Viongozi UKAWA wakutana faragha

Viongozi UKAWA wakutana faragha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
IMG-20160909-WA0066.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (katikati) akiongoza kikao cha viongozi wa UKAWA kinachofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Dar es Salaam. Viongozi wa UKAWA wamekutana jijini Dar es Salaam kwa kikao cha faragha kinachoendelea muda huu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kinachomshirikisha kada wa zamani wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, kimewakutanisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Mwesiga Baregu.
 
Ngojea tusubirie updates kamili maana mtoa taarifa hana ata nyepesi nyepesi kuhusu kikao kamili
 
Wamekutana faragha...means hawataki kuwa exposed sasa wewe umewatibulia..😀😀😀
 
Naomba Mwenyezi Mungu awape busara maradufu ili yale wanayojadili na kuamua yawe ni kwa manufaa ya Nchi yetu inayovurugwa na wababe wasio upeo wa uongozi.
 
View attachment 397072
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (katikati) akiongoza kikao cha viongozi wa UKAWA kinachofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Dar es Salaam. Viongozi wa UKAWA wamekutana jijini Dar es Salaam kwa kikao cha faragha kinachoendelea muda huu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kinachomshirikisha kada wa zamani wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, kimewakutanisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Mwesiga Baregu.
Kwa vile mikutano yote ya kisiasa hata mikutano ya ndani, imepigwa marufuku!, hivyo, kikao hicho sii halali na ni kinyume cha amri halali, naomba nijulishe na kunieleza kikao hiki kimefanyikia wapi ili niwaripoti washiriki wa kikao hicho kunako husika ili wahifadhiwe mahali salama! .
Pasco
 
Wote wakutanao wametoka CCm kasoro Freeman Mbowe! Chadema asili wako wapi?
Kingunge,Lowassa, Seif na Baregu
Viongozi wote wakubwa wa upinzani walikuwa ccm, walihama na kuanzisha vyama vipyaa
Kabla ya 1992, sote chama chetu kilikuwa ccm
 
Back
Top Bottom