Viongozi wa chadema kuhojiwa singida leo-kuhusu fujo za ndago iramba.

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Tupo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa kamanda Mkoa Linus Vincent Sinzumwa, kusubiri Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo kuhojiwa kuhusu fujo zilizotokea Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba wiki iliyopita. Hata hivyo baada ya viongozi hawa kufika mapema kadiri ya muda walioambiwa na RPC huyo, Polisi wameshindwa kuanza mahojiano na viongozi hawa kwa kile kilichosemwa kuwa ni kuwasubiri Makamishna na Makachero kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi toka Dar es Salaam. Jana jioni Mtuhumiwa muhimu ambaye alitambulishwa kwa jina moja la Msamaria, Pamoja na mwingine ambaye anajulikana kama Tito, ambao wanahusiswa au kutajwa sana kuwa ndio waliosababisha fujo kubwa zilizopelekea kifo cha mtu mmoja, bado vijana hawa walionekana wakirandaranda nje hata Polisi hawajawakamata, ukiachilia mbali wale ambao kwa sasa tunaweza kusema ndio waliokodishwa toka Dar kuletwa Singida na CCM. Viongozi wa CCM bado wanahaha kuwawekea dhamana hao vijana wa Dar es Salaam, walihojiwa na kusema eti ni wafanyabiashara: Jana ilishindikana, sijui kama leo inawezekana vijana waliosababisha ndugu kuuana kwa fujo walizosababisha. Ndugu zao wapo Dar, lakini wao wakatoka kuja huku kwa ujira kwa nia ya kuua. Ndio kazi ya Katibu wa Uchumi na fedha. Pesa za CCM NDO MATUMIZI YAKE HAYA? TUENDELEE KUULIZA UHUSIANO ULIOPO KATI YA CCM NA VIJANA SABA WALOSABABISHA FUJO MKUTANO WA CHADEMA AMBAO NI:Abdala Mbwana Kingwande, (Mndengereko), ana Miaka 36, Mwislamu, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Segerea Dar es Salaam. wa Pili Ni Nasri Salehe (Mnyamwezi), ana umri 28, Mwislamu, anakaa karikaoo, na ni mfanyabiashara. Wa tatu ni Laizimu Njama, ni MMakua, ana miaka 42, Mwislamu, anatokea Tandika/Temeke Dar es salaam. wa Nne ni Mohamedi Abdalaa, Mluguru, ana miaka 34, Mwislamu, anakaa Kibamba Dar es Salaam, wa Tano ni Rudoviki Muganyizi, Mhaya, ana miaka 32, Mkristo, Ni Injinia. Wa Sita ni Justini Sangu, Mfipa, ana miaka 40, Mkristo anakaa Dar na ni mfanya biashara. wa Saba ni Salumu Ali Rashidi, ni Mmwela, ana miaka 26, Mwislamu, ni Mkaazi wa Tandika Jijijini Dar. Nitaendelea kuwajuza yanayojiri, ngoja tuwasubiri hao wa makao makuu kama wanakuja na kipya ambacho wa Singida waliokuwa kwenye eneo la tukio hawakijui.
 
Bado safari fupi sana kabla nchi haijafika vitani...
 
Hao watu wa Dar lazima watakuwa wamekuja huko na msafara wa Mnyika, ss huoni kwamba hao ni CDM?
 
CHADEMA inahtaj angalao 2wasaidie vijana waliokamatwa ambao n makamanda msaada wa kisheria kwan kesi ya mauaj sio ndogo
 
Nina shaka kuwa madai/mahojiano yanahusu kifo cha yule jamaa Ndago. Ingekuwa hivo, washitakiwa wasingepewa dhamana. Nadhani kifo cha yule bwana kitaachwa kipite kama pepo za kusi na inaishia hapo.

Kuna mwandishi hapo juu anadai wale waliotoka Dar ni wa CDM. Sijui ni kwanini wangeleta vurugu kwenye mkutano wa chama chao. Tumezoea vurugu kwenye mikutano kuwa za wafuasi kinzani.
 
Ahsante kwa taharifa....ila sijapenda ulivyotaja majina ya hao watu kwa dini na makabila yao.
Sijaona umuhimu wowote wa kutaja hivyo vitu.
 
Thanks Mkuu for Info. ni kwanini polisi singida isihonji mpaka waje kutoka Dar? hao makamishina kutoka Dar ni kina nani wanaosubiliwa? asije akawa msangi? Mnyika ingia na Tepu Recoder kabisaaaaa
 
Mbona sijaona jina la kijana anayeitwa Dullah au Dullah Mwanza kama wengi wanavyomjua.


Huyu ndiye aliyeratibu safari ya wale vijana kumi waliotoka Mgodini Sekenke/Mgongo.


Pia anatajwa kuwa na ukaribu na Mh. Mwigulu na ni mpambe wa karibu wa mchimbaji wa dhabu ( Jina: Kolesh ) anayemiliki Benz E240.

Na siku ya tukio, kijana huyu alionekana eneo la Misigiri akiulizia sehemu atakayopata tairi saizi 14 kwani gari lake lilipata pancha eneo la ndago. Hapa ilikuwa ni eneo lile la Bar ya Manka Grocery aliyowapeleka wale wafanya fujo kunywa Konyagi kabla ya kwenda kufanya fujo.
 
Wanaopaswa kuhojiwa ni kina Mwigulu na wafuasi wa thithiemu!!!!

Tunataka kumbananisha OCS na askari wake wanaotajwa kuona vurugu zikianzishwa na kikundi hicho cha kukodi lkn wasichukue hatua,so muhimu kina mnyika na watoe maelezo/ushuhuda wao namna ilivokuwa.Nina habari Mwema kashachoka kupakaziwa anataka kufanya real
 
Thanks Mkuu for Info. ni kwanini polisi singida isihonji mpaka waje kutoka Dar? hao makamishina kutoka Dar ni kina nani wanaosubiliwa? asije akawa msangi? Mnyika ingia na Tepu Recoder kabisaaaaa

Polisi Singida tayari ni watuhumiwa katika kadhia hii,wanatajwa kupokea maelekezo/mlungula toka kwa Mwigulu wafumbie macho vuruge zitokee image ya cdm iharibike,,bahati mbaya hata Mwigulu hakutegemea itapelekea hadi kifo so acha wahojiwe na watu tofauti japo basically ndo wale wale but at least makes sense. Nimependa hapo kwenye Mnyika kuingia na recorder
 
Hata mimi sijapenda lakini nadhani ametoa kwenye taarifa ya polisi ambao huandika jina ,kabila, dini ,urefu n.k.
Ahsante kwa taharifa....ila sijapenda ulivyotaja majina ya hao watu kwa dini na makabila yao.
Sijaona umuhimu wowote wa kutaja hivyo vitu.
 
Polisi Singida tayari ni watuhumiwa katika kadhia hii,wanatajwa kupokea maelekezo/mlungula toka kwa Mwigulu wafumbie macho vuruge zitokee image ya cdm iharibike,,bahati mbaya hata Mwigulu hakutegemea itapelekea hadi kifo so acha wahojiwe na watu tofauti japo basically ndo wale wale but at least makes sense. Nimependa hapo kwenye Mnyika kuingia na recorder

Nimekusoma mkuu, kama hivyo ni vema , isije kuwa wamepewa maelekezo toka IKULU
 
Tupo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa kamanda Mkoa Linus Vincent Sinzumwa, kusubiri Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo kuhojiwa kuhusu fujo zilizotokea Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba wiki iliyopita.

Itabidi hao kwenye red waunganishwe na watuhumiwa wenzao
 
Back
Top Bottom