Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Rais wa Marekani Joe Biden na Samia Suluhu wa Tanzania ni miongoni mwa viongozi waliowasili jijini London tayari kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II siku ya Jumatatu.
Viongozi hao ni miongoni mwa wakuu na viongozi 500 wa kigeni wanaokuja London kwa tukio linalowakutanisha viongozi wa ulimwengu wengi zaidi kuonekana kwa pamoja kwa miongo kadhaa.
Mawaziri wakuu wa Canada, Australia na New Zealand tayari wako Uingereza.
Mzozo unazingira baadhi ya wageni waalikwa, kama vile Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman.
Mbali na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinta Ardern, viongozi wengine wa Jumuiya ya Madola wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina na Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe.
India itawakilishwa na Rais Droupadi Murmu.
Viongozi walioalikwa leo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho huko Westminster na kutia saini kitabu cha maombolezo.
Mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabethi II yatafanyika kesho Jumatatu Westminster Abbey, London, kabla ya mwili wake kulazwa kwenye kasri la Windsor.
BBC