Viongozi wa chadema kuhojiwa singida leo-kuhusu fujo za ndago iramba.

Mkuu Kitila Mkumbo,
Tunakuona upo online kwenye thread. Tunaomba utupe update kinachojiri huko.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - Hull City, UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Tunataka kumbananisha OCS na askari wake wanaotajwa kuona vurugu zikianzishwa na kikundi hicho cha kukodi lkn wasichukue hatua,so muhimu kina mnyika na watoe maelezo/ushuhuda wao namna ilivokuwa.Nina habari Mwema kashachoka kupakaziwa anataka kufanya real

yea,lazima watoe ushuhuda wa kina jinsi walivowakodi hao vijana kutoka ubungo kwenda kufanya unyama kwa wananchi wasio na hatia
 
Policeccm na filamu za kova..... Hao ccm walifuta nini mkutano wa chadema, ajabu wanabebana na viongozi wao?
 
kwa utamaduni tuliouzoea watanzania wa kuishi kwa amani na upendo na sasa tunaona wanasiasa wanaanza kutuingiza kwenye umwagaji damu kwa kutaka kufanikisha ajenda zao za kisiasa lazima watanzania tuwe makini kweli kweli na hawa wanasiasa NJAA.


Hapa lengo la mwanasiasa ni kuyataka madaraka kwa njia yoyote ile hata kutoa roho za wattu kama hivi.hili ni janga lingine la kitaifa.tuikemee tabia hii.tuwakemee wanasiasa wa aina hii kwa nguvu zetu zote
 
Policeccm na filamu za kova..... Hao ccm walifuta nini mkutano wa chadema, ajabu wanabebana na viongozi wao?

akikamatwa mtu wa ccm hapo polisi iko sahihi na imefanya kazi yake lakini akikamatwa muuaji wa chadema kuhusu kuua huko iramba polisi inakuwa ya ccm.
 
Hawana lolote hao police!
Chakujiuliza walikuwa wapi mpaka fuja zinatokea?
 
Ahsante kwa taharifa....ila sijapenda ulivyotaja majina ya hao watu kwa dini na makabila yao.
Sijaona umuhimu wowote wa kutaja hivyo vitu.

mshikachuma, nadhani isango amenukuu kutoka ktk taarifa za polisi (RB) maana ndo huwa wanavyolipoti taarifa zao hivyo. hata mimi jana nilienda kutoa tarifa polisi wakaanza kuniuliza kabila na dini yangu na maelezo mengine binafsi. sikuona kuwa ni issue sana. kwa hiyo we ipotezee tu.
 
Hao watu wa Dar lazima watakuwa wamekuja huko na msafara wa Mnyika, ss huoni kwamba hao ni CDM?

Huu ushirika wa CDM na CCM umeanza lini??? Yani vijana wa CDM wakamatwe halafu wana CCM wahangaike kuwawekea dhamana ambayo ni ngumu kupatikana. La kujiuliza, kwanini wale viongozi wa CDM wa Singida waliweza kupatiwa dhamana na wanachi wa Singida, kwanini hawa iwe ngumu mpaka wana CCM wahanahangaika hivi????
 
Tupo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa kamanda Mkoa Linus Vincent Sinzumwa, kusubiri Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo kuhojiwa kuhusu fujo zilizotokea Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba wiki iliyopita.

Itabidi hao kwenye red waunganishwe na watuhumiwa wenzao


Usipate shida anzeni kumkamata OCD.....La sivyo mtaumbuka


Hii nimeipata humu…. NOLNIZ



Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese.

Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa
wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.


Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi.


Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.




Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda. Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.

Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo. Pamoja na yote haya, Mwigulu watu wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili".
 
Tumefika Hapa Tulipo Kwa Sababu Ya Udhaifu Wa Rais Kikwete, Kwa Uzembe Wa Bunge, Na Kwa Sababu Ya Upuuzi Wa CCM-Mnyika John Mnyika.

Kwa hili hata mimi sifuti kauli hii kwani ina ukweli usiopingika.
 
Duhh, watu wana roho ngumu, hamumuonei huruma.

Tumefika Hapa Tulipo Kwa Sababu Ya Udhaifu Wa Rais Kikwete, Kwa Uzembe Wa Bunge, Na Kwa Sababu Ya Upuuzi Wa CCM-Mnyika John Mnyika.

Kwa hili hata mimi sifuti kauli hii kwani ina ukweli usiopingika.
 
[h=2]Nukuu ya maandishi ya jumbe za simu za kutishwa kuuawa alizotumiwa Mwigulu Nchemba [/h] 18/07/2012
0 Comments


Baadhi ya wabunge wa CHADEMA, wamehusishwa na mauaji ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Kata ya Ndago wilayani Iramba mkoani Singida, Yohana Mpinga (30).

Akizungumza bungeni jana, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alisema kabla ya mauaji hayo anayoona yalipangwa, alitishiwa kuuawa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa simu na wabunge hao kutokana na mijadala yake bungeni.

Nchemba alitoa madai hayo alipoomba Mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya Bunge ya 47 inayohusu kusitishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura la Taifa.

Sehemu ya ujumbe huo ambao Spika wa Bunge, Anne Makinda alimzuia kuusoma, unamtaka Mwigulu asijifanye anajua, kwani mwenzake Chacha Wangwe (Marehemu Mbunge wa Tarime) alijifanya anajua na “sasa yuko wapi?” Ujumbe mwingine ulimwambia kuwa skafu ya Bendera ya Taifa anayovaa shingoni, itageuka sanda yake.

Akiomba Mwongozo huo, Nchemba alisema kutokana na tukio la kinyama lililotokea jimboni mwake juzi la kuuawa kwa Mpinga na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, aliomba Bunge liahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kwa kina.

“Naomba tuahirishe Bunge tujadili suala hili, kwa kuwa inaonesha kilichotokea kilipangwa, nilipokea SMS (ujumbe mfupi) katika simu yangu za kunitishia kuuawa kutokana na mijadala ninayochangia bungeni na namba za walionitumia SMS zimebainika kuwa ni za wabunge wa CHADEMA,” alisema Mwigulu.

Alisema namba za simu zilizokuwa zikitumika kumtumia ujumbe huo mfupi alizipeleka Polisi na tayari wabunge hao waliomtishia maisha wamebainika majina yao na hatua zaidi zitachukuliwa.

Pamoja na kukataa kutaja majina ya wabunge hao, Nchemba nje ya Bunge alionesha ujumbe mfupi aliotumiwa ambao unasema:


  1. “Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatusonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya CCM milele? “Utajutia kimbele mbele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini, hata kama ni kweli, kwa nini kututia aibu?”
  2. “Hata ufanyeje, 2015 tunaingia Ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?”
  3. “Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake, lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja”.
  4. “Fahari yako leo, itageuka kilio kwako. Utatutambua.”

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimkatisha Nchemba asiwataje kwa majina wabunge hao waliomtumia ujumbe mfupi wa kutishia kumwua na kumtaka aiachie Polisi ishughulike na jambo hilo, ambapo pia aliukataa Mwongozo wa kuahirisha kikao.
 
Back
Top Bottom