saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
Wana Bodi Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Njombe ametuomba watanzania kumpatia orodha ya wateule wake ambao wanajikweza na hawatekelezi kikamilifu majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao ili aweze kuwachukua hatua.
Namba tutumie fursa hii tutaja majina ya viongozi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na kusababisha manung'uniko mengi kwa wananchi na hata kusababisha kuvuruga maisha ya wananchi ya kila siku na kuharibu kabisa uchumi wa nchi yetu tukufu.
January Yusuph Makamba, Waziri wa Nishati ambaye ameonyesha wazi wazi kujikweza kulikopitiliza hadi kufikia hatua ya kuwatukana wabunge wa Bunge letu Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaita ni wapuuzi.
Kisa cha kufanya hivyo ni kwa sababu tu wamehoji kupitia Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Biashara na Mazingira kwanini Umeme unakatikatika zaidi ya mara 10 kwenye viwanda na kusababisha viwanda vingi kuzalisha chini ya kiwango na kusababisha uhaba wa bidhaa muhimu kwa wananchi na kusababisha bidhaa nyingi kupanda bei mara dufu na kutuumiza wananchi.
Pili Kamati ya Nishati ya Bunge chini ya Mwenyekiti wake Dustan Kitandula ilihoji sababu za kuchelewa kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo kwa mujibu wa Mkataba lilikuwa likamilike Juni 2022 lakini hadi jana Waziri anasema ujenzi umefikia Asilimia 67 tu bila kutoa maelezo ya sababu zilizosababisha mradi huo kuchelewa huku kukiwa hakuna tatizo la fedha.
Mbaya zaidi Makamba anasimama kwenye Mkutano wa hadhara huko Kanda ya Ziwa na kutamka hadharani kwamba kama watu hawaridhiki na utendaji wake basi waende wakamuue huko ni kukijweza kulikopitiliza kwa kiongozi aliyepewa dhamana ambapo Mhe Samia ameomba tumsaidie kumuonyesha viongozi wa aina hiyo.
Makamba huyo huyo siku ya kusoma bajeti ya Wizara yake Juni 2, 2022 kwa makusudi aliamua kulidharau Bunge kwa kuchelewa kuingia bungeni na Bunge likaahirishwa kumsubiri hadi afike ndio liendee ilikuwa ni kujikweza kwa hali ya juu sana kwa kiongozi mwenye dhamana kubwa kama yake.
Makamba alidaiwa kuwaandaa wabunge maalumu wachangie bajeti yake ili wamsifie kwamba ni Msomi mkubwa aliyesoma Chuo Kikuu cha Havard Marekani huku akijua fika kuwa hakuwa na sifa za kusoma chuo hicho na wala hajawahi kusoma chuo hicho.
Makamba anafanya ziara ya kugawa mitungi ya Taifa Gas mikoani na kuvunja sheri ya ushindani lakini wananchi walipopiga kelele yeye alijibu wanaopinga mpango huo waende wakatapike huko ni kujikweza kwa hali ya juu kwa Waziri wa Serikali.
Lakini Pia tumeshuhudia Rais mwenyewe yuko ziarani mikoa ya Nyanda ya Juu kusini lakini waandishi wanaoripoti taarifa zake ni wa kutoka mikoa hiyo hiyo lakini Makamba yeye anainunua ITV, Mwanchi na Clouds na kutembea na jkundi la waandishi wa vyombo hivyo kutoka Dar es Salaam na kuwaacha wale wa mikoani wanaoripoti habari za Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mawaziri wengine wanaofanya ziara mikoani huko nako ni kujikweza kulikopitiliza.
Mengine mtaendelea wenzangu ya kujikweza kwa Makamba na Viongozi wengine.
Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya wateule wake kuacha kujikweza na badala yake wahudumie wananchi kulingana na viapo vyao.
Mkuu huyo wa nchi amesema hayo leo Jumatatu Agosti, 2022 wakati aliposimama na kuwasalimu wananchi wa Kijiji cha Mayale kitongoji cha Halali kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.
Amesema kama kuna kiongozi hatekelezi hayo apewe taarifa ili achukue maamuzi kwakuwa wamekula kiapo ili kuwahudumia wananchi.
"Lengo ni Tanzania yote ipate maendeleo inanyanyuka watu wote wawe na furaha uchumi ukue na maisha yaendelee" amesema Samia.
Source: Mwananchi Digital AUGUST 08 2022