Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Wanajifunza uongozi, muda uliobakia unatosha kabisa kabla ya uchaguzi 2015. Isipokuwa huyo Heche kwa kweli alikurupuka nadhani alikuwa na kinyongo na Shibuda akasahau kufikiri kwanza kabla ya kutoa tamko. Kwa hiyo ajifunze kwamba uongozi hauendi kwa chuki na kuviziana kwenye kona
Imekuwaje viongozi Chadema waige sera za vijana CCM kila mmoja kuitisha vyombo vya habari na kutoka tamko wakati wote wako ofisi moja? Nani anayewapa pesa hizo za kukodi kumbi za hoteli kutolea matamko kama si mafisadi wa CCM? Wasira ameshatamka akijua nini alichokifanya na matokeo ndiyo haya. Tuweni macho sana na hawa vijana.

Katika hali ya kawaida Makamu Mwenyekiti alitakiwa kuwasiliana na Mwenyekiti wake kabla ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari! Hata kama Mwenyekiti alikosea lakini kitendo cha Makamu Mwenyekiti kumkosoa hadharani ni utovu wa nidhamu.
Namshauri Makamu Mwenyekiti asifanye KUKURUPUKA kama Bibi Kiroboto alipokuwa Naibu Spika!
Kuharisha uharishe wewe halafu alaumiwe CCM!
Komaa kidogo mkuu.
Matamko ya mmoja mmoja hata kama anakinga ya kikatiba yahakubaliki kwa ajili ya kulinda mshikamano na umoja katika utawala wa kisheria. Ni dalili ya kuwepo ufa katika mfumo wa uongozi na nihatari kutohimili vishindo vya tetemeko la ardhi litokeapo nyumba yenye ufa.
Narudia kauli ambayo nilishawahi kumwambia Katibu Mkuu Dr. Slaa ambaye kwa sasa amefanikiwa kurekebisha kutoka safu ya juu Chadema, lakini tatizo ni kwa Ngazi ya juu Umoja wa Vijana Chadema.
Lazima kuondokana na mripuko wa kujibu kwenye vyombo vya habari ghafla bila upembuzi wa kutosha, bila kutuliza kwanza nerves, bila kikao cha kushauriana nini cha kujibu na papo kuangalia upande wa pili wa sarafu athari zake kwa tamko litakalotolewa.
Busara inavyoonekana katika uongozi wa juu kwenye Uongozi wa Chadema naheshimu na ndicho kinachotakiwa, ila ipo kazi kuwaweka sawa viongozi wa BAVICHA.
Mkuu hapo nilikuwa na maana ya kuhimiza wapenzi wa CDM kukua na kujiangalia kwa undani makosa wanayofanya kioganaizesheni.Hujasoma kujua kuwa nukuru ndiyo njia bora ya kutoa majumuisho ya hitimisho katika uchambuzi, uamuzi? Hivi we umeshawahi kufanya utafiti? Hata hukumu mahakamani hunukuru yaliyopita hata yaliyotolewa na mahakama nyingine katika nchi nyingine.
Nakubaliana nawe, kiongozi unatakiwa kuwa na subira katika kutoa tamko, vinginevyo kauli inaweza kusababisha mkanganyiko na wabaya kupata nafasi ya kusema yao kama Wasira alivyosema jana.
Absolutely Candid scope,
actually kuna mahali nimesema hivi..
I Expected BAVICHA cadres and organs to organize more activities with more appeal to young citizens, and strengthen the youth council's construction to increase the council's influence among Tanzanian's youth.Petty squables are not healthy.
Tarehe 28/5/2012(jumatatu ijayo) Baraza la vijana Chadema Taifa linamaliza mwaka mmoja tangu lichaguliwe.
Nategemea wiki hiii itakuwa ni wiki maalumu kwao katika kujitathmini kwamba ndani ya Mwaka mmoja BAVICHA imefanya nini.
Nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutoa tahadhari.JF haikuwa Hewani lakini waliokuwa wanachama wa JF facebook tulijadili.Nilisema Shibuda hastahili kujibiwa.Anastahili kuachwa tu bila kujibizana nae kwenye media kwani huo ndiyo mchezo anaoutaka.Anataka kupandishwa chati kisiasa(najua kamanda shibuda ni member wa hapa JF unachungulia humu).Ulichungulia humu hata nilipokuwa nakutolea mfano kuhusu mtizamo wangu na cross-carpeting za wanasiasa kutoka chhama kimoja kwenda kingine.Nilisema bila darasa la Itikadi hapa itakuwa kazi kweli kweli.Itabidi kuwe na timua timua za ovyo kwenye vyama vya siasa.
Akiwa CCM alitangaza kugombea Urais kupambana na Jk mwaka 2010.Hakuna mwana-CCM makini aliyemjibu isipokuwa Mzee Makamba aliyeapa kwamba yupo radhi kwenda Jela kuliko kuruhusu upinzani dhidi ya JK,2010.mnalijua hilo,linajulikana
The best way to deal with comrade Shibuda is to ignore him.
Makosa yanafanyika pamoja na kwamba ni demokrasia lakini utani mwingine ni gharama kweli kweli.Huwezi kutangaza kugombea Urais Chadema halafu ukataka meneja kampeni wako awe mwenyekiti wa CCM halafu tukuchukulie mtu serious.Haya ni makusudi kwa kuwa Shibuda ni mzoefu wa michezo ya kisiasa na anajua analenga nini.
Hata mimi ningekuwa mwenyekiti wa vijana nisingevumilia kuona hili.
Sasa naamini hili suala litatauliwa kwa busara.Makamu Mwenyekiti Juliana Shonza ni kiongozi makini na shupavu kweli kweli.Ni kiongozi hodari.ni kiongozi adimu ambaye hawezi kupatikana kwingine isipokuwa ndani ya chadema tu.Anapenda kusema kile anachoamini.Nilipogombea uenyemkiti wa vijana huyu ndiye alikuwa chaguo langu.Aliniunga mkono na nilimuunga mkono.Sijawahi kutilia mashaka uwezo wake wa kuongoza.Kama kuna tatizo la flow of information nadhani tatizo hili litamalizika ndani ya vikao vya chama tu.It's not a big deal at all
Laiti tungekuwa na muundo kama wa ANC-YL ya Afrika Kusini basi leo tungekuwa na msemaji wa kama alivyo comrade floyd shivambu wa ANCYL.Mabaraza yote na jumuiya zote za vijana ndani ya vyama vya siasa Tanzania hatuwa na muundo kama huo kitu ambacho kinaweza kutoa mwanya kwa vijana kujikanganya au kuburuzana katika uendeshaji wa shughuli za kila siku kisaiasa na pengine hata maadui wa demokrasia kutumia mwanya huo kuleta mvurugano.
Naamini Baraza la vijana,litamaliza tatizo hili.Tusiwe na papara za kuhukumu watu.Tuwe na subira,tusikurupuke.Diplomasia na Busara inahitaji kutumika hapa.This is the right time to show leadership.
Malumbano ya watu binafsi yasiharibu taasisi.Shutuma kwamba Baraza la vijana ni wahuni hazivumiliki
Tatizo naona huyo binti anataka mambo yaendeshwe kama ccm. Tumeona mlolongo mrefu wakati wa kufanya reshuffle baraza la mawaziri. Walianza ccm bungeni, ikaja CC ya ccm DAR then wakakaa wakubwa tena ndio week mbili baadae rais anafanya mabadiliko! Huu ni udhaifu mkubwa maana baraza la mawaziri liko chini ya Rais, mambo ya vikao ni kupotezeana muda.
Sasa huyu binti anataka issue ya kumaliza kwa dakika chache waitane kila kona na kujadili! Wajadili nini? Yeye mwenyewe anakubaliana na tamko la Shibuda?
Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.Absolutely Candid scope,