Ombi langu kwa viongozi wa dini!

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,421
4,729
Naomba kutumia jukwaa hili kuwaomba viongozi wa dini zote kuacha kabisa kulumbana kwasababu za mambo ya kisiasa.

Badala yake viongozi hawa waungane kwa pamoja na kutoa tamko la kuliombea TAIFA. Yawepo maombi ya siku kadhaa ya kuliombea taifa.

Tunakoelekea sio kuzuri, hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya kwa wananchi wa hali duni. Ukame/ukosefu wa mvua za kutosha na/au mvua zinazozidi zimesababisha mazao ya chakula kuwa bei ghali.

Kupanda kwa gharama za bidhaa ni tatizo karibu kila mahali wananchi wengi wanalalamika hali ngumu.
Tuliombee taifa letu.

Viongozi wengi wa kisiasa wapo kwa ajili ya kutimiza maslahi yao binafsi. Tumuombe Mwenyezi Mungu aliponye TAIFA LETU LA TANZANIA!
 
Back
Top Bottom