashamba lenye ukubwa wa ekari ngapi, umevuna kiasi gani, kijiji kizima kinajumla ya eka ngapi! Mara nyingi takwimu zitolewazo toka kwa wakulima walio wengi juu ya maeneo yao ya uzalishaji huwa ni haya mashamba yaliyopimwa kwa kutembea tena kwa kuhesabu hatua 70 x 70 !

Hebu fikiria kama mpimaji wa shamba hatua yake ni sawa na cm 75 akipima hatua 70 atapata urefu wa sm 75 x 70 = sm 5,250 ukibadili kipimo cha sm kuwa mita sm 5,250 ni sawa na urefu wa mita 52.5. Kwa hiyo kupima hatua 70 x 70 ni sawa na kupima mita 52.5 x mita 52.5 = mita mraba 2756.25.

Hebu sasa linganisha eneo halali la ekari moja (mita mraba 4000) na eneo la ekari Feki 2756.25 tunazopimiwa kienyeji !!! Eneo la Ekari Feki ni asilimia 69 ya ekari halisi! Yaani katika kila ekari 100 unazopimiwa eka halisi ni 69 tu!!

Naomba nisisitize kuwa upana wa hatua ya sm 75 niliotumia ndiyo hali halisi maana wapimaji wengi hupima kwa kutembea kawaida, wachache sana hufikia hatua ya kukaribia mita moja (sm 100)!

Kwa hiyo ndugu zangu mavuno mengi tunayoambiwa hutokana na eneo feki hilo, unaweza kusema mkulima kapata kipato kidogo lakini ukikokotoa kwa ekari moja halisi unakuta amejitahidi sana! Pia eneo feki lina hasara moja mkulima anatumia madawa, mbolea na kiasi cha mbegu iliyoshauriwa kwa eneo la ekari moja yeye huweka kwenye eka moja feki, kwa hiyo au anazidisha dozi au anapata gharama kubwa isivyostahili.

Changamoto kwenu wajasiria mali wa kilimo, ACHANENI KABISA na upimaji wa maeneo ya mashamba kwa kutembea! Mtu mrefu na mfupi hatua zao tofauti, mtu aliyeshiba na mwenye njaa hatua zao tofauti, mtu anaeuza na anaenunua shamba hatua zao tofauti, mlimani na mabondeni hatua ni tofauti, shamba safi na chafu hatua zake tofauti! Kama unanunua shamba, au unakodi ukakuta mwenye mali hataki kupima kwa kipimo halisi basi wewe kubali yaishe ukishamiliki shamba pima mwenyewe ili ujihakikishie pasi na shaka eneo halisi la shamba lako! Poleni kuwachosha wandugu maana nami sinaga dogo mweee!! Mheshimiwa Malila nakusalimia sana popote ulipo, umenitia chachu kwa ushauri na ukarimu wako wa kumegeana maarifa nimeamua nifuate nyayo zako!
 
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2015
Messages
4,128
Points
2,000
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined May 28, 2015
4,128 2,000
acre ni saw na ekari? kwnye vipimo katika square metre inakuaje au ina ukubwa gani wakuu kwa units hzo?
 
HONDA XL

HONDA XL

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
139
Points
225
HONDA XL

HONDA XL

Senior Member
Joined Apr 4, 2012
139 225
Acre ndo ekari. Hapo ni swala la lugha, kingereza na kiswahili. Tofauti iko kwenye ekari na Hekta au kwa lugha nyingine acre & hectare
Ni kweli kuwa 70 kwa 70 imetokana na matumizi ya yard. Yard moja ni sawa na 0.91 Mira ambayo ni sawa na cm 91 au futi 3 pungufu kidogo ya mita moja. Na ukichukua yard 70 ni sawa na mita 64 ambazo kama ni mraba, kwa maana ya 64x64 inaleta 4096sqm around ekari moja.

Ni ukweli kuwa kutojua uhalisia wa vipimo kunaleta matokeo yasiyo.
Wakati Fulani nilienda kukodi eneo la shamba maeneo ya Ruaha Mbuyuni. Nikiwa na jamaa yangu, tukakodi ekari 6, aliyetukodisha alikuwa akipima kwa kamba ambayo alishaipima kuwa ni mita 70 kwa 70,
Baada ya kupima, akatukabidhi eneo letu la ekari 6, Mimi nikapita na GPS, kulizunguka nikakuta ni ekari 7.5.
Utaona ni jinsi gani mwenye eneo amejipunja lakini pia mkulima kama alishaandaa bajeti ya kuudumia eneo itamlazimu gharama kuongezeka bila kujua au akaishia njiani kwani anahudumia eneo kubwa zaidi ya alilokuwa amejipanga bila kujua.
 
LENGISHO

LENGISHO

Member
Joined
Sep 15, 2017
Messages
82
Points
125
LENGISHO

LENGISHO

Member
Joined Sep 15, 2017
82 125
KWA KITAALAM HAKUNA EKARI YA MIGUU,UKUBWA WA EKARI MOJA NI MITA ZA
ENEO 4000 SAWA NA UREFU MITA 100 NA UPANA MITA 40 AU MITA 64 UREFU NA UPANA
MITA 63,KIPIMO CHA MIGUU SIYO SAHIHI INGAWA WATU WENGI HUTUMIA KWA
MAZOEA KWA KUPIMA MIGUU 70 UREFU NA MIGUU 70 UPANA,LAKINI KUMBUKA
WATU TUNATOFAUTIANA UREFU WENGINE NI WAFUPI
 
jimmykb197

jimmykb197

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Messages
409
Points
500
Age
33
jimmykb197

jimmykb197

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2017
409 500
Punje, hapo umemaliza na hasa ulivyoeleza source ya huu mchanganyo wa 70 x 70!!

Amini amini nawaambia taarifa nyingi hapa Tz hasa kutoka kwa wataalam wasiokuwa makini ni zenye ubora wa chini sana na hazina usahihi kabisa! Taarifa hizo zinaweza kukupoteza ukadhani mambo ni mazuri au mabaya kumbe ni kinyume chake! Mkulima anaulizwa unashamba lenye ukubwa wa ekari ngapi, umevuna kiasi gani, kijiji kizima kinajumla ya eka ngapi! Mara nyingi takwimu zitolewazo toka kwa wakulima walio wengi juu ya maeneo yao ya uzalishaji huwa ni haya mashamba yaliyopimwa kwa kutembea tena kwa kuhesabu hatua 70 x 70 !

Hebu fikiria kama mpimaji wa shamba hatua yake ni sawa na cm 75 akipima hatua 70 atapata urefu wa sm 75 x 70 = sm 5,250 ukibadili kipimo cha sm kuwa mita sm 5,250 ni sawa na urefu wa mita 52.5. Kwa hiyo kupima hatua 70 x 70 ni sawa na kupima mita 52.5 x mita 52.5 = mita mraba 2756.25.

Hebu sasa linganisha eneo halali la ekari moja (mita mraba 4000) na eneo la ekari Feki 2756.25 tunazopimiwa kienyeji !!! Eneo la Ekari Feki ni asilimia 69 ya ekari halisi! Yaani katika kila ekari 100 unazopimiwa eka halisi ni 69 tu!!

Naomba nisisitize kuwa upana wa hatua ya sm 75 niliotumia ndiyo hali halisi maana wapimaji wengi hupima kwa kutembea kawaida, wachache sana hufikia hatua ya kukaribia mita moja (sm 100)!

Kwa hiyo ndugu zangu mavuno mengi tunayoambiwa hutokana na eneo feki hilo, unaweza kusema mkulima kapata kipato kidogo lakini ukikokotoa kwa ekari moja halisi unakuta amejitahidi sana! Pia eneo feki lina hasara moja mkulima anatumia madawa, mbolea na kiasi cha mbegu iliyoshauriwa kwa eneo la ekari moja yeye huweka kwenye eka moja feki, kwa hiyo au anazidisha dozi au anapata gharama kubwa isivyostahili.

Changamoto kwenu wajasiria mali wa kilimo, ACHANENI KABISA na upimaji wa maeneo ya mashamba kwa kutembea! Mtu mrefu na mfupi hatua zao tofauti, mtu aliyeshiba na mwenye njaa hatua zao tofauti, mtu anaeuza na anaenunua shamba hatua zao tofauti, mlimani na mabondeni hatua ni tofauti, shamba safi na chafu hatua zake tofauti! Kama unanunua shamba, au unakodi ukakuta mwenye mali hataki kupima kwa kipimo halisi basi wewe kubali yaishe ukishamiliki shamba pima mwenyewe ili ujihakikishie pasi na shaka eneo halisi la shamba lako! Poleni kuwachosha wandugu maana nami sinaga dogo mweee!! Mheshimiwa Malila nakusalimia sana popote ulipo, umenitia chachu kwa ushauri na ukarimu wako wa kumegeana maarifa nimeamua nifuate nyayo zako!
Samahani mada ni ya muda mrefu sana hii ila naomba kujua, nikitaka kupata kipimo halisi nitumie kifaa gani hasa kama nataka kupima eka kumi za pamoja. Asante
 
TsafuRD

TsafuRD

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2013
Messages
1,644
Points
2,000
TsafuRD

TsafuRD

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2013
1,644 2,000
Ni kweli kwa vipimo vya miguu huwa tunaibiwa sana. Mwaka 2009 mimi niligawiwa shamba na kijiji changu baada kutoa michango iliyoainishwa kwa kila ekari moja. Nilipewa ekari 50 kwa vipimo vyao vya kuhesabu miguu. baada kukabidhiwa nikamchukua mtaalamu wa kuipima kitaalamu ikapatikana ekari 28 tu. KWA MSINGI HUO KIPIMO CHA KUHESABU MIGUU HUWA SIYO SAHIHI HATA KIDOGO.
 
W

wakurochi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
699
Points
1,000
W

wakurochi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
699 1,000
Tumia kifaa kinaitwa GPS kinauzwa bei mbaya kidogo au mkodi mwenye nacho. Kidogo kama simu jaribu ku google (garmin gps ) ataweka alama sehemu ya kuanzia akizinguka shamba na kumalizia hapo hapo alipoanzia utapata ukubwa wa shamba kwa acre au hata mita za mraba .
 
W

wakurochi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
699
Points
1,000
W

wakurochi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
699 1,000
Nimecheki mahali humu humu Jf kwamba simu janja unaweza kuseti ukapima shamba. Ila anza na GPS ni uhakika ila hakimisha imesetiwa katika mita na sio futi
 
steph felix

steph felix

Member
Joined
Jul 26, 2015
Messages
10
Points
20
steph felix

steph felix

Member
Joined Jul 26, 2015
10 20
..70 X 70 imetokana na vipimo vya YADI; katika vipimo hivyo eka ilihesabika ni yadi 70 kwa yadi 70; na hatua moja ya mtu mzima ililinganishwa na yadi moja. Yadi moja ni sawa na futi tatu kama ninakumbuka vizuri. hivyo eka moja nisawa na yadi 4,900 za mraba; 4,900 yd[SUP]2[/SUP]. kwa ufahamu zaidi YADI 1 NI SAWA NA MITA 0.9144; AU MITA 1 NI SAWA NA YADI 1.093613298337708. NIDHANIITAWASIDIA WENGI.
Mkuu vipi, Kuna jamaa anataka kuniuzia kiwanja ila anasema robo eka ni 22mx17.5m.
Vipi hapo, vipimo viko Sawa?
 
Forum statistics

Threads 1,284,377
Members 494,064
Posts 30,823,405
Top