Viongozi wa Afrika hawana budi kujali maslahi ya watu wao kuliko yao binafsi, mabeberu wa nchi za Magharibi na wengineo

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,861
20,714
Watanzania wengi ni maskini,hakuna shaka yeyote kuhusu jambo hilo.Kwa nini Watanzania ni maskini ndilo jambo ambalo limeonekana kusumbua watu wengi. Kikwete yeye alisema hajui kwa nini Watanzania ni maskini. Sasa inashangaza kwa kuwa kama ni hivyoo, kwanini alitamani kuwa Rais kwa vile jukumu moja kubwa la Rais ni kuwaletea wananchi wake maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwaondelea umaskini!! Sasa usipojua kwa nini ni watu wako Ni maskini,utawaondoleaje umaskini?

Hata hivyo kwa mtu au kiongozi mwenye nia njema na Watanzania, sababu kwa nini Watanzania ni maskini ipo wazi:Watanzania ni maskini kwa sababu ya matumizi mabaya ya rasilimali zao na ubinafsi wa viongozi.

Tanzania ni nchi tajiri.Hayati Magufuli alisema jambo hili wazi na bila kumung'unya maneno,na katika uongozi wake uliodumu kwa takriban muhula mmoja,tuliona ukweli huu.Miradi mingi ilianzishwa na kwa mara ya kwanza Watanzania wakajivunia kuwa Watanzania. Waliokuwa wanatamani kuwaibia Watanzania rasilimali zao hata hivyo, hawakupenda Watanzania kujua ukweli huu,kwa hiyo wakapanga njama za kumdhulumu Magufuli uhai wake. Hatimaye walifanikiwa na ndoto ya Watanzania ya kuwa na Tanzania yenye maisha bora ikapotea.

Katikà awamu ya kwanza tuliambiwa Tanzania ni maskini,jambo ambalo si kweli.Sina hakika kama Mwalimu alikuwa na nia mbaya ya kuwaficha Watanzania kwamba nchi yao ni tajiri,hata hivyo wimbo uliokuwa Tanzania ni maskini.

Katika awamu ya pili tuliambiwa "ruksa" kufanya lolote, ili mtu aweze kujikimu.Subliminally nadhani tulikuwa tunaambiwa serikali haiwezi kutuhudumia,nchi ni maskini,kwa hiyo kila mtu atafute pori lake. Matokeo ya sera hii isiyo rasmi kwa wale tuliokuwepo yalikuwa mabaya sana. Kila mtu alifanya alilo-ona linafaa,pesa ikahama serikalini na kuingia kwenye mikono ya watu,na literally serikali ikafilisika kabisa na ikashindwa kutimiza kabisa majukumu yake ya msingi kwa wananchi.

Katika awamu ya tatu,tuliambiwa "kasungura" ni kadogo,lakini nia ikiwa ile ile:kuwaficha Watanzania walio wengi ukweli kwamba nchi yao ni tajiri,ili wachache waendelee kufaidi rasilimali za taifa wakishirikiana na wadhalimu wa nchi za magharibi na wengine.

Katikà awamu ya nne wimbo ukawa ule ule,nchi ni maskini,lakini hakuna shaka yeyote kwamba nia ilikuwa ile ile ovu,kuwaibia Watanzania rasilimali zao.

Katika awamu ya sita,nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kufuta yale yote ambayo awamu ya tano iliingiza kwenye vichwa vya Watanzania,kwamba nchi yao ni tajiri, na hivyo kutembea kwa kujiamini na kuwa na matumaini. Ni wazi nia ni ile ile, kufuta mawazo kwamba nchi ni yetu ni tajiri, na hivyo kuendeleza kushirikiana na mabepari wa nchi za magharibi na wengine kuendeleza kuwapora Watanzania rasilimali zao.Ufuatao ni ukweli mchungu wa hali ilivyo kwa Africa na viongozi wengi wa Africa.


View: https://youtu.be/-BZgM70nhg0?si=_ghvjIuQYJMwtmMI


View: https://youtu.be/fkjyy2IJGts?si=C8nw1Wl3z973sQBd

Wote ni mashahidi jinsi ufisadi ulivyorejea kwa kasi kwenye serikali ya awamu ya sita,mpaka kusababisha mikataba mibovu kama DP World kubuniwa.Katika hali ya kushangaza, hata baada ya CAG kufunua uozo katika matumizi mabaya ya rasilimali za uma, zikiwemo fedha,hakuna mtendaji yeyote ambaye mpaka sasa amechukuliwa hatua,ikidhihirisha wazi kwamba ufisadi ni mfumo wa serikali yetu.

Kuthibitisha hili katika siku za hivi karibuni,kumekuwa na taarifa inayozunguuka mitandaoni kwamba Rais wetu ni mmoja wa Marais kumi tajiri kabisa Africa, yeye akiwa wa saba (chini mwisho). Haijalishi kama hii taarifa ni kweli au siyo kweli, ila tayari wasiwasi umeshaingia kuhusu kiongozi wetu.Mtu unajiuliza,utajiri wote huu katika muda mfupi huu? Hii ni kweli?Tena wakati Watanzania ni maskini wa kutupwa?Haingii akilini.

Mwisho,lini viongozi wa Africa na wa Tanzania watajali maslahi ya wananchi wanao-waongoza na kuacha kushirikiana na wadhalimu na mabeberu wa nchi za magharibi na wengine kuiba rasilimali za Africa na kuwafukarisha watu wao, lini? Inasikitisha kwamba na rasilimali zote tulizonazo,baada ya miaka sitini na tatu(63) ya Uhuru wetu, tunatembeza bakuli na hatuna chochote cha maana cha kujivunia kimaendeleo, wakati wale wanaotuibia rasilimali zetu wanafanya maendeleo nchini mwao ya kutisha. Kwa rasilimali tulizo nazo tulipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo. Naomba nisisitize tena kwamba ushahidi unaotolewa na viongozi wetu kwamba tumepiga hatua kimaendelea si lolote ukilinganisha na rasilimali tulizo nazo na pia ukizingatia kwamba tumekuwa huru sasa kwa miaka sitini na tatu.

Mwalimu Nyerere alituachia usia(chini mwisho), alisema,"tuipende nchi yetu kama mama yetu."Ndio viongozi wetu hawaipendi nchi yao kama mama yao, ndio maana wanashirikiana na wageni kuihujumu.
 

Attachments

  • IMG-20230828-WA0001.jpg
    IMG-20230828-WA0001.jpg
    55.1 KB · Views: 1
  • IMG-20230828-WA0002.jpg
    IMG-20230828-WA0002.jpg
    62.5 KB · Views: 1
  • VID-20230828-WA0000.mp4
    6.5 MB
Back
Top Bottom