Viongozi wa dini wamvaa Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wamvaa Lema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by issenye, Aug 1, 2011.

1. i

issenye JF-Expert Member

#1
Aug 1, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 1,146
Likes Received: 989
Trophy Points: 280
[h=2]Wadau tujadili hii habari[/h]

“Tunamtaka Lema aache mara moja siasa za vurugu, uchochezi, matusi na vitisho kwa kuwa migogoro katika sekta zote ni kikwazo cha maendeleo. Fujo zake ni kuwapumbaza wananchi ili miaka ipite akiendesha siasa chafu na vurugu. Atimize ahadi alizotoa kwa wananchi.
NA SHAABAN MDOE, ARUSHA

VIONGOZI wa madhehebu ya dini jijini Arusha, wamemuonya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, aache siasa chafu za kuchochea vurugu. Wamesema siasa chafu zinazofanywa na Lema zinalenga kuwasahaulisha wananchi ahadi alizowapa, ambazo hadi sasa hajazitekeleza zaidi ya kuhamasisha vurugu na maandamano. Hayo yamo kwenye tamko lililotolewa na viongozi wa dini na kutiwa saini na Askofu wa Kanisa la Blazing Alter, Issaya Sizya. Viongozi hao wamesema hawako tayari kuona amani ikivunjika. Alisema haoni mantiki ya Lema kuendeleza malumbano na vurugu zisizo na tija kwa wananchi, kwa kutangaza kutoutambua muafaka uliofikiwa kuhusu Meya wa Jiji la Arusha, huku akifahamu vikao vyote vilivyokuwa vikifanyika.
“Kama Lema aliona muafaka huo haukufuata taratibu, alipaswa kutoa taarifa kwa chama chake ili madiwani na viongozi waliohusika wazuiwe kuendelea na mchakato huo. Haya anayotaka kuendeleza ni kuwavuruga wananchi na kuhatarisha amani,” alisema. Askofu Sizya alisema kitendo cha Lema kuendeleza siasa chafu kinawadhalilisha viongozi wenzake na kina dhihirisha yeye ni kiongozi asiyeshaurika na mwenye kuamini mawazo yake ndiyo sahihi kuliko ya wengine. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Lema ameonyesha ishara mbaya ya kutaka kutawala jimbo la Arusha Mjini kwa kumwaga damu, na kwamba kamwe viongozi wa dini hawatakuwa tayari kuacha hilo liendelee. Walikemea maandamano yanayoratibiwa na Lema mara kwa mara, wakisema ni ya hatari na yanazorotesha uchumi wa Arusha na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi. “Tunamtaka Lema aache mara moja siasa za vurugu, uchochezi, matusi na vitisho kwa kuwa migogoro katika sekta zote ni kikwazo cha maendeleo. Fujo zake ni kuwapumbaza wananchi ili miaka ipite akiendesha siasa chafu na vurugu. Atimize ahadi alizotoa kwa wananchi,” ilisema sehemu ya tamko hilo.
Viongozi hao walisema wananchi wa Arusha Mjini wana kero nyingi, zikiwemo za msongamano wa magari, uhaba wa majisafi na salama na ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi cha Ngulelo na Kisongo, ambazo ni sehemu ya ahadi zake kuwa atazitatua.
Walisema ahadi nyingine ni za ujenzi wa jengo la Machinga Complex, hospitali kubwa tatu na ukarabati wa miundombinu ya majitaka.

Source: Gazeti la udaku Uhuru

2. ChaterMaster

ChaterMaster JF-Expert Member

#2
Aug 2, 2011
Joined: Aug 17, 2009
Messages: 1,280
Likes Received: 405
Trophy Points: 180
USHASEMA CHANZO NI GAZETI LA UDAKU UHURU-Basi hamna haja hata ya kujadili yaandikwayo na magazet ya kufungia maandaz!

"THE ONLY ABSOLUTE TRUTH IS THAT THERE ARE NO ABSOLUTE TRUTHS"

3. d

dotto JF-Expert Member

#3
Aug 2, 2011
Joined: Sep 29, 2010
Messages: 1,720
Likes Received: 18
Trophy Points: 135
Huyu Askofu alipewa uaskofu na nani!!. Umoja upi wa maaskofu!!?? Alichakachua uaskofu ili apate sadaka kwa jeuri yake!!

4. j

janja pwani Senior Member

#4
Aug 2, 2011
Joined: Jul 27, 2011
Messages: 104
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
wabunge wengi wa chadema hawatarudi bungeni wengi wameendekeza kutafuta umaarufu kupitia bunge huku wamesahau kutimiza ahadi zao majimboni

5. n

ngwendu JF-Expert Member

#5
Aug 2, 2011
Joined: Jun 7, 2010
Messages: 1,967
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
mkuu hilo mbona liko wazi. wengi tunajua hivyo isipokuwa mazezeta machache tu ambayo yamelishwa jaziba kama lile lililomuuliza ndugai kuhusu ushaidi wa akina lema na lisu. Jaziba.

6. menyidyo

menyidyo JF-Expert Member

#6
Aug 2, 2011
Joined: Oct 9, 2010
Messages: 1,339
Likes Received: 14
Trophy Points: 135
Tupa kule vuta nyingine.

7. Lole Gwakisa

Lole Gwakisa JF-Expert Member

#7
Aug 2, 2011
Joined: Nov 5, 2008
Messages: 3,962
Likes Received: 403
Trophy Points: 180
Mwaka mmoja umeshapita na kwa Arusha hakuna lolote bali malumbano yanayoishia makao makuu ya CDM.
Kubomoa rahisi ngoma ipo katika kujenga.

8. Mumwi

Mumwi JF-Expert Member

#8
Aug 2, 2011
Joined: Jan 9, 2011
Messages: 592
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Huyo Mchungaji Isaya mi simtambui kama askofu alijifanya ni rafiki Wa mbunge Lema sasa hivi baada ya kuona hajapata alichokuwa anataka ndo kamgeuka Hutu mchungaji njaa tu inamsumbua askofu gain kanisa lake lina waumini hawafiki hata kumi ndo anajiita askofu alikuwa na kesi na muumini wake ambaye alitoa milioni kumi ajengee kanisa yeye kala ndo kashtakiwa.

9. Arafat

Arafat JF-Expert Member

#9
Aug 2, 2011
Joined: Nov 17, 2009
Messages: 2,582
Likes Received: 41
Trophy Points: 0
Nipeni kwanza hile list ya wauza madawa ya kulevya niipitie maana nilisikia kuna watu wanajiita Maaskofu wamo katika list hile ndipo nichangie hii hoja

10. Safety last

Safety last JF-Expert Member

#10
Aug 2, 2011
Joined: Mar 24, 2011
Messages: 4,224
Likes Received: 164
Trophy Points: 160
I always say Lema ni Tingatinga

11. jogi

jogi JF-Expert Member

#11
Aug 2, 2011
Joined: Sep 25, 2010
Messages: 19,335
Likes Received: 12,799
Trophy Points: 280

umekalia big G na ni lazima uba..n..duli..we. unakura moja tu, unaihukumuje kura yangu!!

12. Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

#12
Aug 2, 2011
Joined: Nov 25, 2010
Messages: 31,784
Likes Received: 36,779
Trophy Points: 280
Is it credible source???

13. Kimilidzo

Kimilidzo JF-Expert Member

#13
Aug 2, 2011
Joined: Jan 3, 2011
Messages: 1,346
Likes Received: 38
Trophy Points: 135
Wewe ndio Zezeta....

Mbona JK alituahidi maisha bora akatupa maisha bomu halafu wewe kwa uzezeta wako na upunuani ukampa kura kurudi bungeni...

Hata kama mumeo ni mwana CCMagamba hayo ni mambo yenu ya ndani ya nyumba usilazimishe kila mtu kupenda magamba, hata kabla ya uchaguzi mlisema wengi hawatarudi ikawa kinyume. Wewe kura yako ni moja tu, labda ya pili ndio hiyo ya mumeo usiwasemee wanachi wengine.

14. A

AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

#14
Aug 2, 2011
Joined: Feb 8, 2011
Messages: 274
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

hivi hili gazeti bado kuna watu wanatoa pesa zao kununua kweli,maana huku mtaani kwetu nina miaka kadhha sijaliona

15. yutong

yutong JF-Expert Member

#15
Aug 2, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 1,604
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
Kwani hiki si kipindi cha bunge kaka? wewe unategemea waache bunge aende kutekeleza ahadi gani wewe? hivi unadhani kutekeleza ahadi si kunaanzia bungeni? kama hivyo basi wabunge wote wa CCM hawatorudi kabisaaaa bungeni maana sioni wanachotekeleza. CCM mmejisahau sana na kuona kama sisi wapumbavu sana, hivi hamjui sasa hivi mnajisaidia choo cha magunia kisicho na mlango? Usijione umesimama angalia usije ukaanguka.

16. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#16
Aug 2, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,558
Likes Received: 1,916
Trophy Points: 280
Si nasikia kuna wengine ni madrug dealers?Hawa unaweza kuta wanapiga kelele ili kuficha madhambi yao.Maaskofu gani hao.Habari yenyewe pia kweli ka udaku.Ni viongozi wa madhehebu gani hayo?Jina la kanisa lenyewe limekaa kitapeli tapeli,eti blazing Alter,what da....
Kwenye upande wa changamoto walizompa Lema,ni wazi atazifuatilia hizo ahadi alizowapa wananchi.Tuna muencourage kufanya hivyo.

17. yutong

yutong JF-Expert Member

#17
Aug 2, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 1,604
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
wanajipendekeza kwa vasco dagama II aka mawingu

18. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#18
Aug 2, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 104
Trophy Points: 145

watu kama huyu wasioweza kuona kwamba miaka 50 chini ya magamba hatujapata maendeleo na bado wanaisfia huku wakihoji maendeleo ya arusha kwa miezi tisa ni janga la familia zao na taifa kwa ujumla. Si ajabu ukaongezeka kwenye list ya watakaojitoa roho 2015 chadema itakapochukua uongozi wa nchi.

19. only83

only83 JF-Expert Member

#19
Aug 2, 2011
Joined: Oct 15, 2010
Messages: 5,252
Likes Received: 445
Trophy Points: 180

Naomba kusema kuwa;

Moja,hao viongozi wa dini sijawai wasikia ni wa madhehebu gani?

pili,ukisoma UHURU unaweza ukapata matatizo ya kufikiri...

20. LiverpoolFC

LiverpoolFC JF-Expert Member

#20
Aug 2, 2011
Joined: Apr 12, 2011
Messages: 11,001
Likes Received: 153
Trophy Points: 160

Mkuu! Hapo umemaliza sina la nyongeza. Naunga mkono 100%

Loading...