Viongozi wa Tanzania fuateni misingi ya utawala bora

Nihaomedia7

Member
Jul 19, 2021
32
77
Misingi ya utawala bora kwa miaka kadhaa imekuwa ni adimu kupatikana miongoni mwa viongozi wengi, ambapo kwa kiasi kikumbwa imekuwa ikizorotesha maendeleo ya kiuchumi na kudhoofisha demokrasia nchini. Misingi ya utawala bora katika jamhuri ya Muungano inajumuisha, uadilifu, demokrasia, utawala wa kisheria, haki za binadamu, uwajibikaji, ushirikishwaji wa wananchi, uwazi, umoja wa kitaifa, usawa wa kijinsia, uzalendo, uwazi nakadhalika. Wapo viongozi wanaojitahidi kuifuata kwa kiasi chake huku viongozi wengi wakiipa migongo misingi ya utawala bora.

Wapo viongozi ambao kwa makusudi wamekuwa wakikiuka misingi ya utawala bora, ikiwemo kuminya demokrasia, kuzuia haki za wananchi kikatiba kama vile kuzuia mikutano ya hadhara, maandamano ya amani nakadhalika. Jambo hili sio zuri kwani kufanya hivyo kutazuia kutambua maoni ya wananchi juu uongozi wako na juu ya nchi yao.

Kwakuwa wananchi tunao wajibu wakuhakikisha tunaijenga Tanzania inayoheshimu misingi ya utu, usawa, undugu, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mahakama, amani na mshikamano niwajibu wetu kuikumbusha serikali na viongozi wale tunaowaona kwa namna moja ama nyingine wanakiuka misingi ya utawala bora kuanzia mashinani hadi uongozi mkuu wa taifa.

Vile vile viongozi na vyombo hasa bunge la jamhuri, mnao wajibu wakuhakikisha mnafuata misingi ya utawala bora na kuhakikisha katiba inafuatwa kikamilifu.

Aidha vyombo kama mahakama, bunge na vyombo vya habari vinapaswa kuwa huru katika kufanya shughuli zake, mradi tu havikiuki katiba yetu. Vyombo hivi vinapoingiliwa ni dosari kubwa katika nchi inayojinasibu kufuata misingi ya kidemokrasia.

Pamoja na hayo tukitaka kupiga hatua kwa kuwa na taifa lenye viongozi wanaofuata misingi ya utawala bora, nimuhimu sana kuwawajibisha au kujiwajibisha wenyewe pale inapotekea viongozi kukiuka misingi hiyo.

Mwisho. Demokrasia, amani, utu, uwazi, na uwajibikaji ni muhimu sana kwa taifa letu.
 
Bila shaka wanaelewa misingi ya utawala bora tatizo wametawaliwa na greedness,ubinafsi na njaa ya matumbo na kujiona kuwa hii nchi walipewa kama zawadi, hakuna hata mtoto mmoja wa waziri utakayemkuta anasoma shule za walala hoi kama hapa Lingusenguse au Mwananyamala au Makumira na sitegei hata pale Mbuyuni kama kuna mtoto wa waziri pale,tuendelee kulalama humu
 
Back
Top Bottom