Ninachukizwa na jinsi CCM inavyoendeshwa na CHADEMA bila kujijua na kuifanya iwe juu

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Ukiacha na huu upuuzi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa kuwataka wanajeshi wafanye usafi mitaani ili kukabiliana na maandamano ya CHADEMA jambo litakalo wapa credit CHADEMA nje na ndani ya nchi kwamba inawezekanaje jeshi lipambane na waandamanaji na si polisi upuuzi kama huu haujaanza leo kwa viongozi wa CCM kufanya mambo yatayowapa CHADEMA hadhi ya kunyanyaswa na dola .

Mwaka 2007/8 wakati wa kashfa ya Richmond ambapo serikali ya CCM ilinguka bungeni kwa hoja za wabunge wa CHADEMA na kubebwa na CCM badala ya kuzima kashfa wakakomaliana na baadae CHADEMA wanaonekana walikuwa sahihi na mlolongo wa kashfa nyingine nyingi zilizo wamtetemesha utawala hadi kunusulika mwaka 2010 kuangushwa na Dkt Slaa.

Baada ya Magufuli kuwa Rais CHADEMA waliogopa sana kwani alifanyia kila walichokuwa wanapigia kelele kipindi cha Kikwete kupambana na ufisadi, uzembe, madawa ya kulevya, vyeti feki, utoroshwaji wa wanyamapori, safari za viongozi na n.k walipo ona kuwa wanakaliwa kooni na wanapotea kwa hoja wakaibuka na hoja za udikteta, mauaji,ukanda na kukosekana kwa uhuru wa habari hasa ukosoaji.

Hapa wanaccm wajinga wakawa ona kuwa wako sahihi wanawaunga mkono wakawabeba agenda ya CHADEMA na kuizungusha duniani na mitaani, umaarufu wa Magufuli ikazidi kupungua na dunia ikamuona mkosaji kama CHADEMA walivyotaka, hapa CHADEMA walifanikiwa hadi Magufuli anakufa CCM wakawa wameibeba ajenda ya CHADEMA bila kujua.

Samia alionekana ana mvuto mkuu kwa wanachadema ila hakujua kuwa walikuwa wanamchimba wanafahamu vizuri ili waje wamtapike uchaguzi ukifika ndio umefika sasa hapa kuna huu wa serikali za mitaa na ule mkuu mwakani sasa wajinga ndani ya CCM wanawabeba CHADEMA bila kujijua agenda za CHADEMA zinakuwa zao ile kauli mbiu ya nchi haitatawalika inaibuka tena huku tukisubiri hoja za ufisadi, uzembe, madawa ya kulevya vyeti feki,ajira ,mfumuko wa bei na udikteta wa Samia kuelekea mwaka 2025

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom