Viongozi wa Dini wahimizwa kuwahamasisha Waumini kutunza mazingira (ujumbe katika Mkutano wa 52 wa Ahmadiyya)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis ametoa rai kwa viongozi na Taasisi za Kidini Nchini kushiriki ipasavyo kuhimiza utunzaji wa mazingira ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

Naibu Waziri ametasema hayo Septemba 30, 2023 Ilala, Jijini Dar es Salaam alipokuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango kwenye Mkutano wa 52 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya eneo la Ahmadiyya Centre lililopo Kitonga, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
photo_2023-09-30_22-09-01.jpg
Amesema viongozi wa Dini wanayo nafasi ya kuwahamasisha Wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, ambapo amedai kuwa mbinu wanayoweza kuitumia ni pamoja na kutenga fungu maalumu kwa ajili ya hamasa na kutoa elimu.

"Nataka niwaambie viongozi wa dini hakikisheni mnatoa elimu ya mazingira, kadri mtakavyokuwa mnapata fedha zenu wekeni fungu maalum la kuhamasisha utunzaji kukataza uchafuaji wa mazingira tusielekee kwenye athari kubwa za mabadiliko ya tabia ya Nchi," amesema Naibu Waziri.
photo_2023-09-30_22-09-10.jpg
Ameshauri kwa msisitizo kwamba "Kwanza tutoe elimu tupate nafasi tuzungumzie mazingira maana hata tukizungumzia Mitume waliopita nao walikuwa wanatunza mazingira kwa namna yao na kwa wakati huo, lakini kikubwa tupandeni miti kwa wingi kila tunapofanya matukio yetu (event) tupandeni miti."

wa upande wa Jumuiya ya Ahmadiyya, Naibu Amir Abdulrahman Mohamed Ame amesema kuwa wanaunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira na kuwa wapo tayari kushirikiana kwa pamoja katika kuhamasisha jamii tunza mazingira.
photo_2023-09-30_22-08-56.jpg

photo_2023-09-30_22-09-38.jpg
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa viongozi wa dini wanayo nafasi ya kutumia nafasi zao kukemea mmomonyoko wa maadili kwenye jamii na kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kusimamia maadili hususani malezi bora kwa Watoto.

mesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni kwenye jamii kumekuwepo na mmonyoko wa maadili ambapo amedai viongozi wa dini hawana budi kukemea vitendo, hivyo alivyodai ni kinyume na tamaduni pamoja na miongozo ya kidini.

Hata hivyo, Naibu Amir, Abdulrahman Mohamed ameeleza malengo ya mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka akisema:

"Mkutano huu unafanyika ili kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwa washiriki, na tunakumbushana juu ya kumjua vyema Mwenyezi Mungu, kuonesha upendo na moyo wa huruma na kuongeza upendo baina yatu kwa kujenga udugu baina yetu wa ukarimu na ustaimilivu vyote hivi viweze kuwa ndani yetu."

Ameongeza mkutano huo ambao unafanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 29, 2023 pia wanautumia kufanya tathimini mbalimbali za utendaji na kukumbushana masuala tofauti tofauti kwa lengo la kukuza na kustawisha jumuiya hiyo ambayo inadaiwa kuwa na waumini maeneo mbalimbali nchini.

Jumuiya hiyo imekuwa itekeleza na kutoa huduma mbalimbali kwenye jamii ikiwemo katika sekta ya elimu, maji na afya.

Naibu Waziri Khamis amepongeza jitihada zao ikiwemo suala la uchimbaji wa visima kwa ajili ya kuwezesha Wananchi kupata maji safi na salama.

Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya ilianza kutambulika rasmi kisheria hapa Nchini Tanzania mnamo Mwaka 1936 ikiwa makao makuu yake makuu yapo Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka nje ya Tanzania ambao wanashiriki mkutano huo ni pamoja na Amir na M'bashiri Mkuu jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Ghana, Muhammad bin Salih ambapo kwa Afrika Taifa la Ghana linatajwa kuwa na waumini wengi wa Jumuiya hiyo ikilinganishwa na mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom