Viongozi wa Dini wafanya Maombi Maalum ya kuombea Mvua inyeshe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,980
GOOD NEWS FOR ALL MINISTY
MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBA MUNGU MVUA MERARANI - SIMANJIRO

PRESS RELEASE 17 JANUARI 2022
BISHOP CHARLES GADI

Ndugu Watumishi wa Mungu, Maaskofu wachungaji, manabii mitume, walimu wainjiliti wazee wa kanisa na Waandishi wa Habari,

Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo. Awali ya yote napenda kuwashukuru kwa kuja kunisikiliza katika mkutano huu maalum utakaombatana na maombi maalum ya kuombea mvua.

Dhumuni kubwa la mkutano huu ni kutangaza kuendelea kwa maombi rasmi ya kumuomba Mungu Mvua kubwa za kutosha za neema katika wilaya yetu ya Simanjiro na nchi yetu yetu ya Tanzania kwa ujumla. Mzigo wa maombi haya ulikuja kwa sababu mamlaka za hali ya hewa zilishaonyesha kwamba hata kama mvua zitakuwepo lakini zitakuwa chini ya kiwango cha wastani na katika maeneo mengi hazitatosheleza kukuza mazao ya msimu wa vuli na hivyo kuleta tishio upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo hapa nchini. Mpaka tunapoongea leo 17 januari 2022 bado tunashuhudia mvua chache sana hususani zile zilizotakiwa kunyesha mwezi November na December 2021.

Hiyo ina maana kwamba maeneo mengi ya nchi hawajaweza kuvuna mazao ya Vuli, au yaliyopo yanaelekea kukauka kabisa. Na kwa kuwa Rais wetu ameshatoa wito kwa watu wa dini zote kumwomba Mungu ili tuweze kuwa na mvua ya kutosha, Askofu Dr. Charles Gadi kwa kushirikiana na watumishi wa Mungu toka makanisa, dini na madhehebu mbali mbali wetu tumeshaanza mchakato wa kuendesha maombi katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Tulianza kuomba pale Dodoma, Tarehe 8 Januari, ambapo tuliendesha mkutano wa kuombea nchi na mvua pale Dodoma mjini na tunamshukuru Mungu tayari dalili za mvua kuanza kunyesha maeneo mbali mbali hapa nchini zimekwisha kujionyesha. Tunawashukuru Watanzania bila kujali dini zao wala itikadi kwa kuamua kumlilia Mungu kwa ajili ya upatikanaji wa Mvua. Pia tunazo taarifa kwamba mamlaka ya hali ya hewa imetangaza jana 16 januari kwamba kutakuwa na tishio la mvua kubwa zitakazosababisha usumbufu na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Pwani, Arusha, Manyara na Kilimanjaro pamoja na baadhi ya mikoa mingine. Sisi tulimwomba Mungu na tunaendelea kumwomba Mungu mvua ya Neema, kubwa ya kutosha lakini isiyo na madhara kwa maisha ya wananchi na mali zao, wala kuharibu miundo mbingu ya maendeleo.

Ndugu Watumishi wa Mungu na Waandishi wa habari,
Tumekuja katika wilaya hii ya Simanjiro baada ya kuona taarifa zinazosambaa mitandaoni toka kwenye vyanzo mbali mbali vya habari kwamba Zaidi ya ng’ombe 62000 wamekufa na wengine wapo hatarini kufa kwa sababu ya ukosefu wa malisho na maji. Jambo hili si zuri na ni muhimu sana tumwombe MUNGU AINGILIE KATI kwa sababu pamoja na kilimo, lakini ufugaji ni uti wa mgongo wa uchumi wa wilaya hii.

Ingawa kwa sasa si msimu wa kulima katika wilaya hii lakini wanyama wa kufugwa hawana msimu wa chakula, hivyo tunaamini zikianza kunyesha mvua mapema nyasi na malisho mengine yatamea na hivyo kuokoa wale ambao wapo hatarini kufa kwa njaa na kiu. Wapendwa, mvua ni muhimu si tu kwa kilimo bali kwa wanyama wa kufungwa, wanyama mwitu wanaotuingizia pato kubwa la Taifa kwa shughuli za utalii, mazao ya kudumu, misitu na uoto wa asili, vyanzo vya maji ya kunywa na yale yanayozalisha umeme. Hivyo kukosekana kwa mvua kunaathiri shughuli, huduma na viumbe hai vya kila namna katika dunia.

Watumishi wa Mungu na waandishi wa habari, Kuomba Mvua ni jambo linalokubalika Kibiblia kwani mara nyingi Mungu amedhihirisha katika Neno lake kwamba Mvua ni hazina yake nzuri na ndiye mwenye uwezo wa kuifunga au kuiachilia. Ingawa zipo sababu za kisayansi na kijiografia kusababisha miaka ya ukame, lakini hata hivyo Mungu ana uwezo na anapenda kuingilia kati hali hiyo na kuwaeletea watu wake neema ya mvua wanapomwomba. Mfano katika 2 Nyakati 7:13-14 aliwaambia wana wa Israell: “Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” Tena alisema katika Kumbukumbu la Torati 28: 12 aliwaahidi Wana wa Israeli: “Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.” Baada ya kujihakikishia kuwa mvua ni mali ya Mungu basi tunao ujasiri wa kumwomba, lakini si hilo tu, bali pia ametuahidia kupitia Yesu kristo kwama Lolote tutakalomwomba kwa Jina la Yesu atatupatia. Huu ndiyo uhakika na ujasiri tulio nao kwa Mungu sawasawa na ahadi zake.

Kabla ya kuomba mvua tutatumia nafasi ya mwanzo kumwombea mheshimiwa Rais wetu, Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake na viongozi waandamizi wawe na afya njema, nguvu, hekina na uwezo wa kuendelea kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao mema ya kuliletea taifa letu maendeleo. Pia tutaombea sekta mbali mbali za kiuchumi, na kijamii katika nchi yetu ili viendelee kufanikiwa katika kuboresha hali ya maisha ya watanzania.

Ndugu watumishi wa Mungu na waandishi:
Sambamba na kumwomba Mungu mvua, lakini tunao wajibu wa kutunza mazingira yetu, vyanzo vya maji na misitu yetu ya asili ambayo Mungu ameshatupatia kwa ajili ya kuhifadhi unyevunyevu na kunyonya hewa ya ukaa (Co2)ambayo ikizidi kwenye anga husababisha ongezeko la joto. Aidha tunao wajibu wa kutunza mito na maziwa yetu ambayo ni hazina kubwa Mungu aliyotujalia Tanzania, ambapo nchi nyingi duniani hawanavyo. Hivtyo tunatoa wito kwa serikali, mashirika na watu binafsi katika nafasi zao kuhakikisha kwamba hivi vinalindwa ili kusaidia hali endelevu ya utunzaji wa mazingira.

Kabla sijamaliza nipende kuwakumbusha kwa wale waliokuwa wakitufuatiliua, tumeanza kuombea maswala ya mvua, mazingira, na dhidi ya majanga mbali mbali tangu mwaka 2006 Januari ambapo rais wa wakati huo, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kwanza aliwaomba wananchi kumwomba Mungu kwa ajili ya mvua, maana kuna ukame mkali ulikuwa unaitafuna nchi. Hata mabwaya yetu ya kufua umeme na vyanzo vyetu vya maji vilikuwa vimekauka, hususani bwawa la Mtera.

Watumishi wa Mungu na waandishi wa habari;
Tulianza maombi ya namna hiyo katika viwanja vya Jangwani mwezi 2006 mara baada ya wito wa Rais wa wakati huo, na kisha tukazunguka mikoa mbali mbali hapa nchini ikiwemo Mtera Bwawani, na kumwomba Mungu alete mvua. Kufikia mwezi wa tatu mwaka huo mvua nyingi zilinyesha nchi nzima na kuondoa lile tishio la ukame. Mito na mabwawa ya umeme yalijaa na kuondoa mgao mkali wa umeme uliokuwa umeanza. Baada ya hapo tulizunguka nchi mbali mbali zikiwemo Kenya, Botswana, Brazili, Jamaika, Panama, Canada na nyinginezo kwa kazi hiyo hiyo ya kuombea mvua na tumeona Mungu akitujibu kwa miujiza mikubwa, akiachilia mvua nyingi hata wakati mwingine kabla hatujaondoka kwenye viwanja vya maombi. – na tunaweza kushuhudia kuwa hadi leo hatukumbuki kuwepo kwa tishio kubwa la ukame na njaa, kwani Mungu alijibu kwa ukubwa. Kwa hiyo kwa uaminifu huo wa Mungu tunajitokeza tena kumwomba Mungu maana tunajua ni kweli anajibu maombi.Na hata sasa anaenda kutujibu.

Mungu awabariki: Asanteni kwa kunisikiliza

Askofu Dr. Charles Gadi
GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY.
IMG-20220119-WA0041.jpg
IMG-20220119-WA0038.jpg
IMG-20220119-WA0032.jpg
IMG-20220119-WA0031.jpg
 
Uafrika kazi sana na nitashangaa isiponyesha watu tutakufa njaa nawakati tumezungukwa na maji! Serikali kilimo cha umwagiliziaji kinawezekana taifa hili msisubiri mpk tuwasengenye.
 
Tunawashukuru,Mungu kasikia maombi yao pamoja na sisi ,mvua zimeanza kunyesha Sana tuu mikoa karibu yote.

Mimi mkoa niliko kuivisha ni uhakika kama itaendelea hivi hivi kunyesha.
 
Uafrika kazi sana na nitashangaa isiponyesha watu tutakufa njaa nawakati tumezungukwa na maji! Serikali kilimo cha umwagiliziaji kinawezekana taifa hili msisubiri mpk tuwasengenye.
Sio uafrika ni uwezo wa teknolojia na pesa kuwekeza kwenye kilimo.cha kisasa.
 
Sio uafrika ni uwezo wa teknolojia na pesa kuwekeza kwenye kilimo.cha kisasa.
Sio Kama haupo mbona upo unafikiri hiyo mitirioni na mibilioni inashindwa!,maji tumepewa karibia Kanda zote ardhi tumepewa yenye rutuba kwa mazao tofauti tofauti ktk Kanda hizi,hali ya hewa nzuri na yenye utulivu ipo na watenda kazi wapo!.

Ndugu kukaa na hizo fikra za hatuwezi ni ujinga,watu wanaweza kwenda angani tushindwe kilimo cha umwagiliziaji. Chakukushauli punguza kula wanga kwa wingi kula protein.
 
Back
Top Bottom