Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
107
Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa

Monday, 08 November 2010
Salim Said

JOPO la viongozi wa dini limefanya ziara ya ghafla kwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Wiilibrod Slaa na kumtaka akubali matokeo au atumie njia za kisheria kudai haki yake, Mwananchi imebaini.

Dk Slaa hakutokea kwenye hafla ya kutangaza mshindi wa kiti cha urais wala sherehe za kuapishwa kwa Jakaya Kikwete kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano na aliahidi kuwa angetoa tamko zito jana.

Wakati Tume ya Uchaguzi (Nec) ikiendelea kutangaza matokeo, Dk Slaa aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa hangekubaliana na matokeo kutokana na kubaini kuwa Nec ilikuwa inatangaza matokeo tofauti na yaliyo kwenye nyaraka walizosaini na hivyo kuitaka isitishe zoezi hilo ili kura zianze kuhesabiwa upya.

Dk Slaa pia aliituhumu Idara ya Usalama wa Taifa kuwa ilihusika kuchakachua kura kwa lengo la kumbeba mgombea mmoja wa urais, tuhuma ambazo ziliifanya taasisi hiyo, inayofanya kazi kwa siri, ijitokeze hadharani kujibu na kumuelezea katibu huyo mkuu wa Chadema kuwa "ni mzushi".

Tamko hilo la Dk Slaa lilionekana kuwashutua viongozi wa dini na kuhisi dalili za kutokea mvutano ambao ungeweza kusababisha kuvunjika kwa amani.

Mwananchi imebaini kuwa ziara ya kimya kimya ya viongozi hao wa dini ilifanywa wiki iliyopita kabla ya Nec kumtangaza Kikwete kuwa ni mshindi.

Kwa mujibu wa habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kwamba viongozi hao walimtaka Dk Slaa asisababisha mvutano ili kudumisha amani ya nchi.

Habari za ziara hiyo ya dharura ya jopo hilo la viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu zilithibitishwa na meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu. Profesa Baregu aliiambia Mwananchi kuwa ujumbe mkubwa uliofikishwa na jopo hilo ulikuwa ni kuwaomba viongozi wa Chadema kutumia njia sahihi za kudai haki yao ambazo hazitazusha vurugu, fujo wala uvunjifu wowote wa amani.

" Ujumbe wao kwetu ulikuwa ni kutuomba kwamba kusiwe na vurugu, fujo wala uvunjifu wowote wa amani wakati wa kutangazwa matokeo na hata baada ya kutangazwa, " alisema Profesa Baregu. "Badala yake wakatuomba kama hatujaridhika na matokeo basi tutumie taratibu za kisheria zilizowekwa kudai haki. Lakini sisi tuliwaeleza kuwa hatuna nia ya kufanya vurugu wala kuandamana, lakini uchaguzi umevurugwa na hatuwezi kukubali."

Alisema jopo la viongozi hao wanne wa dini wakiongozwa na askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa lilifanya ziara hiyo baada ya Chadema kuitaka Nec kusitisha utangazaji wa matokeo kwa kuwa Usalama wa Taifa wamechakachua matokeo.

"Sijui walikuwa na wasiwasi gani au nani aliwashauri kuja tena kuonana na viongozi wa Chadema, lakini nadhani ni baada ya kuona tumesema hatungekubali matokeo kwa kuwa uchaguzi umechafuliwa, " alisema Profesa Baregu.

Alisema pamoja na wasiwasi huo wa viongozi wa dini, Chadema haikuwa na mpango wowote wa kuunganisha nguvu ya umma na kuingia barabarani, kama ilivyofanyika Kenya, kudai haki. "Lakini hatujaridhika na matokeo kwa sababu uchaguzi ulikuwa mchafu.

Rais amechaguliwa na robo tu ya wapigakura. Nec imeongeza majina kwa sababu kabla ya uchaguzi ilisema wapigakura wote ni 19.9 milioni, lakini akitangaza mshindi Jaji Lewis Makame anasema ni 20.1, hatujui wametoka wapi, " alisema Profesa Baregu.

Kwa mujibu wa Baregu wengine waliokuwamo katika msafara huo wa viongozi wa dini walikuwa ni kutoka Kanisa Katoliki na Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata).
 

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,145
880
Dr angewafukuza wanafiki wakubwa hawa, kama kweli wanaipenda amani wangeanzia kuiambia CCM iache kuwadhulumu watanzania haki yao kwa kuchakachua matokeo ya urais. Lakini wanakaa kimya halafu tuwaeleweje!
 

Kidege

Member
Jul 18, 2009
87
7
viongozi wetu wa dini wanahubiri amani huku waki-support wizi na udanganyifu
 

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Ni viongozi wapi walio mfuata, Ebu tupenyezee kidogo. Isije kua kama wale waliojiita ni waandishi wa habari kumbe 70% walikua ni usalama wa taifa Dr. akagundua na akaahirisha kikao na waandishi wa Habari.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,518
6,090
MAJIZI MAKUBWA HAYA..JITU linaiba kura linajichekesha jekesha tu kazi kucheza viduku ikulu wanataka kuleta mambo ya ajabu hapa
 

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
139
Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa
"Rais amechaguliwa na robo tu ya wapigakura. Nec imeongeza majina kwa sababu kabla ya uchaguzi ilisema wapigakura wote ni 19.9 milioni, lakini akitangaza mshindi Jaji Lewis Makame anasema ni 20.1, hatujui wametoka wapi, ” alisema Profesa Baregu.

Ina maana shughuli yote ile kumbe Prof wangu alikuwa akishindania wapiga kura laki mbili tu katika nchi yenye watu milioni 45!!!!
 

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
Dr angewafukuza wanafiki wakubwa hawa, kama kweli wanaipenda amani wangeanzia kuiambia CCM iache kuwadhulumu watanzania haki yao kwa kuchakachua matokeo ya urais. Lakini wanakaa kimya halafu tuwaeleweje!

wanafiki wakubwa hao, mbona zanzibar kwa seif hawakuenda? au kwa sababu ni mwenzetu. Ujinga huu unakera sana. Wamuache tu aumie kivyake kama ilivyokuwa kwa seif.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,920
3,210
Dk Slaa Fukuza hao wanafiki.

Kwa nini hao Viongozi wa dini hawakusema na NEC??

Kwa nini hao viongozi wa Dini wasingewaambia CCM wasichakachue kura.

Hao viongozi wa dini wameshiba na hivyo hawatetei masilahi ya watanzania
 

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
56
Ina maana shughuli yote ile kumbe Prof wangu alikuwa akishindania wapiga kura laki mbili tu katika nchi yenye watu milioni 45!!!!

quote_icon.png
Originally Posted by Shaycas
Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa
"Rais amechaguliwa na robo tu ya wapigakura. Nec imeongeza majina kwa sababu kabla ya uchaguzi ilisema wapigakura wote ni 19.9 milioni, lakini akitangaza mshindi Jaji Lewis Makame anasema ni 20.1, hatujui wametoka wapi, " alisema Profesa Baregu.


prof baregu hakuwa akipigani wapiga kura 200,000, yeye alisema wapiga kura mil 19.9, ni wengi , ukilinganisha na watu wenye umri wa kupiga kura
 

Mimibaba

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
4,558
1,285
Hawa watu ni hatari. Wanalinda sana madhambi ya watawala kwa kutudanganya waumini kwa kisingizio cha amani na utulivu. Mbona Yesu alikabiriana na udhalimu hivyo hivyo. Mungu ameshaadhibu mataifa kwa sababu ya uongozi batili. Adhabu tuliyonayo Tanzania ya maisha magumu, ufisadi ni dhahiri ni ghadhabu ya Mungu. Kwa sisi wote wenye imani na Dr. Slaa tumtie moyo apiganie haki zetu kwa sababu Mungu anasikia vilio vya sisi wanyonge wenye kuporwa haki kupitia utaratibu halali za sanduku la kura. Napenda kuwaomba wote kuwa hili siyo suala la Dr. Slaa bali letu sote tulioporwa haki hata kama ni kura moja.
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,889
1,007
Hawa watu ni hatari. Wanalinda sana madhambi ya watawala kwa kutudanganya waumini kwa kisingizio cha amani na utulivu. Mbona Yesu alikabiriana na udhalimu hivyo hivyo. Mungu ameshaadhibu mataifa kwa sababu ya uongozi batili. Adhabu tuliyonayo Tanzania ya maisha magumu, ufisadi ni dhahiri ni ghadhabu ya Mungu. Kwa sisi wote wenye imani na Dr. Slaa tumtie moyo apiganie haki zetu kwa sababu Mungu anasikia vilio vya sisi wanyonge wenye kuporwa haki kupitia utaratibu halali za sanduku la kura. Napenda kuwaomba wote kuwa hili siyo suala la Dr. Slaa bali letu sote tulioporwa haki hata kama ni kura moja.
Kuna ukweli katika message yako
 

Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
78
dunia nzima wanafiki namba moja ndio hao wajiitao viongozi wa dini ndo waliomshauri mchakachuaji apunguze uhuru wa vyombo vya habari, na ndio hawahawa walikuwa wanapiga kampeni kwenye nyumba za ibada na ndio hawa hawa wamegeuza taasisi zao kuwa za kibiashara maadili yako wapi shame on hypocrites religious leaders you are ccm cadres and you are benefiting from the corrupt systems!:doh:
 

3D.

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,013
279
Viongozi wa dini ni wanafiki sana. Bahati mbaya Watanzania wengi kutokana na elimu ndogo wanakwenda kichwa kichwa makanisani na misikitini. Ikiwa nitaridhika kuwa Dr. Slaa amepooza kwa sababu ya viongozi wa dini hatopata kura yangu tena.
 

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Hawa viongozi wa dini wanadhalilisha imani za waumini wao kwa kukingia kifua uozo unaofanywa na watawala, CCM na NEC. Hii inakatisha tamaa kweli-kweli! Badala ya kuwa imara kama Askofu Mkoba wa Zimbabwe kumsema Mugabe kwa kudhulumu, hapa wanakuwa wanafiki? aibu!

Na wanaposhauri kupipa kisheria na wanajua urais haupingwi mahakamani si unafiki na ushauri mbovu?

Chadema wawe na maamuzi thabiti kichama na kama ni sheria, kwa ushahidi waliokwishakusanya, wawashtaki Makame, Kiravu na maafisa usalama ambao chadema kimefichua kuwa waliongoza au kusimamia uvunjifu huu wa haki, kuharibu uchaguzi, kuhatarisha amani na demokrasia.

Hapo ndipo wananchi na taifa litapona vidonda vya uharibifu waliofanya.
wananchi wanasubiri hatua na maamuzi ya haraka ya kisheria ya chadema
nawasilisha
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,696
1,681
Kwa Matokeo ya Ubunge CHADEMA wanaweza kwenda mahakamani . . .

Lakini je kwa matokeo ya Urais, watafuata utaratibu gani wa sheria?
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,889
1,007
Kwa Matokeo ya Ubunge CHADEMA wanaweza kwenda mahakamani . . .

Lakini je kwa matokeo ya Urais, watafuata utaratibu gani wa sheria?
Naomba swali hili aulizwe Dr Mokiwa. Labda kama zile milioni 10 alizichukua.
 

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Roho inauma sana, hasa pale inapotegemewa dini ziondoe na kuvunja dhuluma, ndiyo zinazidi kuwaondolea wananchi hata ile haki kidogo wanayotaka kuijenga na kuitetea!
hawa mafisadi ni mkono wa ibilisi, na yeyote anayesimama upande wao, naye ni baba wa uovu.
tanzania inahitaji ukombozi.
dini ni mambo ya kiroho, ila wanasahau kama mwili una mateso, hata dini haikubaliki popote. wao wana-assume kuwa raia watateseka kimwili na papo hapo waweze kutii dini? kamwe haitatokea. wakumbuke darfur, congo, rwanda, irak, afghan nk. hawataki hata kuisikia neno dini, kwani haijawaondoa ktk machungu ya dhuluma zilizowapata.

haki kwanza, ndipo imanina dini itapata nguvu.
 

rastaman

Member
Nov 1, 2010
41
0
Roho inauma sana, hasa pale inapotegemewa dini ziondoe na kuvunja dhuluma, ndiyo zinazidi kuwaondolea wananchi hata ile haki kidogo wanayotaka kuijenga na kuitetea!
hawa mafisadi ni mkono wa ibilisi, na yeyote anayesimama upande wao, naye ni baba wa uovu.
tanzania inahitaji ukombozi.
dini ni mambo ya kiroho, ila wanasahau kama mwili una mateso, hata dini haikubaliki popote. wao wana-assume kuwa raia watateseka kimwili na papo hapo waweze kutii dini? kamwe haitatokea. wakumbuke darfur, congo, rwanda, irak, afghan nk. hawataki hata kuisikia neno dini, kwani haijawaondoa ktk machungu ya dhuluma zilizowapata.

haki kwanza, ndipo imanina dini itapata nguvu.
that is why i believe in myself.
Viongozi wa dini upuuzi mtupu. kuwaibia waumini wao sadaka tu. na kujikomba kwa watawala wadharimu.
hakuna kitu hapo wote wamefilisika kimawazo.
wewe tembelea makanisa, misikiti mahubiri wanayo toa ni kutoa sadaka na zaka ili wale washibe.
the white guys were very smart enough. the brought jesus story and paradise after death story to make us good slaves and servants. Uongo mtu. believe in yourself. that is all. mtu asikudanganye eti kuna dini.. unafiki na wizi mtu huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom