Vipaji maalum si lolote, si chochote

Vipaji maalum si lolote, si chochote

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Tanzania ina Shule sita zinazojulikana kama Vipaji Maalum. Zipo nne za wavulana na mbili za wasichana. Shule hizo ni Mzumbe,Tabora Boys,Ilboru,na Kibaha(kwa wavulana). Kwa wasichana ni Kilakala na Msalato.

Katika matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 yaliyotangazwa leo,Shule hizo za vipaji maalum zimeboronga. Hakuna hata moja iliyo kwenye kumi bora. Zimeshindwa kujidhihirishia utofauti wao. Vipaji maalum sasa hakuna lolote,hakuna chochote.

Nafasi zao ni kama ifuatavyo: Mzumbe(17),Kibaha(18),Ilboru(31),Tabora Boys(44),Msalato(59) na Kilakala(63).

NOTE: Shule mpya ya Marian Boys ambayo ndio kwanza imeanza kutoa wahitimu wa kidato cha nne imeshika nafasi ya pili kitaifa. Hii ni Shule pacha ya Marian Girls (zote ziko Bagamoyo).Marian Girls imekamata nafasi ya nne nyuma ya Feza Boys(3) na vinara St. Francis Girls ya Mbeya.

Kwaheri vipaji maalum!
 
enzi hizo ndio zilikuwa kipaji maalum sasa hivi hakuna la ziada hapo
 
Mpaka leo sijapata jibu la swali langu!

Vipaji maalum maana yake nini na ni vigezo gani ambavyo waliamua kutumia kuamua huyu ana kipaji maalum na huyu hana?

Kwa sababu kupata alama za juu tu kwenye masomo haimaanishi kwamba una kipaji maalum.

Hao wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule kuna hata mmoja aliyevumbua chochote cha kuboresha maisha ya mwanadamu?

Halafu, hao wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule za vipaji maalum mbona tunawakimbiza sana huku uraiani.

Vipaji maalum maana yake nini?
 
Hao wa enzi hizo kuna hata mmoja aliyeshinda tuzo ya Nobeli katika nyanja yoyote ile?

Kuna hata mmoja aliyevumbua hata kikanuni cha uongo na kweli katika fani yoyote ile?

Vipaji Maalum kwa hali hii ya UCHAKACHUAJI? Kila kitu ndani ya utawala wa sasa ni kuchakachua ili kufurahisha nafi ya bosi wako.....JK upo, unategemea nini?

Mfano mdogo tu ni lile sakata la Mitaala. Kila kitu tanzania hii hakuna kinacho aminika kwa sasa....dampo.
 
Bottom line ni kwamba hayo mambo ya vipaji maalum ni hogwash!

Hizo shule si za vipaji maalum. At least mimi sijaona umaalum wala kipaji chochote kwa wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule.

Kama wapo kweli na wanacho cha kuonyesha kuthibitisha umaalum wa vipaji vyao basi naomba mwenye hayo majina na accomplishments zao anipatie hapa.
 
Mkuu kuna vipaji maalum serikali na vipaji maalum binafsi. Na kutokana na ufundishaji mzuri wa vipaji maalum binafsi wanafunzi wengi "cream" wanaishia huko kwa akina St. Francis, Marian, etc. Wale ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia hizo karo kubwa ndo wanaenda huko Mzumbe, Ilboru na kwingineko. Kwahiyo na matokeo lazima yawe mazuri zaidi kwa vipaji maalum binafsi kwasababu pia huwa wanawachuja kila muhula.
 
Swali lako zuri sana Nyaningabu hata nami ningependa kujua criteria ya kuziita special schools. Maana definition ya special school ni tofauti na kilichopo katika hizo shule in terms of special teachers, buildings, learning activities etc.
 
Last edited by a moderator:
watu ambao hawajasoma spesho utawajua tu!! wivu umewajaaa! Subirini matokeo ya 4m 6 mwezi wa 5 ndo mseme

Kwa nini unakimbilia kunyoosha kidole cha wivu badala ya kujibu swali lililoulizwa?

Vipaji maalum maana yake nini na ni vigezo gani wanatumia kuamua huyu mwanafunzi ana kipaji maalum na huyu hana?
 
Ngalu, hapa nafikiri wanamaanisha vijana wenye akili kuliko wengine na si vipaji vya uvumbuzi wa vitu fulani.

Kwa hiyo ina maana nikiwa nina bidii sana ya kujisomea na bidii hiyo kupelekea kufanya vizuri katika mitihani ya taifa basi nitakuwa na kipaji maalum?

Na kwani kipaji cha uvumbuzi siyo ishara ya akili kuliko wengine?
 
kila kitu now days ni politics tupu, alikuwepo mkuu wa shule Iriboru ametandika pesa na wanasiasa wanafunzi na wafanyakazi wakasala anyway kwenye mgongo wa wanafunzi wakamkataa, leo nasikia yupo Pugu on the same position, siasa mbaya ya CCM imeharibu kila eneo, so hata ukipewa jibu sahihi why special school nadhani for this time halina maana tena, tuangalie njia mbadala ya kulinusuru hili taifa na janga la ujinga, maana kwa matokeo haya ya leo wandugu balaa linazidi. Watu wanakamuliwa na serikali through shule za kata then hakuna wanachopata, hizi hasara wanazopata wazazi watazirudishaje.

Lawama zote kwa serikali, maana ndio imeshindwa kutimiza wajibu wake, hakuna walimu wa kutosha, maabara hakuna, vitabu hakuna, mishahara midogo walimu kila siku wanalia, tutarajie nini zaidi ya hiki.
Watoto wanakwenda kukua kimo/umri kwa miaka mianne, academically hakuna kitu na tukumbuke hawa hata form 2 walishafeli wakaruhusiwa kuendelea mbele, unachanganya taaluma na siasa, tena siasa za hovyo za kutafuta sifa za kijinga.
 
Kwa hiyo ina maana nikiwa nina bidii sana ya kujisomea na bidii hiyo kupelekea kufanya vizuri katika mitihani ya taifa basi nitakuwa na kipaji maalum?

Na kwani kipaji cha uvumbuzi siyo ishara ya akili kuliko wengine?

Hili swali inabidi tumpelekee Kawambwa na timu yake watupe majibu
 
Hili swali inabidi tumpelekee Kawambwa na timu yake watupe majibu

Ndiyo maana nasema bado kabisa sijaona hivyo vipaji maalum vya hao wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule za vipaji maalum.

Kufanya tu vizuri kwenye mtihani haimaanishi una kipaji maalum. Serikali yetu ilibugi kabisa hapo.
 
Mpaka leo sijapata jibu la swali langu!

Vipaji maalum maana yake nini na ni vigezo gani ambavyo waliamua kutumia kuamua huyu ana kipaji maalum na huyu hana?

Kwa sababu kupata alama za juu tu kwenye masomo haimaanishi kwamba una kipaji maalum.

Hao wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule kuna hata mmoja aliyevumbua chochote cha kuboresha maisha ya mwanadamu?

Halafu, hao wanafunzi waliosoma kwenye hizo shule za vipaji maalum mbona tunawakimbiza sana huku uraiani.

Vipaji maalum maana yake nini?

Wakuu hizi Shule zinajulikana kama Special Schools; Ni special sababu wanaokwenda kule kwa Form One (ni wale waliofanya vizuri kuliko wenzao darasa la saba) na Form V (ni kwa wale waliofanya vizuri kuliko wenzao Form IV)..

Hicho ndio kipimo mitihani ya darasa la saba au form IV; Sasa maswali ya kama wameshinda Nobel Prize na mimi nikuulize ni watanzania wangapi wameshinda Nobel Prize ?, na kuhusu uvumbuzi wa mambo hicho sio kipimo hapa kipimo ni mitahani ambayo in short hawa jamaa walifanya vizuri kuliko wenzao. Ukitaka vipaji hata kina Diamond au wachoraji na wachonga vinyago hawa wanavipaji ingawa hizo tasnia hazifundishwi kwenye hizo shule.

Sasa kuboronga kwao after four or two years haimaanisha kwamba two or four years ago they performed brilliant. Kumbuka maisha sio sprint ni marathon (Its not a Battle its a War) na kushindwa kwao maisha haimaanishi kwamba walikuwa vipanga darasa la saba au form four. Every game has its rule Hizo shule haimaanishi kuna watu wenye akili kuliko wengine Tanzania nzima, bali inamaanisha kuna watu walio-perform brilliant than their counterparts. Lakini lack of teachers au kubweteka on their part inaweza kusababisha wakashindwa maisha mbeleni
 
Wakuu hizi Shule zinajulikana kama Special Schools; Ni special sababu wanaokwenda kule kwa Form One (ni wale waliofanya vizuri kuliko wenzao darasa la saba) na Form V (ni kwa wale waliofanya vizuri kuliko wenzao Form IV)..

If that is the case then whole idea is misguided! Performing with flying colors in a final national exam doesn't make one a gifted student.

Hicho ndio kipimo mitihani ya darasa la saba au form IV;

That is a misguided barometer.

Sasa maswali ya kama wameshinda Nobel Prize na mimi nikuulize ni watanzania wangapi wameshinda Nobel Prize ?

Ahaa! See now...? Further proof that the whole notion of having special schools for gifted students and the criterion used is misguided. It is misguided because passing an exam with flying colors doesn't mean that you are that gifted. If you are studious and work hard in your studies more likely you will get good results - which is totally different from being gifted - having a great natural ability.

na kuhusu uvumbuzi wa mambo hicho sio kipimo hapa kipimo ni mitahani ambayo in short hawa jamaa walifanya vizuri kuliko wenzao. Ukitaka vipaji hata kina Diamond au wachoraji na wachonga vinyago hawa wanavipaji ingawa hizo tasnia hazifundishwi kwenye hizo shule.

Again, the barometer used to determine whether a student is gifted or not is misguided. There are many naturally gifted people who never were good students in school but did a whole lot to contribute to humanity.

Sasa kuboronga kwao after four or two years haimaanisha kwamba two or four years ago they performed brilliant.

Perfoming well in an exam does not mean you are gifted.

Kumbuka maisha sio sprint ni marathon (Its not a Battle its a War) na kushindwa kwao maisha haimaanishi kwamba walikuwa vipanga darasa la saba au form four. Every game has its rule Hizo shule haimaanishi kuna watu wenye akili kuliko wengine Tanzania nzima, bali inamaanisha kuna watu walio-perform brilliant than their counterparts. Lakini lack of teachers au kubweteka on their part inaweza kusababisha wakashindwa maisha mbeleni

I'm not least bit convinced. There is nothing special in many of the students who went to those schools. If there is, then I haven't seen it. And if I haven't seen it that means they've got nothing to show for it.

So come again, brotherman! Nice try, though.
 
Back
Top Bottom