Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,866
2,000
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).

Hatujawahi kupata mrejesho kutoka kwa Bw. Kilagi kuhusu Songas, ila serikali inamiliki kupitia TANESCO na TPDC.

Mkataba wa kuuza wa umeme wa Songas na TANESCO unaisha ama unategemea kuisha mwaka 2024. Songas imekua na harakati za kutaka kuongezewa mkataba pale mkataba uliopo utakapofika mwisho na kulikua na ugumu kidogo kwani serikali inategemea kua na umeme wa bei rahisi wa maji kutoka JNHPP wa Megawati 2115. Songas wamekua wakitumia ushawishi mkubwa waongezewe mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO.

Mimi binafsi sioni haja ya kuendelea na hawa mabeberu kwani kwa hali ya sasa bado tunajitosheleza, tuna megawati 1600 ikiwemo Songas ya megawati 185 na maximum demand ni megawati 1200 kama alivyosema Rais juzi. Hivyo hata tukiwaondoa Songas sasa hivi bado tunaweza kukidhi mahitaji yetu ya juu kabisa na kusiwepo na shida ya umeme.

Juzi nilimsikiliza mkurugenzi wa TPDC akiongea TBC, alikiri kua bei ya gesi iko juu sana hapa TANZANIA, kwa maana kua TANESCO inauziwa umeme kwa bei ya juu sana na hawa kina Songas na bado inatakiwa kuuzia Watanzania.

Kuna kinyerezi 1, 2, kinyerezi 2 extension, kinyerezi 3, Ubungo 1, Ubungo 2 zote za gesi na kuna mpango wa kujenga hadi kinyerezi 5 ya megawati 600, sasa Songas ya nini tena?

Ni wakati sasa Watanzania tujifunze, haya makampuni ya umeme hapa Tanzania ya binafsi yatatufirisi. Kulikua na Agreko, Symbion, IPTL, Songas na sijui itakuja ipi nyingine.

Ngoja tuone kama mama atawatolea nje hawa jamaa. Mwendazake alikua ametoa nje kabisa hiyo deal ya extension.

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,579
2,000
Najiuliza swali gumu; kwa sasa yupo mtu serikalini mwenye ubavu wa kusema NO baada ya JPM kutangulia mbele za haki?

Vv
Na kama jlikuwa 2024 bas JPM akisubiri hicho kipindi cos kilibaki kidogo najua katu asingeweza kuongeza uo mkataba zaidi kama waketaka mitambo yao angewaambia wafungue watokenayo.

Kwasasa hakuna wakuwaambia Hatutaki haya mambo yenu hamtaki kaeni na mamitambo yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,866
2,000
Na kama jlikuwa 2024 bas JPM akisubiri hicho kipindi cos kilibaki kidogo najua katu asingeweza kuongeza uo mkataba zaidi kama waketaka mitambo yao angewaambia wafungue watokenayo.

Kwasasa hakuna wakuwaambia Hatutaki haya mambo yenu hamtaki kaeni na mamitambo yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa taarifa ni kwamba Songas walianza toka mwaka 2019 mazungumzo ya kutaka waongezewe mkataba na kuahidi kua mkataba mpya watapunguza bei ya umeme wanaoiuzia Tanesco lakini mwendazake alikua amekataa hilo wazo la kuongeza mkataba.

Walikua wanatumia ushawishi wa hali ya juu sana kuongezewa mkataba ila hawakua na uhakika maana mwenzake alikua meshagoma.

Nadhani baada ya JPM kufariki jamaa walishangilia maana sina hakika kama watakataliwa. Tusubiri tuone.

Mikataba ya take or pay ukishaingia mkataba, utumie hicho mlichokubaliana ama usitumie unalipa.

Mashirika yetu haya yanatengeneza hasara kwa sababu ya wanasiasa wasio waaminifu. TANESCO imetwishwa madeni, ATCL imetwishwa madeni, TTCL imetwishwa madeni na yote yanatokana na mikataba mibovu.
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,675
2,000
Serikali isijitusu kudumbukia kwenye huu mtego.
Hatuhitaji umeme wa bei ghali kwa sasa. Tu-focus kuimalizia JNHPP.
Songas wajikite kwenye kubadili biashara wajielekeze kwenye kutengeneza gas ya majumbani labda inaweza kuwalipa.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,975
2,000
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).

Hatujawahi kupata mrejesho kutoka kwa Bw. Kilagi kuhusu Songas, ila serikali inamiliki kupitia TANESCO na TPDC.

Mkataba wa kuuza wa umeme wa Songas na TANESCO unaisha ama unategemea kuisha mwaka 2024. Songas imekua na harakati za kutaka kuongezewa mkataba pale mkataba uliopo utakapofika mwisho na kulikua na ugumu kidogo kwani serikali inategemea kua na umeme wa bei rahisi wa maji kutoka JNHPP wa Megawati 2115. Songas wamekua wakitumia ushawishi mkubwa waongezewe mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO.

Mimi binafsi sioni haja ya kuendelea na hawa mabeberu kwani kwa hali ya sasa bado tunajitosheleza, tuna megawati 1600 ikiwemo Songas ya megawati 185 na maximum demand ni megawati 1200 kama alivyosema Rais juzi. Hivyo hata tukiwaondoa Songas sasa hivi bado tunaweza kukidhi mahitaji yetu ya juu kabisa na kusiwepo na shida ya umeme.

Juzi nilimsikiliza mkurugenzi wa TPDC akiongea TBC, alikiri kua bei ya gesi iko juu sana hapa TANZANIA, kwa maana kua TANESCO inauziwa umeme kwa bei ya juu sana na hawa kina Songas na bado inatakiwa kuuzia Watanzania.

Kuna kinyerezi 1, 2, kinyerezi 2 extension, kinyerezi 3, Ubungo 1, Ubungo 2 zote za gesi na kuna mpango wa kujenga hadi kinyerezi 5 ya megawati 600, sasa Songas ya nini tena?

Ni wakati sasa Watanzania tujifunze, haya makampuni ya umeme hapa Tanzania ya binafsi yatatufirisi. Kulikua na Agreko, Symbion, IPTL, Songas na sijui itakuja ipi nyingine.

Ngoja tuone kama mama atawatolea nje hawa jamaa. Mwendazake alikua ametoa nje kabisa hiyo deal ya extension.

Miradi ya aina hii ndiyo wanayoipenda sana wapigaji kuendelea kuwadidimiza waTanzania, na ndiyo maana ya kuwepo na kelele nyingi hata humu JF juu ya serikali kutojihusisha na biashara kama hizi.

Ngoja tuangalie mwelekeo wa huyu mama ni upi hasa kuhusu mambo haya.

Hapa ndipo tutakapoanza kujua kama tumerudi moja kwa moja kwenye awamu ya nne, au tunasafisha uchafu wa awamu ya tano na kuimarisha mazuri yake.

Haitashangaza tukianza kusikia ujenzi wa bwawa sasa unasuasua, kwa mbinu (hujuma) tu za hawa jamaa, na wakala wao!
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,227
2,000
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).
Hii ina harufu kama ile ya TTCL kupokwa kampuni ya Celnet.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,975
2,000
"Viongozi wakuu wa kampuni ya Songas"..., ndio akina nani hao?

Hasa hao watatu waliopo kwenye picha, ni akina nani hao?

Haya mambo tuanze kuwa tunayafanya kwa uelewa, tusiwe tunalalamika tu kijumlajumla bila kujua tunacholalamikia!
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,579
2,000
Kwa taarifa ni kwamba Songas walianza toka mwaka 2019 mazungumzo ya kutaka waongezewe mkataba na kuahidi kua mkataba mpya watapunguza bei ya umeme wanaoiuzia Tanesco lakini mwendazake alikua amekataa hilo wazo la kuongeza mkataba.

Walikua wanatumia ushawishi wa hali ya juu sana kuongezewa mkataba ila hawakua na uhakika maana mwenzake alikua meshagoma.

Nadhani baada ya JPM kufariki jamaa walishangilia maana sina hakika kama watakataliwa. Tusubiri tuone.

Mikataba ya take or pay ukishaingia mkataba, utumie hicho mlichokubaliana ama usitumie unalipa.

Mashirika yetu haya yanatengeneza hasara kwa sababu ya wanasiasa wasio waaminifu. TANESCO imetwishwa madeni, ATCL imetwishwa madeni, TTCL imetwishwa madeni na yote yanatokana na mikataba mibovu.
Ahsante kwa nyongeza mkuu ila hapa unaweza kupima ni nani hasa wanakuwa wanashangilia kifo cha Hayati Magufuli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom