Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Hiyo picha ipo wapi

  • Nigel Whittaker
    Managing Director
  • Anael Samuel
    Managing Director
  • Sebastian Kastuli
    Chief Financial Officer and Officer
  • Agatha Keenja
    Personnel Manager
Ipo ukurasa wa kwanza wa mada hii mkuu 'August'.
 
Ngoja tuangalie mwelekeo wa huyu mama ni upi hasa kuhusu mambo haya.
Mama alishasema yeye na Mwendazake ni kitu kimoja. Kwa hiyo mawazo ya aliyemtangulia yanashabihiana na yake kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwa nini watu wana mashaka? Wanataka Mama aseme nini sasa?
 
Lifanyie kazi hili wazo lieleweke vizuri mkuu, naona kuna matumaini katika wazo lako.

Tusichotaka kamwe, ni hawa viongozi kuendelea kutuhujumu.
Ni kweli halieleweki kwa wengi lakini lipo kwenye mfumo, utekelezaji wake umeshindikana kwa awamu zote pamoja na kuwepo kwenye mipango na kuwahi kujadiliwa bungeni sababu kuu ikiwa kuwa inagusa maslahi ya watu wachache. Anahitajika mtu mwingine mwenye utashi na uthubutu wa kuhakikisha kuwa kinachoamuliwa huko Bungeni kinatekelezwa.

Mali za nchi hii ni zetu sote. Serikiali inamiliki hisa za makampuni na mashirika ya umma kwa asilimia mia, viongozi tuliowachagua ndio wasimamizi wa hizi mali na kwa mamlaka tuliyowapa wanaweza kuamua kuyaendesha kwa kuegemea pale yalipo maslahi yao. Sehemu pekee ya mwananchi wa kawaida kuweza kuhoji juu ya mwenendo wa hizi mali ni kushiriki moja kwa moja kwenye umiliki wa hizi mali kupitia soko la hisa.
 
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).

Hatujawahi kupata mrejesho kutoka kwa Bw. Kilagi kuhusu Songas, ila serikali inamiliki kupitia TANESCO na TPDC.

Mkataba wa kuuza wa umeme wa Songas na TANESCO unaisha ama unategemea kuisha mwaka 2024. Songas imekua na harakati za kutaka kuongezewa mkataba pale mkataba uliopo utakapofika mwisho na kulikua na ugumu kidogo kwani serikali inategemea kua na umeme wa bei rahisi wa maji kutoka JNHPP wa Megawati 2115. Songas wamekua wakitumia ushawishi mkubwa waongezewe mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO.

Mimi binafsi sioni haja ya kuendelea na hawa mabeberu kwani kwa hali ya sasa bado tunajitosheleza, tuna megawati 1600 ikiwemo Songas ya megawati 185 na maximum demand ni megawati 1200 kama alivyosema Rais juzi. Hivyo hata tukiwaondoa Songas sasa hivi bado tunaweza kukidhi mahitaji yetu ya juu kabisa na kusiwepo na shida ya umeme.

Juzi nilimsikiliza mkurugenzi wa TPDC akiongea TBC, alikiri kua bei ya gesi iko juu sana hapa TANZANIA, kwa maana kua TANESCO inauziwa umeme kwa bei ya juu sana na hawa kina Songas na bado inatakiwa kuuzia Watanzania.

Kuna kinyerezi 1, 2, kinyerezi 2 extension, kinyerezi 3, Ubungo 1, Ubungo 2 zote za gesi na kuna mpango wa kujenga hadi kinyerezi 5 ya megawati 600, sasa Songas ya nini tena?

Ni wakati sasa Watanzania tujifunze, haya makampuni ya umeme hapa Tanzania ya binafsi yatatufirisi. Kulikua na Agreko, Symbion, IPTL, Songas na sijui itakuja ipi nyingine.

Ngoja tuone kama mama atawatolea nje hawa jamaa. Mwendazake alikua ametoa nje kabisa hiyo deal ya extension.

Songas ni matokeo ya uongozi wa kipumbavu ulioachia kila kitu kwa faida binafsi. Bila shaka nyuma ya songas kuna mapapa wa kiswahili wengi wa tawala zilizopita ukiondoa wa Hayati Magufuli.
 
Na kama jlikuwa 2024 bas JPM akisubiri hicho kipindi cos kilibaki kidogo najua katu asingeweza kuongeza uo mkataba zaidi kama waketaka mitambo yao angewaambia wafungue watokenayo.

Kwasasa hakuna wakuwaambia Hatutaki haya mambo yenu hamtaki kaeni na mamitambo yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kwamba alikuwa anasubiri hicho kipindi, JPM alishawaambia, 2024 wasipoteze hata sekunde waondoke.

Panafrican na TPDC-GASCO ndo walikuwa wanajengewa uwezo na tayari walishamudu. Visima vya gesi inaendeshwa na watanzania chini ya Panafrican. Walijaribu ku-lobby kipindi cha JPM ndo wakamkera kabisaaaa, 2024 ilikuwa ishaisha, na hakuna aliyepiga kelele, sio balozi wala mstaafu yule.

Ngoja tuone KAZI iendelee kwa kukusanya kodi bila shuruti, kuwavutia wawekezaji, kuruhusu expatriates na kugawana sawa mapato na visiwa.
 
Kama utakumbuka ishu ya IPTL, magufuli alikuta mkataba wa IPTL, hakuona busara kuuvunja ule mkataba kwani muda wake wa kuisha ulikua umebakiza miezi kadhaa, muda ulipoisha akawanyima IPTL leseni, IPTL ikafa kifo cha mende. Hakuna kuvunja mkataba na hakuna gharama zozote za kuvunja mkataba.

Songas pia idea ni hiyo, kuuvunja ule mkataba utaleta shida nyingi na bado Songas ilikua inategemewa kwani miradi kama Kinyerezi imekamilika sio miaka mingi iliyopita, nadhani kuanzia 2017.

Leseni ya Songas inaisha muda wake 2024, mwaka huo huo tutakua na umeme wa Megawati 2115 kutoka JNHPP, hivyo tutakua na sababu zote za kuwanyima leseni Songas na hakuna wa kutudai.

Hiyo ndio akili.
Hawawezi kukuelewa, mungu Antipas amewaambia wabishe mpaka kufa
 
Umenena vema advocate.
 
Sio kwamba alikuwa anasubiri hicho kipindi, JPM alishawaambia, 2024 wasipoteze hata sekunde waondoke.

Panafrican na TPDC-GASCO ndo walikuwa wanajengewa uwezo na tayari walishamudu. Visima vya gesi inaendeshwa na watanzania chini ya Panafrican. Walijaribu ku-lobby kipindi cha JPM ndo wakamkera kabisaaaa, 2024 ilikuwa ishaisha, na hakuna aliyepiga kelele, sio balozi wala mstaafu yule.

Ngoja tuone KAZI iendelee kwa kukusanya kodi bila shuruti, kuwavutia wawekezaji, kuruhusu expatriates na kugawana sawa mapato na visiwa.

..tatizo mkataba unaisha 2024.

..na 2025 ccm inahitaji fedha za kampeni za uchaguzi mkuu.

..hapo ni lazima waweke rehani rasilimali za watanzania.

..tusubiri tuone itakuwaje.

cc tindo
 
Kwa taarifa ni kwamba Songas walianza toka mwaka 2019 mazungumzo ya kutaka waongezewe mkataba na kuahidi kua mkataba mpya watapunguza bei ya umeme wanaoiuzia Tanesco lakini mwendazake alikua amekataa hilo wazo la kuongeza mkataba.

Walikua wanatumia ushawishi wa hali ya juu sana kuongezewa mkataba ila hawakua na uhakika maana mwenzake alikua meshagoma.

Nadhani baada ya JPM kufariki jamaa walishangilia maana sina hakika kama watakataliwa. Tusubiri tuone.

Mikataba ya take or pay ukishaingia mkataba, utumie hicho mlichokubaliana ama usitumie unalipa.

Mashirika yetu haya yanatengeneza hasara kwa sababu ya wanasiasa wasio waaminifu. TANESCO imetwishwa madeni, ATCL imetwishwa madeni, TTCL imetwishwa madeni na yote yanatokana na mikataba mibovu.
Nipo nasali kwa nguvu ili wafuatao wasiwe wabunge wa JMT(2025)
, maana wao ndio MAKUWADI na chochoro za kupitisha ujinga kama huu, kama mnadhani wameachana na siasa mnajidanganya wapo wanajifua kweli kweli na wana backup ya mtandao hadi nje ya nchi!
. Ngereja
. Chenge (aka Joka la Makengeza)
. Chegeni
. Sospeter
. MwamiLuyagwa Kabwe
.......
Leo ngoja niishie hapa!
 
..nilitegemea walau mmoja kati ya hao apigwe marisasi kwa usaliti na kuuza rasilimali zetu. badala yake walenga shabaha wakaelekezwa kummaliza mtanzania aliyetumia ujana wake wote kupigania rasilimali za nchi hii.

cc Pascal Mayalla, Mag3, The Palm Tree , Richard, tindo
 
..tatizo mkataba unaisha 2024.

..na 2025 ccm inahitaji fedha za kampeni za uchaguzi mkuu.

..hapo ni lazima waweke rehani rasilimali za watanzania.

..tusubiri tuone itakuwaje.

cc tindo
NMB, ALAF, TCC,TBL n.k, sijui zimebaki hisa kiasi gani baada ya kunamna gani na wastaafu kujichoteapo kwa mgongo wa uchaguzi pia.w
 
Hiyo picha ipo wapi

  • Nigel Whittaker
    Managing Director
  • Anael Samuel
    Managing Director
  • Sebastian Kastuli
    Chief Financial Officer and Officer
  • Agatha Keenja
    Personnel Manager
Agatha Keenja ni mtoto wa Charles Keenja?
 
Back
Top Bottom