SoC03 Viongozi kutowajibika huvuruga amani

Stories of Change - 2023 Competition

File Suleiman

Member
Jun 5, 2023
9
7
Msingi mkubwa wa kila taifa ni ulinzi na usalama, kuweza kulinda nchi na mipaka yake ili kuhaikisha usalama unakuepo na nchi inapata amani na kuhakikisha shughuhuri zengine zinaendelea mana bila amani hakuna cha mana ivyo basi mataifa mengi duniani hutumia bajeti kubwa katika ulinzi na usalama wa nchi ili tuu amani na utulivu uwepo katika nchi husika mara nyingi nchi hujilinda na kuvamiwa na nchi zengine au vikundi vya kiuhalifu au madui wapya kama mazingira, afya, chakula na kadharika ila katika miaka ya ivi karibuni tumeshuhudia duniani kote migogoro na uvunjifu wa amani hautoki tena nje ya nchi bali unatoka ndani ya nchi na mara zote husababishwa na vioongozi kutowajibika ambapo matokeo yake huzaa vita na uvurugwaji mkubwa amani.

Viongozi wengi wanajisahau sana katika majukumu yao ambapo hufanya matarajio ya wanachi kudidimia, kutoweka na kukosa imani na uongozi na viongozi waliopo madarakani na hii husababisha chuki ndani ya wananchi ambapo wanakua hawana tena imani na viongozi wao na uongozi mzima, na hii ni kutokana na viongozi kuwepo katika wimbi la ubadhilifu wa mali za uma, kuwepo katika wimbi la rushwa pia kuminya na kukandamiza haki, hali hii ni mbaya sana na matokeo yake ni kujaza chuki kwa wananchi mwisho wa siku inakua ni hatari katika usalama wa nchi na hapo ndio tunaona michafuko mbalimbali ulimwenguni utokana na hali hii ya uwajibikaji hafifu wa viongozi hutia chuki na hufifisha imani ya wanachi juu ya serikali na viongozi wao.

Ripoti mfufulizo za Mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali sio za kuziacha zipite ivi ivi zinabidi zifuatiliwe ili kujenga afya ya wanachi na serikali yao, uwajibikaji kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu husaidia kulifanya taifa letu liendelee kua na amani, tukumbuke zama zimebadilika sana. Tukio la migomo ya mara kwa mara inayoendelea hapa nchini haiji kwa bahati mbaya labda kuna pahali hakuna uwajibikaji na hii ni hatalishi kwa usalama wa nchi yetu, nani alifikiria ipo siku wafanyabiashara wa Kariakoo watafunga maduka kwa siku tatu mfululizo??, kumgomea mkuu wa mkoa!, kulazimisha mkutano ufanyike sehemu ya wazi na sio tena kwa watu wachache?!, nani aliweza waza haya??.

Wanasema hakuna moshi bila ya moto, yanayoendelea nchi zengine yalianza kama yanavyoanza hapa Tanzania itafika muda uvumilivu utawashinda watanzania na wao wataingia mabarabarani kwa fujo ivyo basi wanaopata nafasi ya kutumikia wananchi kwa njia yoyote ile kuanzia walimu, wauguzi, wahandisi, polisi, wahasibu, wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wenyekiti wa mitaa na vijiji, wahudumu wa ndege na mabasi kila nyanya inayomgusa mwananchi na yahitaji uwajibikaji basi watumishi wa uma wawajibike ipasavyo mana makosa yao yanaweza yakasababisha moja kwa moja uvunjifu wa amani wa nchi yetu na moja kwa moja wananchi lawama zao zikaenda kwa rais na viongozi wa ngazi za juu katika uwajibikaji na utowaji uamuzi akianzia Rais, makamu wake na waziri mkuu wawe macho katika uwajibikaji ipasavyo makosa ya wengine wajue ni yao na pia wakichelewa katika kuwajibika wajue matokeo yake ni makubwa mnoo na sana.

Mwaka 2019 Sudan wananchi waliandamana kisa kupanda kwa bei ya makate na ikaibua mambo mbalimabli na kuchochea hisia za wanachi na kumng'oa Omar Al-Bashir, leo hii Tanzania bidhaa ngapi zimepanda bei na serkali inachukua wajibu gani?

Mwaka 2010 hadi 2011 nchini Tunisia wananchi walianza maandamano hadi kumtoa madarakani rais Zine EL Abidine Ben Ali kutokana na kijana Mohamed Bouazizi kujichoma moto mbele ya ikulu ya Tunisia baada ya wagambo wa jiji kumchukulia na kumwagia bidhaa zake azokua anauza pembezoni mwa barabara kama ingekua hapa nyumbani ni mmachinga na hili jambo likagusa hisia za watunisia wengi wakaingia barabarani na kuanza mgomo na maandamano ya kushinikiza raisi ajiuzulu na kweli 2011 akajiuzulu ila nchi ilichafuka vya kutosha je leo hii hapa Tanzania upangaji wa wamachinga unauwajibikaji ndani yake au unaonevu?? Tumemwaga bidhaa ngapi za wamachinga, tumewatia hasara mara ngapi?? na hii matokeo yake tunayajua??

Mwaka 2012 huko Syria maandamano yalianza kwa kitu kidogo sana baada ya wanafunzi kuchora ukuta ukionyesha kutaka raisi Bashar al Assad ajiuzuru, wale vijana wakakamtwa na vyombo vya usalama , wazazi wa wale vijana wakaanza mgomo katika shule za vijana wao na kidogo kidogo mandamano yakanza yakitaka wale vijana waachiwe na badae mandamano yakanza ita na machafuko yakaanza na ambayo yamejitokeza kwa zaidi ya miaka 10 japo kulikua na sababu nyengine ila kuna wimbi kubwa la watu waliingia barabarani kwa sababu tuu ya vijana kukamatwa. Haimanishi turuhusu raia waongee hovyo tuu kuhusu serikali na viongozi wake hapana bali tunawajibika vipi baada ya matukio kama hayo ili yasilete matokeo mabaya na makubwa zaidi?

download (2).jpg


(Picha ikionyesha wandamanaji nchini Tunusia wakiwa wameambatana na picha kubwa ya mmachinga Mohamed Baouaziz, aliejichoma moto mbele ya ikulu ya Tunisia na kusababisha mandamano ya nchi nzima 201 hadi 2011)

download (3).jpg

( picha ni bendera ya Sudan na Mkate ukionyesha jinsi bei ya matae ilivyoleta taharuki nchini umo katika mwaka wa 2019 ulisababisha Omar Al Bahir kupinduliwa madarakani)

Katika kila jambo likienda ovyo katika nchi basi mara zote kuna wahafidhina watachukua nafasi katika jambo hilo kuweka imani na aidia zao ili wafanikishe majambo yao na hii tumeona kwa aliekua rasi wa Libya Muamar Gadaffi ambapo wapo walikua na nia ovyo na Libya wanatumika kuweza kumuangusha Muamar na njia walioitumia kwa wananchi wa Libya ni kuwahadaa kuhusu demokrasia ambapo japo walipata kila kitu ila uhuru wa mambo mengine ikawa ni kosa dogo sana alilofanya Muamar na wahafidhina wakalitumia kosa hilo, mana yangu ni nini?

Serikali iwe makini katika kila eneo ambalo linaweza likawa sababu ya michafuko na taharuki haijalishi serikali itafanyia mangapi meme na wanachi wake ila jua tuu panapo na kasoro ndipo patazungumzika kuhusu mema yote serikali itafanya na pia serikali itamube kuna wengi wanaiombea mabaya kama wengi wanavyoiombea mema ivyo serikali ikiruhusu kuteleza mara kwa mara inwapa nafasi wabaya kutumia nafasi io katika kuwajenga wabaya wa nchi ivyo basi katika swala la uwajibikaji serikali iwe macho muda wote na pasiwe na kasoro hata kidogo ili Tanzania iendelee kua hai na salama muda wote yenye amani.

Hatuna Tanzania zaidi ya hii aliotuachia Nyerere na Karume, Tanzania kwetu ni Baba na Mama, Tanzania kwetu ni Kaka na dada, Tanzania kwetu ni mke na mume, Tanzania kwetu ni rafiki na jamaa, hatuna nchi zaidi ya hii Tanzania, Mungu ibariki Tanzania, wabariki Watanzania, Wabariki na viongozi wake.
 
Back
Top Bottom