Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,675
- 40,926
Wakati Rais Magufuli akiwa madarakani tuliwaona mkiandamana nae kila mahali katika ufunguzi wa miradi mbalimbali.
Na wakati mkiandamana naye mlipata nafasi ya kutoa neno na katika kufanya hivyo mliisifia miradi na kutuambia kuwa iko sawa kabisa, tuliwaamini kwakua nyie ndio mliyobeba dhamana yetu kwa nafasi mlizopo.
Vilevile wakati CAG anatoa ripoti zake, hatukuwahi ambiwa kuwa hiyo miradi haifai bali tumekua tukisikia tu kuwa kila kitu kipo sawa. Sasa ghafla baada ya Dr. Magufuli kututoka tunaona kauli tofauti na zile za awali toka kwa watu wale wale.
Binafsi naamini kabisa kwa nafasi zao watu hao walikuwa wasaidizi na kwa namna flani washauri wa Rais kwa mambo mbali mbali, watuambie ni mambo mangapi katika haya tunayoyaona walimshauri Rais vibaya.
Je, majukumu ya CAG ni pamoja na kurecommend umuhimu wa mradi au yanaishia kwenye mahesabu tu?
Ndio kusema kwamba CAG amejitwika majukumu yasiyokuwa yake?
Au kama hayo ndio majukumu yake kwanini ripoti yake ya mwaka jana haikuwa na mambo kama haya, nia ya CAG hasa ni nini?
Mimi nawashauri kama raia mwaminifu ili wasiendelee kutuchanganya kwa kauli ambazo naona kama hazina tija sana kwa kulikuza taifa letu wajiuzulu au Rais awasaidie.
Binafsi naona ni vyema tukajikita kwenye kufanya kazi kuliko kuambiana yaliyopita na ili hayo yafanyike waliopo wajiuzulu nafasi zao.
Rais ateue watu wapya watakaoendana na vision yake.