To: Nyani Ngabu
Nimesoma comment zako zote kwenye hii thread ni kana kwamba ulikuwa na wivu fulani kwa jamaa waliokwenda vipaji maalum enzi hizo unasoma sekondari.
Hapana, umenisoma vibaya. Sijawahi, sina, na sitakuja kuwa na wivu kama huo. I have a ton of confidence in my abilities and never did I even once aspire to go to those so called special schools. Matter of fact, those who know me know how much I loathed going to boarding school. So jealousy and envy is not it for I don't think many of those students got anything on me anyway.
Kwanza kabisa nikumbushe tena kuwa shule za vipaji maalum zilifutwa. Sasa hivi yamebaki mazoea tu kuwa bado wanajitahidi kupeleka waliofaulu vizuri kwenye shule zilizokuwa za vipaji maalum, japokuwa vigezo sio strict sana kama zamani. Hata wa kawaida wanachomekwa. Ile spirit imeshakufa.
Beef yangu si uwepo wake au la. Beef yangu ni identification methods zilizokuwa zinatumiwa kuamua wewe una kipaji maalum na lesser mortal NN hana. Hivyo wewe unapangiwa Ilboru au Mzumbe na poor lil' 'ol me napangiwa Kibasila.
Kuhusu hoja yako inatakiwa utambue kwanza kitu gani kinathaminiwa katika elimu ya Tanzania. Kinachothaminiwa ni kufaulu mitihani. Hilo ndio jambo la kwanza.
Enhee...hapa kidogo sasa naona kama umeelewa hoja yangu. Hicho kinachothaminiwa hasa ndiyo kilicho misguided. Na methodology iliyokuwa inatumika kuthaminisha ilikuwa iko flawed. Hebu fikiria....mtu ni average student lakini anajitahidi sana kujisomea, kwenda darasani, yaani ana bidii kweli kweli. Kila akifanya term exams anafanya vizuri....national exam nayo anakuja kufanya vizuri. Anapata divisheni wani yake swaafi....matokeo yake anapangiwa shule ya "vipaji maalum" kwa sababu ana "kipaji maalum" kwa sababu tu kapata divisheni wani kali. Sasa kweli mtu huyo utasema ana kipaji maalum cha taaluma? Hapo si utakuwa unachanganya kipaji na bidii?
Kwa hiyo dhana ya vipaji maana yake ndio hiyo. Kwamba "academically gifted". Kufaulu mitihani ndio academics zenyewe.
Hapana. Sikubaliani na wewe. Kuwa na kipaji maalum ni, kwa mfano, mtoto wa darasa la tatu mwenye uwezo wa kushuka college level multivariable calculus na kwenda toe to toe na watu waliomzidi umri na ambaye wanafunzi wenzake wa umri/rika lake anawaacha mbali sana. Hicho ni kipaji maalum.
Au mtoto wa miaka miwili kuweza kusoma na kuelewa vizuri kabisa na ambaye hata akianza darasa la kwanza shuleni itabidi watumie silabasi tofauti kumfundishia kwa sababu ile ya kawaida atakuwa yuko too advanced kuizidi.
Sasa, hizo "special schools" zilikuwa zinatumia silabasi tofauti na ambazo wanafunzi wa Jitegemee au Buluba sekondari walikuwa wanatumia? Hao wanafunzi wa vipaji maalum walikuwa wanasoma mambo ambayo wanafunzi wengine walikuwa hawayasomi? Yaani kwa mfano walikuwa wanasoma mambo ya chuo kikuu wakiwa O-level? Na mitihani yao ya taifa ilikuwa iko tofauti na ambayo walikuwa wanafanya wengine?
Kwenye nchi za Ulaya na Marekani huwa wana methods mbalimbali wanazotumia kumtambua mtoto mwenye kipaji maalum na mojawapo ni IQ test. Je, hao wa kwetu walikuwa wanapimwa IQ zao?
Hayo mambo ya kushinda Nobel, kugundua dhana au vitu vipya kimsingi hayako kwenye mtaala wa sekondari. Angalia waliotunukiwa Nobel wote wametunukiwa kwenye ngazi gani. Utakuta ni watafiti waliokuwa kwenye vyuo vikuu.
Hahahaaaa hapa ndo ntakukamata wewe. Wengi sana wa hao Nobel laureates ukifuatilia historia zao utagundua kwamba ni watu ambao unaweza kusema walikuwa na vipaji maalum kweli kweli na siyo kama hivyo vya NECTA. Wengi wao utakuta walionyesha uwezo mkubwa sana tokea awali kabisa wakiwa wadogo. Na wakifika kwenye mavyuo makuu huko ndo wanafanya mambo yanayoonyesha kweli walikuwa na vipaji maalum. Sio hawa wa kwetu ambao "vipaji" vyao "maalum" vinaanzia na kuishia kwenye mitihani ya taifa.
Kwa lugha nyingine wewe unaangalia matokeo ya baadae sana nje ya muktadha wa vipaji maalum. Imani ni kwamba mtaala unamjenga mwanafunzi aje kufanya vema baadae kimaisha. Lakini kila mtu anajua kuwa kufaulu masomo darasani sio kwamba ndio utakuwa na tajiri kwenye biashara, au bosi kazini au mshindi wa Nobel hapo baadae.
Kufaulu tu masomo ya darasani hakumfanyi mtu awe na kipaji maalum. Hicho ndo ninachokataa mimi kwa sababu kufaulu tu mitihani si lazima uwe na kipaji maalum kwani hata mimi nimeshafaulu mitihani mingi tu na kwenye undergraduate hakuna term ambayo sikuwa kwenye dean's list lakini kusema ukweli sina kipaji maalum. Ni bidii tu ndo iliniwezesha kupata hayo mafanikio. Na kuna watu ambao wamesoma hizo shule za vipaji maalum, wengine wapo humu humu JF, wengine tunao mtaani, lakini mimi sijaona kabisa umaalum wa vipaji vyao. Ni watu wenye intellect ya kawaida kabisa. Lakini eti walisoma shule za watu wenye vipaji maalum....lol. Funny stuff.
Kwa hiyo kwa kipindi kile ambacho walikuwa sekondari kipimo pekee kilikuwa ni mtihani. Wamefaulu mtihani, wamestahili kuitwa "academically gifted". Kama una mtazamo tofauti basi angalia mtaala na mitihani, kuwa labda mtaala n mitihani haifai kutambua vipaji maalum.
Kufaulu mtihani siyo kuwa na kipaji maalum.
Hapo naamini tumeelewana.
Kama kwako kufaulu mtihani ndiyo kuwa na kipaji maalum basi usijipe moyo maana sikubaliani na hiyo hoja.