Vioja, vituko au matukio wakati uko shule

Vioja, vituko au matukio wakati uko shule

Kingkorlar

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2018
Posts
875
Reaction score
996
Maisha ya shule bhana yana raha na karaha zake, ni maisha ambayo yanawakutanisha watoto au vijana WAKOROFI, WAONGO, WEZI, WAHUNI na WALIMU Wenye visa mbalimbali.

NAMBA 1

Kuna mwanafunzi mwenzetu kidato cha 4 wakati huo, jamaa alikuwa yuko njiani anaenda shule asubuhi, wakati anaendelea na mwendo nyuma yake kulikuwa na Mwalimu wa B/math tena wa kike age kama 40+... JAMAA akawa amemchek Madam.. Lakini ghafla jamaa akabanwa haja ndogo bhana!! Alichofanya si akageukia anakotoka ambako ndio Madam anatokea akalegeza ZIP akaanza kukokojoa.

Madam akamcheki na akamtambua ni flani)tena wa darasa lake, madam akafumba macho na kugeuka kukwepa asiendelee kumuona walikuwa jirani sana .. jamaa akamaliza safari ikaendelea.

Walipofika shule muda wa PAREDI Madam ikabidi amuite jamaa mbele ya Paredi na Mkuu wa shule alikuwepo, Madam akamshitak jamaa kwa alichokifanya.. Jamaa katika kujitetea akasema "Sasa pale njiani hakuna choo yeye angefanyaje?.. Tena anadai kama madam amemuona kwa nini isiwe siri yake"

Ni noma!!
 
Back
Top Bottom