Ving'amuzi vya Azam vibovu

thehunk

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
528
227
Ni kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikikutana na usumbufu kutoka kwenye hivi vingamuzi vya azam, yani hakiwezi kukaa mwaka mmoja kikafanya kazi lazima kiharibike. Sitaki kuandika sana ila ningependa kutoa matukio machache juu ya ubovu huo.

Kwanza ni sehemu yangu ya biashara nimefunga hiki kingamuzi...baada ya mwaka mmoja kile kingamuzi kikawa kinazima na kuwaka chenyewe, cha pili ni cha rafiki yangu yeye baada ya mwaka mmoja kikawa baada ya muda kinasema insert card wakati kadi ipo hapo mpaka uzime uwashe ila baada ya muda inajirudia. Cha hapa nyumbani ni wiki sasa kingamuzi kimezima chenyewe tu kimegoma kuwaka.
 
Mimi changu ninacho zaidi ya mwaka kiko poa, labda baada ya kupata soko zuri isijekuwa wajanja wameksha ingiza feki kupata soko kupitia mgongo wa azam, ni mtazamo tu
 
Kwa ukwel sehem ya biashara kuna mambo mengi kubongeaza kupitia king'amu badala ya remot inaweza rahidisha kuharibika haraka
 
Unachofanya ni kuharibu biashara za watu kwa research yako ya kibwege, mi changu kina mwaka na miezi kadhaa bado kiko fit, usipende kukurupuka kuandika vitu visivyo na uhakika
 
Unachofanya ni kuharibu biashara za watu kwa research yako ya kibwege, mi changu kina mwaka na miezi kadhaa bado kiko fit, usipende kukurupuka kuandika vitu visivyo na uhakika
hivi kuna watu mna akili gani...kwa hiyo unabisha kwamba vingamuzi vyangu havijaharibika au?na nani kakwambia nimefanya research?unajua nilikuwa najiulizaga sana kwanini mtu anamtukana mtu humu jf wakati hawafahamiana lakini kumbe kuna watu mnastahili kutukanwa
 
Mkuu ni kweli, hata mimi changu kimekwama hivyo hivyo! Nimeamua kutumia zuku na Aristat.
 
Natumia mwaka wa pili sasa kipo poa sana...inategemea ba mazingira ulipo mkuu..by the way ukiacha DSTV,Azama wanakimbiza sanaaaa...hao wengune tupa kulee
 
Vibovu kweli me home wanalalamika wanasema hakipeleki signal wakati dish na ungo vipo safi tuu bora dstv aisee
 
hivi kuna watu mna akili gani...kwa hiyo unabisha kwamba vingamuzi vyangu havijaharibika au?na nani kakwambia nimefanya research?unajua nilikuwa najiulizaga sana kwanini mtu anamtukana mtu humu jf wakati hawafahamiana lakini kumbe kuna watu mnastahili kutukanwa

Babu, jifunze kuwa mtunzani usijifunze kutukana watu...kuna watu tuna matusi hapa hadi tukipita mtaani watu wanaingia ndani, kuwa mpole. Mwambie na huyo demu wako kwamba, aandike namba za kadi ili kwamba anapotaka kulipia asiwe na haja ya kuchomoa kadi mara kwa mara na kuchubua ule utepe kiasi iwe inamprompt kuinsert kadi.....sawa?

Mkishindwa njooni muangalie TV kwangu, ila mkumbuke mkineng'eneka na king'amuzi....KONZI, mi cha kwangu hakichezewi. Karibuni.
 
Back
Top Bottom