Ving'amuzi vya Zuku ni anti-mvua

Ving'amuzi vya Zuku ni anti-mvua

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
12,268
Reaction score
9,154
Imekuwa inatokea mara kwa mara kwa hivi ving'amuzi vya Zuku kila mvua inyeshapo hasa iwe na upepo /radi au mvua kubwa basi vinakuwa ni kukwama hadi basi, ni kama upo disco ambapo DJ ana scratch Cd , kweli inaudhi sana,hao mafundi wao nao ni kutaka fedha tu hakuna wanachokifanya,kwa hakika kwenye msimu wa mvua kama hizi za masika ,ni kuwa hela yetu inaliwa bure bila kupata huduma stahili kutoka kwa hawa Zuku, hata CC yao ni ya hovyo hawajibu chochote simu zinaita tu zingine zinaenda kwa watu wa mitaani,sijui na wanaotumia DStv huu ujinga upo?
 
ZUKU sio ANTI-MVUA.... pole sana mjomba... nikipata nauli ntakuja kukurekebishia.. maana hao ni
ANTI-VIRUS..
 
Sisi kikwetu tunaita Mvuaphobia!
 
Anti-mvua?
Kama vingalikuwa anti-mvua basi vingalifaa sana.
Nahic ulitaka kusema ni mvua-incompatible.
 
Hivi hii biashara ya ving'amuzi ni ya nani maana haiwezekani program ya kitaifa iendeshwe na wahuni wa kichina
 
Kwa utaalamu wa vingamuzi serikali imewachoka raia wake hasa vingamuzi vya startimes,Serikali imewalaghai watu na vingamuzi vya kihuni.Wananchi wameshindwa kutambua kuwa mfumo wa digital ni wa siku nyingi sana hapa bongo.Kwa mtumiaji yeyote anayetumia dish na receiver yuko digital siku nyingi sana.Kama ni digital makampuni kama dstv siku zote wapo huko.Hivi vingamuzi vya TELESTAL ni ujinga mtupu. Kingamuzi ni cha Satellate tu.Ukiona chenga kwenye tv yako kwa kutumia satellate dish,ilo ni tatizo la fundi wako.
 
Imekuwa inatokea mara kwa mara kwa hivi ving'amuzi vya Zuku kila mvua inyeshapo hasa iwe na upepo /radi au mvua kubwa basi vinakuwa ni kukwama hadi basi, ni kama upo disco ambapo DJ ana scratch Cd , kweli inaudhi sana,hao mafundi wao nao ni kutaka fedha tu hakuna wanachokifanya,kwa hakika kwenye msimu wa mvua kama hizi za masika ,ni kuwa hela yetu inaliwa bure bila kupata huduma stahili kutoka kwa hawa Zuku, hata CC yao ni ya hovyo hawajibu chochote simu zinaita tu zingine zinaenda kwa watu wa mitaani,sijui na wanaotumia DStv huu ujinga upo?

Heshima yako mkuu, kiufundi mvua/snow na miti vinazuhia mawimbi ya microwave kupita - hivyo basi mvua ikinyesha kubwa kidogo haijalishi kama una dishi ya DStv au Zuku picha zita onekana kukwama kwama, kukatika katika na kama mvua ni kubwa screen itakuwa blank kabisa au utaona raster tu bila picha; kasi ya kukatika matangazo utokana na band ya microwave: kama ni C-Band unaweza kuendelea kuona picha kama mvua si kubwa lakini Ku-Band hiyo haivumilii mvua hata kidogo hata mvua ya rasha rasha itakatiza matangazo.
 
Hilo tatizo la signal kupotea kipindi cha mvua hata kwenye DSTv lipo, sio Zuku pekee yake
 
heshima yako mkuu, kiufundi mvua/snow na miti vinazuhia mawimbi ya microwave kupita - hivyo basi mvua ikinyesha kubwa kidogo haijalishi kama una dishi ya dstv au zuku picha zita onekana kukwama kwama, kukatika katika na kama mvua ni kubwa screen itakuwa blank kabisa au utaona raster tu bila picha; kasi ya kukatika matangazo utokana na band ya microwave: Kama ni c-band unaweza kuendelea kuona picha kama mvua si kubwa lakini ku-band hiyo haivumilii mvua hata kidogo hata mvua ya rasha rasha itakatiza matangazo.

nakubaliana nawe 100%
 
Mkuu Bukyanagandi ahsante kwa kumuelimisha mwanaJF wenzetu, ni kama ulisoma mawazo yangu kabla. Mara nyingi tatizo hilo hutokea kwa wale wanaotumia madishi hasa ya bati kutokana na maji kujaa, ajaribu kulisimamisha ili maji yasituame ndani.
 
point yako ni nzr sana ya maji hata mi ckufkiria hilo,

ila huku mwshoni kuna mzaha umeingia sa ukilismamisha dish, ndo position gan hii na utaona nini kwny tv yako?
 
point yako ni nzr sana ya maji hata mi ckufkiria hilo,

ila huku mwshoni kuna mzaha umeingia sa ukilismamisha dish, ndo position gan hii na utaona nini kwny tv yako?
Mkuu sio kulisimamisha kabisa, at least kuwe na slope (mwinuko).
 
Back
Top Bottom