Ving'amuzi vya Azam vibovu

Ving'amuzi vya Azam vibovu

Kwa matatizo yote ya Azam tv kingamuzi nendeni ofisi za azam zamani national milling buguruni
 
hivi kuna watu mna akili gani...kwa hiyo unabisha kwamba vingamuzi vyangu havijaharibika au?na nani kakwambia nimefanya research?unajua nilikuwa najiulizaga sana kwanini mtu anamtukana mtu humu jf wakati hawafahamiana lakini kumbe kuna watu mnastahili kutukanwa
Changu nimekaaa nacho mwaka kikaungua nikawapelekea wakanibadilishia kwa malipo ya 60000 tzs na remote sasa some buttons hazifanyi kazi nikawaendea wakasema haitengenezek8 nunua mpya 25000tzs sikuwa na hela siku hiyo ila wakati nipo mtaa napiga mayowe ubovu na ughali wa vifsa vya azam ndipo swahiba mmoja akaniuliza "wewe si una kisimbuzi cha star time pia?" "Nikamjibu naam"
Basi akaniambia kuwa tumia remote ya startime kwa kisimbuzi cha azam .
Huyo anaepinga kuhusu udhaifu wa vifaa vya azam akapimwe akili
 
Pole kwa changamoto unazopata kwenye ving'amuzi vya Azam. Bila shaka wewe ni mpenzi na mdau wa Azam maana una vingamuzi vitatu vya Azamtv.Umeangalia na jinsi unavyotumia hivyo ving'amuzi?
Kwa msaada wasiliana na AzamTV customer care at info@azam-tv.com
Huwa wapo faster sana ku-respond.

Note: Kwa kinachotokea kwako hiyo haitoshi kusema kwamba " Ving'amuzi vya Azam vibovu sana"
 
Ni kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikikutana na usumbufu kutoka kwenye hivi vingamuzi vya azam, yani hakiwezi kukaa mwaka mmoja kikafanya kazi lazima kiharibike. Sitaki kuandika sana ila ningependa kutoa matukio machache juu ya ubovu huo.

Kwanza ni sehemu yangu ya biashara nimefunga hiki kingamuzi...baada ya mwaka mmoja kile kingamuzi kikawa kinazima na kuwaka chenyewe, cha pili ni cha rafiki yangu yeye baada ya mwaka mmoja kikawa baada ya muda kinasema insert card wakati kadi ipo hapo mpaka uzime uwashe ila baada ya muda inajirudia. Cha hapa nyumbani ni wiki sasa kingamuzi kimezima chenyewe tu kimegoma kuwaka.
mkuu, hivyo ving'amuzi vya azam ni JIPU.
 
Sio kwl jmn mbona mi changu kina miaka 3 tena ni vile vya toleo vya kwnz kipo poa kabisa hakina shda jaribun kumwita fund akichek labda sehem ulipogongelea misumal inalegea ndo maana kinapoteza signal au kusikrachi
 
Babu, jifunze kuwa mtunzani usijifunze kutukana watu...kuna watu tuna matusi hapa hadi tukipita mtaani watu wanaingia ndani, kuwa mpole. Mwambie na huyo demu wako kwamba, aandike namba za kadi ili kwamba anapotaka kulipia asiwe na haja ya kuchomoa kadi mara kwa mara na kuchubua ule utepe kiasi iwe inamprompt kuinsert kadi.....sawa?

Mkishindwa njooni muangalie TV kwangu, ila mkumbuke mkineng'eneka na king'amuzi....KONZI, mi cha kwangu hakichezewi. Karibuni.
kweli we maana mtoka pabaya,gani ukipita mtaa watu wanaingia ndani?? duh
 
Mimi navyowajua Watanzania wenzangu, mtu atapakia tani 2 kwenye kirikuu na kesho atasimama jukwaani kusema 'Suzuki Carry, labda nipewe bure' lkn muulize kama aliwahi kusoma manual book ya carry.......mbio.

Tufahamu kuwa, kukalia remote ya TV si sehemu ya makubaliano ya huduma na mtoa huduma. Mwanao kuibutabuta chini si sehemu ya matumizi ya kifaa hicho. Joto la mahali husika lina nafasi ya kudumu na ubora wa huduma utakayopata. Hakuna UNGO wowote unaofanya vizuri ikiwa uelekeo wake unakabiliana na matone ya mvua.

Kabla hatujavurumisha comments kuhusu ubora wa bidhaa fulani, tujikague mazingira na tabia zetu za matumizi.
 
Changu nimenunua mwezi wa 3 mwaka 2014 na hamna tatizo kama hilo labda kama wanaongeza channel ndo kinaji update
Sema mimi wameniboa tu kupandisha bei ya vifurushi...
 
Mimi navyowajua Watanzania wenzangu, mtu atapakia tani 2 kwenye kirikuu na kesho atasimama jukwaani kusema 'Suzuki Carry, labda nipewe bure' lkn muulize kama aliwahi kusoma manual book ya carry.......mbio.

Tufahamu kuwa, kukalia remote ya TV si sehemu ya makubaliano ya huduma na mtoa huduma. Mwanao kuibutabuta chini si sehemu ya matumizi ya kifaa hicho. Joto la mahali husika lina nafasi ya kudumu na ubora wa huduma utakayopata. Hakuna UNGO wowote unaofanya vizuri ikiwa uelekeo wake unakabiliana na matone ya mvua.

Kabla hatujavurumisha comments kuhusu ubora wa bidhaa fulani, tujikague mazingira na tabia zetu za matumizi.
Cut the crab...
 
Mkuu hapo najikanya kwenye remote maana haka katoto chetu na hiyo remote ni majanga!
 
Viko poa mi kinakarbia kutimiza mwaka wa 3 kinadunda tu kikubwa utunzaji..ila remote yangu naona imeshachoka na sijui nitaipataje..
 
Haya malalaiko yenu kuhusu ving'amuzi vya local providers ndio mnafanya DSTV wazidi kutukamua,hebu nendeni kwa wahusika huko mkasaidiwe,sisi wengine kwa DSTV ni kama mbwa na chatu hatupindui ingawa with crocodile tears
 
Mm changu nimenunua ile mara ya kwanza kabisa zilipoingia sokoni, mpaka leo ninacho na hakijawaji kunisumbua
 
Back
Top Bottom