Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,777
- 41,066
Hivi hawa viongozi wetu wataanza lini kutekeleza majukumu yao badala ya kila siku kutoa maonyo ya kila aina kana kwamba watu wanawasikiliza. Mara "Rais kaonya hiki ama kile", mara "Waziri Mkuu ametoa maonyo kwa watu hawa na wale"... Mara "Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kali kwa wabadhirifu na wezi wa mali ya umma waache mara moja"... Hivi haya maonyo yamepunguza ubadhirifu kwa kiasi gani? Hivi ni watu wangapi wameweza kubadili tabia zao baada ya kusikiliza maonyo ya viongozi!!! Tumechoka na maonyo ya kitoto! Ni maonyo ya kumkataza mtoto kulamba sukari, na baadaye mtoto analamba utadhani hana akili
nalizungumza hili kwa hasira leo!!!
nalizungumza hili kwa hasira leo!!!