GLOOMY
Member
- Jul 24, 2019
- 38
- 88
Nawasalimu ndugu zangu.
Miezi kadhaa nilileta mada hapa nikashauriwa na kufarijiwa nanyi, ushauri wenu kwa 75% niliufanyia kazi na wengi walishauri kurudia vipimo hospital nyingine hasa Kamanga Hospital na nilifanya kwa mwongozo wa Dr. bingwa.
Majibu yalikuwa yale yale 0 sperm count.
Dr. hadi leo anasema hajui hii hali imesababishwa na nini.
Ukweli sikutaka kurukia hatua nyingine bali nikajitafakali:
1.Mwaka 2008 nilikuwa na mahusiano na mdada, tulifanikiwa kupata mtoto, Ila sikumuoa kwa sababu nilikuwa bado nasoma na nilivyomaliza alikuwa tayari ameshaolewa.
2. Mtoto nilimchukuwa na naishi naye. Lakini kwa matatizo haya ya uzazi nikalazimika kupima DNA huyu mtoto, vipimo vinaonesha ni mtoto wangu.
3. Nina 0 sperms count na siwezi kuzalisha. Nikamrudia mzazi mwenzangu kwa swali la mtego tu (nimepima nimeonekana siwezi kuzalisha, hivyo basi hata mtoto huyu bila shaka sio wangu).
Jibu nililopewa ni kwamba mtoto ni wangu, ila hata yeye hajui kwa nini sizai, mama yake mzazi pia alikiri kuwa ni mtoto wangu Ila mwenzangu alichukia nilivyoenda chuoni na kutomuoa, hivyo nimtumie hela ya nauli aende mkoani akaongee naye kama kuna kitu alikifanya.
Kaka mtu pia alionesha mashaka na aliniahidi kuongea nao, mwisho wa siku alisema yeye kaongea nao lakini mengine nijiongeze mwenyewe.
Lakini ukweli inaonekana nimeumizwa na mzazi mwenzangu, kwa sababu alichukua picha zangu na kuna nguo zangu za ndani zilipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Lakini sikutilia shaka kwa sababu ya uchanga wangu kwenye mahusiano na malezi niliyokulia.
Kwenu wadau, jitihada zangu zimeishia kwa kutafuta chanzo lakini suluhisho ndilo liko juu ya uwezo wangu, na sikuwa na imani na masuala haya na sasa yamenipata.
Changamoto ni kujua wataalamu wa kweli maana hapa Mjini wengi wafanyabiashara.
Naomba tena ushauri na connection ya kulitatua hili suala.