Hizo gharama ni nje ya mahari, hata hivyo bado mahari haikuwa kubwaAsa hyo mahari mbona ni sawa na umepewa mke kama sadaka tu mkuu..,kinachokulalamisha hasa ni nin kwan?ebu nenda uchagan uone ka utaweza kuoa!
Dah, nimekuelewa vizuri. Ahsante sana!Gazeti ukisikia mkaja kwa pwani ni kama vile 'mkanda' au belt.
Mkaja wa mama ni pale baada ya kujifungua hujifunga tumbo kwa kanga au kitenge ili lisilegee. Hiyo ni mila sijui kama inasaidia au la lakini ile kanga/kitenge hukunjwa vizuri kama belti na mzazi hujifunga tumbo lake.
Mkaja wa baba sina hakika sana lakini zamani vile vile baba walikuwa wanajifunga kitu kama belti kuzuia kikoi (munaita msuli). Kwenye hilo belti kuna sehemu ya kuwekea coins ambazo zamani ndiyo zilikuwa fedha nyingi sana.
Sasa hivo unalipishwa kama ni shukurani kwa wazee kumlea mtoto wao vizuri.
Hivyo vya babu na bibi nadhani sasa ndiyo vimebadilishwa kidogo.
kwani gharama zikiwa kubwa ni ujanja?
unaweza oa mke wa mamiliono kumbe kicheche full
na mwingine akaoa kwa elfu kumi tu
na akapata mke wa kweli..
Jana ndio tulifuata majibu hayo kwa ajili ya rafiki yangu
ambaye amechumbia binti wa kizaramo. Majibu hayo yamenisisimua
na kuniacha hoi hasa upande wa mambo ambayo tunatakiwa
kulipia. Haya ndiyo mambo yenyewe.
Kwanza tulitozwa faini kwa makosa mawili.
1. Tulipeleka barua ikiwa kwenye bahasha imefungwa kwa GUNDI
Hilo tuliambiwa ni kosa inabidi tusiifunge hiyo bahasha kwani inamaanisha
kuwa baba mzazi wa huyo binti hajatahiriwa. Duh!
2. Kwa haraka ya kutaka kuifungua mjomba wa yule rafiki yangu akaichana
kwa nyuma, nalo likawa kosa lingine eti matusi nani umemuona anatahiriwa
nyuma.
Makosa yote mawili tumelipia 25,000 kila moja siku tuliyofuata majibu ya barua.
HIZI NI BAADHI YA GHARAMA AMBAZO TUMETAKIWA KULIPA
1.Kisamvula ndevu - 25.000
2.Mkaja wa Bibi - 25,000
2.Mkaja wa Babu - 25,000
3.Kakwambia nani kama kuna mchumba 25,000
Naomba ufafanuzi kutoka kwa Wazaramo Mkaja na kisamvula ndevu ni vitu gani?
Pamoja na yote hayo nimefurahia mapokezi mazuri na ya aina yake ambayo
yananitamanisha kutafuta binti wa kizaramo.[/QUOTE pole kwa yaliyo wakuta,..!
Mwaka 2000, jamaa yangu alitozwa mahari ya Tsh 7000/= akajipatia jiko la binti wa Kizaramo...................
Nakubaliana nawe kabisa mkuu. Nimewahi kuona wana vitu vidogo vidogo vingi lakini vyote ni 'symbolic'. Halafu ni wakarimu sana kwa wakwe zao.Wazaramo ni progressive kwa msingi huu. Mahari ni "token" of appreciation, sio kama bei ya kununua mtumwa.
Ha! Mtwara na Lindi mpaka 50,000 unaweza kupata jiko.
Kuoa Uzaramoni mbona safi sana, wenyewe wanataka mdundo mkali wa muziki, hata ukiwapa maandazi mawilimawili hawana noma