Vipimo vinaonesha sitoweza kuzaa, kama kuna msaada tafadhali

Vipimo vinaonesha sitoweza kuzaa, kama kuna msaada tafadhali

Awali ya yote nikupe pole ya dhati mkuu, pili nikushauri sana Mtegee Allah maana kwake hakijawahi haribika chochote, tatu nnaomba kama unaweza tembelea clinic moja iko Chanika inaitwa Tikaya, ujaribu na hapo pengine utasaidika kwa uwezo wa Allah,

la mwisho lkn kwa umuhimu nnakuomba tuliza akili kabisa, kaa na tulia usipaparike kabisa, nyakati hiz ukiwa na pupa utakua sehemu ya majaribio kwa matapeli na madawa ya kila aina, mwisho utaishia hata kumkosea Allah kwa kwenda kwa waganga,

Mimi nnakuombe kwa Allah akupe utulivu wa nafsi na subra ya hali ya juu, Mungu wetu usieshindwa na jambo nnakuomba umpiganie mja wako huyu na akapate hitaji la moyo Wake Aaamin
 
Pole sana mkuu.Ila kwa ushauri wangu naomba uzingatie "WATER THERAPY" kwa miezi walau mitatu.Ni very very very important.Tumia kwa wingi vyakula vya protini (mfano, karanga,maziwa,mayai nk).Pia epuka kula processed products.Zingatia balanced diet.Ndani ya hiyo miezi nahakika utakuja kutoa ushuhuda hapa.
NB1:EPUKA POMBE +SIGARA + STRESS
NB2:Heri usahau vyote hapo juu ila sio hiyo WATER THERAPY.NI MKOMBOZI WA WENGI,Kama huielewi i-google.[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Nimeisoma na nimeilewa ndugu,nitaifutilia, Asante Sana
 
Kuwa na imani utapona,usikubaliane na maelezo ya vipomo vya dr kwani kwa hakika utapona,Nina experience pana na hii kitu,kuwa na imani huku ukihangaika kwa wataalam zaidi,

Muhimbili wapo ma Dr wanatibu kwa tiba mbadala ie dawa zao ni vidonge lakini sio hivi vipatikanavyo MSD,vidonge vyao kwenye maduka ya madawa hakuna huwa wana import wenyewe,lakini chanzo cha dawa hizi ni miti na mingi ya miti hii inapatikana India.

Hawa wanakupima na huwa hawalazimishi ili kula pesa yako,wakikupima hueleza wazi kwamba tatizo lako linatibika ama haliwezekani wanakwambia,tiba yao ni gharama kidogo lakini kama watakwambia kwamba inawezekana,hakika kwa imani utapona.

Wapo waume kwa wake huwa wanapimwa mahospitalini na wanaambiwa kabisa kwamba hawezi kuzaa lakini leo wanamapacha.

Mimi nimekupa mwanga tu sasa kazi kwako nenda mwenyewe ufuatilie Muhimbili ili upate connection.
Mungu akutangulie.
 
Jaribu kutafuta second na third opinion.

Najua kuna utaalamu wa kuweza kuzi retrieve mbegu kutoka huko zinakotengenezwa moja kwa moja na kuzipandikiza kwa mama mtarajiwa, licha ya kwamba kipimo/ vipimo vya awali vimeonyesha hakuna mbegu.
Ndiyo hiyo pia imenisukuma kuja kwenu mdau,wapi inatolewa hii huduma? Maana Dr aliyenihudumia kasema mhimbili lakini hakuwa more openly
 
Pole sana mkuu. Yupo mtu huko Mwanza anaweza kukusaidia ngoja niwasiliane naye kwanza nimuulize kama atakubali nikupe simu yake uwasiliane naye! Zipo dawa za kienyeji kusukuma zinatibu tatizo hilo.
 
Tuambie ilikuaje had umekua hvyo. Je, ni life style gan unaish labda imepelekea ukapata tatzo hlo?
Na sie tujifunze..je
1.ulishawai umwa magonjwa ya zinaa kitambo
2.je uliwai umwa magonjwa ya kutumia dawa mda mref
3.wewe ni mwanachama wa chaputa
4.ushawai kua exposed na mionzi yoyote
 
Pole sana mkuu. Yupo mtu huko Mwanza anaweza kukusaidia ngoja niwasiliane naye kwanza nimuulize kama atakubali nikupe simu yake uwasiliane naye! Zipo dawa za kienyeji kusukuma zinatibu tatizo hilo.
Njoo PM nikuelekeze kuna miti fulani ipo huko Mwanza naijua kwa kisukuma sasa sijui utailewa!
 
Mkuu nakushauri ujaribu pia hizi Nuts za almonds, nasikia zinasaidia pia, ila tatizo lake ukila unakuwa na hamu na kufanya tendo, jaribu kutumia hata kwa mwezi mmoja sio mbaya (ila bila kufanya tendo ili sperms zijae), huko Kariakoo wanauza 15,000 nusu kilo, sijui huko mwanza...all the best
 
Mkuu Mungu yupo na anaweza mwombe kwa imani atakusaidia, epuka manabii na waombaji piga magoti usiku, asbh, mchana na kila unapokuwa na muda atakusikia na kukusaidia upesi na kukuza imani yako soma biblia kila mara itakusaidia sana kumsogelea Mungu

Kingine kuwa makini na matapeli watu watataka kutumia fursa ya frustration yako kukupiga pesa

Jingine hilo swala lako linatatuliwa kwa lishe kwa naamini lishe mbovu ya masukari mengi imechangia sana kwa mafunzo ya lishe bora mfatilie Dr Boaz Mkumbo MD anatumia jina hilo Fb, insta, YouTube n.k

Naamini utajifunza kitu na kama hutojali kk walau unishirikishe hata pm tushare zaidi... Pia msikilize Dr Sebi yeye alikuwa na ttzo la kutosimamisha kbsa na anashauri kwa mtu asie na sperm zenye ubora atumie juisi ya nanasi na vijiko 2 vya k swaumu... Mkuu fuatilia utajifunza kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom