Asalaam wana JF
Nafikiria kununua king'amuzi cha Easy Tv,ila kabla sijalipia ningeomba kupata maoni yawe chanya au hasi kwa yule ambaye anakitumia king'amuzi hiki.
Natanguliza shukrani zangu
Nakitumia maskani. Nikifananisha Easy TV na Startimes, ETV is by far the best, ni sawa na kufananisha mafua na Ebola. Bila kusuasua we kinunue tu. Monthly fee ni flat, 9000/-.
Wana channel 5 za Movie, 2 za katuni (Nikkelodeon na Mbc3), 2 za taarifa za kimataifa (BBC na Al Jazeera), MTV na Channel V (Burudani), za dini ziko 4 (Emmanuel Tv, EWTN, na za Kiislamu 2, moja Kiingereza na moja Kiswahili), za Michezo kuna Optima (wanaonesha recorded matches za EPL) na Dubai Sport. Kama we mpenzi wa mieleka basi hapo ndio penyewe. Za hapa nyumbani unapata:-
Itv, Channel 10, Tbc1, Eatv, Clouds Tv, DTV na capital. Star TV imeondolewa (wana ugomvi wa kibiashara, kwa sababu Star Tv wanataka Tv hiyo iwe kwenye kisimbuzi chao tu)
nakitumia,nikizuri sana japokuwa kuna wakati baadhi ya chaneli zinagandaganda hasa za muvi.sijaweza kubaini tatizo ni nini kama ni king'amuzi chenyewe au ni setting yangu ya antennae ndo sio nzuri.pia star tv mara nyingi huwapotea hewani.kwa sasa ina wiki mbili haipatikani.sijajua tatizo ni nini pia au ndo wameshajitoa.nawasilisha kwa msaada
Ndugu, niliuliza wakala wao mmoja, alisema kwamba Star TV hawataki channel yao ipatikane kwenye visimbuzi vingine, wanataka waioneshe kwente Continetal yao tu, ndio sababu wameiondoa. Ila niliambiwa itarejeshwa, kwa sababu suala hilo linashughulikiwa na TCRA