Vioja vya majibu ya barua ya posa 'UZARAMONI'

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Jana ndio tulifuata majibu hayo kwa ajili ya rafiki yangu
ambaye amechumbia binti wa kizaramo. Majibu hayo yamenisisimua
na kuniacha hoi hasa upande wa mambo ambayo tunatakiwa
kulipia. Haya ndiyo mambo yenyewe.

Kwanza tulitozwa faini kwa makosa mawili.
1. Tulipeleka barua ikiwa kwenye bahasha imefungwa kwa GUNDI
Hilo tuliambiwa ni kosa inabidi tusiifunge hiyo bahasha kwani inamaanisha
kuwa baba mzazi wa huyo binti hajatahiriwa. Duh!

2. Kwa haraka ya kutaka kuifungua mjomba wa yule rafiki yangu akaichana
kwa nyuma, nalo likawa kosa lingine eti matusi nani umemuona anatahiriwa
nyuma.

Makosa yote mawili tumelipia 25,000 kila moja siku tuliyofuata majibu ya barua.

HIZI NI BAADHI YA GHARAMA AMBAZO TUMETAKIWA KULIPA
1.Kisamvula ndevu - 25.000
2.Mkaja wa Bibi - 25,000
2.Mkaja wa Babu - 25,000
3.Kakwambia nani kama kuna mchumba 25,000
Naomba ufafanuzi kutoka kwa Wazaramo Mkaja na kisamvula ndevu ni vitu gani?

Pamoja na yote hayo nimefurahia mapokezi mazuri na ya aina yake ambayo
yananitamanisha kutafuta binti wa kizaramo.
 
duh, pole kwa kuoa mke kwa bei nafuu.

Jamaa yangu aliwahi kuniambia gharama ndogo husaidia kumkomboa binti pindi anapopata figa jingine halafu kidume ukaanza kulalama urudishiwe gharama zako. Sina uhakika kama hizi tabia bado zinaendelea lakini nakumbuka binti ambaye aliolewa mara 2 ndani ya mwaka mmoja,

hata kama lol

gharama ina heshima yake, haihusiani na ukicheche wala kutulia.

kwani gharama zikiwa kubwa ni ujanja?
unaweza oa mke wa mamiliono kumbe kicheche full
na mwingine akaoa kwa elfu kumi tu
na akapata mke wa kweli..
 
hahahhahhahahahahaha hii mada imenifurahisha sana,kisamvula ndevu na kutahiriwa nyuma... hilarious....:A S 41::smile:
 
Naomba ufafanuzi kutoka kwa Wazaramo Mkaja na kisamvula ndevu ni vitu gani?
Hii mkuu ni kwa ajili ya kunyolea nywele za sehemu za NANIHII saluni...
 
Ha ha haaaaa! Hili jibu linafanana na Avatar yako mkuu, by the way
hii kutahiriwa nyuma ni burudani ya aina yake.
 
Jana ndio tulifuata majibu hayo kwa ajili ya rafiki yangu
ambaye amechumbia binti wa kizaramo. Majibu hayo yamenisisimua
na kuniacha hoi hasa upande wa mambo ambayo tunatakiwa
kulipia. Haya ndiyo mambo yenyewe.

Kwanza tulitozwa faini kwa makosa mawili.
1. Tulipeleka barua ikiwa kwenye bahasha imefungwa kwa GUNDI
Hilo tuliambiwa ni kosa inabidi tusiifunge hiyo bahasha kwani inamaanisha
kuwa baba mzazi wa huyo binti hajatahiriwa. Duh!

2. Kwa haraka ya kutaka kuifungua mjomba wa yule rafiki yangu akaichana
kwa nyuma, nalo likawa kosa lingine eti matusi nani umemuona anatahiriwa
nyuma.

Makosa yote mawili tumelipia 25,000 kila moja siku tuliyofuata majibu ya barua.

HIZI NI BAADHI YA GHARAMA AMBAZO TUMETAKIWA KULIPA
1.Kisamvula ndevu - 25.000
2.Mkaja wa Bibi - 25,000
2.Mkaja wa Babu - 25,000
3.Kakwambia nani kama kuna mchumba 25,000
Naomba ufafanuzi kutoka kwa Wazaramo Mkaja na kisamvula ndevu ni vitu gani?

Pamoja na yote hayo nimefurahia mapokezi mazuri na ya aina yake ambayo
yananitamanisha kutafuta binti wa kizaramo.

mkuu vp hawajakuambia na kitanda ha bibi harusi?maana hiki ni lazima.
 
Asa hyo mahari mbona ni sawa na umepewa mke kama sadaka tu mkuu..,kinachokulalamisha hasa ni nin kwan?ebu nenda uchagan uone ka utaweza kuoa!
 
Back
Top Bottom