SoC03 Utawala bora na uwajibikaji ndio nguzo ya msingi katika kuleta amani na maendeleo ya taifa

Stories of Change - 2023 Competition

AfrixOne

New Member
Jul 19, 2021
1
0
Utawala Bora ni dhana inayohusu utawala mzuri na wa haki, ukiwezesha ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya serikali yao na kuimarisha mifumo ya kisheria na utawala. Inalenga kuendeleza utawala ulio wazi, uwajibikaji, na ufanisi katika kutoa huduma na maendeleo kwa jamii.

Uwajibikaji ni jukumu la kuhusika na kutekeleza majukumu yako kwa uaminifu na kwa ufanisi. Katika muktadha wa utawala, uwajibikaji unahusu watawala kuwajibika kwa wananchi na kuheshimu matakwa ya umma. Hii inaweza kujumuisha uwazi katika utendaji kazi, kutoa taarifa za kifedha na matumizi ya serikali, kusikiliza maoni ya wananchi, na kuchukua hatua za kurekebisha makosa na kujibu changamoto za kijamii na kiuchumi. Uwajibikaji ni msingi muhimu wa utawala bora na utawala wa haki.

Ni dhahiri kuwa kama taifa tunazo nyenzo kubwa na mahususi kwa ajili ta kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma, Serikali, Vyama vya Kisiasa na hata Asasi za Kiraia kama mashirika na makampuni. Nyenzo hizi ni kama vile Sheria, Katiba, Miongozo na Kanuni. Lakini swalinni JE! NYEZO HIZI ZINAFUATWA?

Dhana ya Utawala Bora na Uwajibikaji inagusa sekta zote katika Taifa bila kuacha hata moja.

Namna Viongozi wanavyopaswa kuwajibika kwa jamii
• Kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuleta njia za maendeleo
• Kuandaa Mipango chanya ya maendeleo kwa taifa kwa ajili ya leo na kesho.
• Kusimamia haki, usawa na kanuni zilizotungwa na bunge.
• Kuwajibika pale wanapofanya makosa, kama kujiuzuru, kushitakiwa au kusimamishwa kazi.
• Kuwa daraja la kuisaidia jamii kwa usawa na haki.

Namna jamii inavyowajibika katika taifa
• Kutekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi wa nchi na taasisi mbalimbali.
• Kutoa mchango wa maoni, mawazo na mapendekezo katika sekta mbalimbali za taifa kwa ajili ya maendeleo.
• Kusimamia na kuheshimu sheria zilizotungwa na kupitishwa na bunge ili kuendelea kudumisha amani kwa ajili ya maendeleo.
• Kushiriki kikamilifu kuandaa kizazi cha kesho katika malezi mema, kuandaa watumishi wazuri, wanajamii wema na wadau wakubwa wazalendo wa taifa lao.
• Kuendelea kuchangia Pato la ukuaji wa Nchi.

Uwajibikaji wa mifumo, Idara na Taasisi mbalimbali katika taifa.
• Kusimamia haki katila taifa letu.
• Kuwaunganisha wananchi kwa haki
• Kutelekeza majukumu yake kwa usawa

Baadhi ya sababu zinazopunguza Uwajibikaji na Utawala Bora?
1. Kukosa uzalendo kwa Taifa na Jamii ya leo na kizazi kijacho, Uzalendo ndio kiini kikubwa cha utawala bora na uwajibikaji kwa jamii yoyote ile, kunapokuwa hakuna uzalendo, basi hakuna tena utawala bora.
2. Ukosefu wa elimu ya maadili kwa viongozi na hata jamii katika utekelezaji wa majukumu.
3. Kupungua kwa hofu ya MUNGU kwa watumishi na jamii pia.
4. Tamaa na Ubinafsi, kutokutosheka na anachopata mtu.
5. Kisasi, hii inaweza kutokana maisha ya nyuma aliyopitia mtu, na yakamfanya kuishi kwa kufanya visasi anapohudumia jamii.
6. Kukosekana kwa mifumo mizuri ya utendaji kazi na vitendea kazi. Huwenda ikawa sababu ya uzembe katika kutimiza majukumu ya watumishi.

Nini kifanyike ili kuchochea/kuongeza kasi ya Uwajibikaji na Utawala Bora katika Jamii na Utumishi wa Umma?
Maeneo ya msingi katika uboreshaji wa utawala bora na uwajibikaji nchini;

1. Kuimarishwa kwa Taasisi na Mifumo ya Usimamizi wa Utekelezaji haki na usawa katika jamii dhidi ya utawala Bora na Uwajibikaji.
Kwa mfano Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni taasisi nyeti inayosaidia sana kuhakikisha haki inatendeka kwa watumishi wa umma na wana jamii katika maeneo mbalimbali, uwepo wa rushwa unazaa kukosekana haki na usawa na hii inaashiria ukosefu wa utawala bora.

TAKUKURU iongeze ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuendelea kubaini hawa adui wa uwajibikaji katika taifa na kuhakikisha wanafikishwa mahakamani. Sanjari na hilo, TAKUKURU iendelee kueneza kasi ya elimi kwa jamii ili kuwafungua macho juu ya namna haki inavyoweza kukandamiza haki zao.

2. Kuimarishwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na majeshi ya ulinzi.
Kwa kuwa na watumishi watiifu katika idara hii ya usalama wa taifa na kupitia mboresho ya Sheria ya mwaka 2023 ya usalama wa taifa itasaidia sana kuongeza nguvu ya idara hii nyenye kusimamia usalama wa nchi yetu. Idara ya usalama wa Taifa ni jicho la Siri linaloona yote yanayofanyika nyumanya pazia, tunaweza kuona kwa macho hakuna shida lakini kumbe ndani kuna matendo maovu yanatendeka.

3. Kuongeza Nguvu na Uzito wa Viapo vya utumishi katika serikali na ofisi za umma na adhabu kali kwa yoyote atakaekuwa kinyume na kiapo hicho.
Hii itasaidia sana kuongeza nguvu ya uwajibikaji kwa watumishi wa Umma.

4. Kuundwa kwa chombo mahususi kitakachodhibiti, kusimamia na kukagua matumizi ya nguvu katika nyazifa za uongozi, uadilifu na viwango vya uwajibikaji kwa jamii kupitia utumishi wao.
Chombo hiki kitasaidia kutoa picha halisi ya viongozi na utumishi wao kwa umma jambo ambalo litasaidia viongozi kuwa na uwajibikaji wa kila siku kwa wanajamii.

5. Kuboresha mifumo ya uwasilishaji wa hoja kutoka kwa jamii kwenda kwa viongozi na serikali. Hii ya kutegemea Mbunge kwa jimbo haitoshelezi katika utumishi wa leo, kuwepo na mfumo mbadala wa ukusanyaji maoni ya wananchi kila mwezi ili kuwapa nafasi wao kuchangia maendeleo ya taifa lao.

6. Kuboresha sera za elimu, mitaala ya shule na elimu ya chuo kwa kuweka masomo ya uwajibikaji na utawala Bora kama masomo ya lazima ili kusaidia jamii kupata elimu ya msingi ya mambo haya muhimu katika ujenzi wa Taifa.

7. Kurudisha sera ya uzalendo kwa kila mtu kuanzia ngazi ya vijana wadogo mpaka watu wazima, ili kuwapa watu moyo wa kulipenda taifa lao na kuepuka matendo yasio na tija kwa jamiii.

8. Kuimarishwa kwa mifumo inayosimamia haki, Mahakama ni ngao ya kutenda haki kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Mahakama zinapokuwa huru zaidi kufanya kazi, bila kuingiliwa na chombo chochote inasaidia kuweka hali katika usawa na kuongeza uwajibishwaji kwa wanaokwenda kunyume na taratibu za nchi yetu.

9. Kutoa Semina za mara Kwa mara za viongozi, watumishi na jamiii dhidi ya utawala bora na faida zake, ili kuwafanya watu kutii sheria bila shuruti.


• Maendeleo thabiti kwa Taifa
• Taifa kuwa na amani na Usalama
• Imani ya Jamii kwa viongozi na Taifa, inaongezeka sana.
 
Back
Top Bottom