Pretty hao wa ughaibuni hawako sahihi kwa kila kitu.Hivyo basi siyo watu wakujilinganisha nao;kwasababu na wao wanakosea pia kama wewe unavyokosea halafu unataka kwenda nao sawa wakati na wao wanachemsha/kutokota kabisa.Naomba tuache kuwa wanafiki,sidhani kama kuna mahali katika maandiko na maadili katika sehemu husika yanakubaliana na hilo vazi!watanzania tumezidi kulalamika, mbona nchi za ughaibuni watu wanaenda kanisani na vimini au short pants watu hawalalamiki? Kwani kanisani ulienda kumuomba Mungu au kuangalia watu wamevaaje? Au nyie wanaume waafrika mpo tofauti na wanaume wa huko ughaibuni, au nyie ndio mnajua kuhisi sana mnapoona msichana kavaaa nguo fupi?
We Muteso kama unaenda kanisani nenda kasali, usiende kuangalia wasichana wamevaaje. Wasichana wengine wanapovaa nguo fupi sio kwamba ili kuwavutia wanaume, ila mwingine nguo fupi ndio anayopenda.
Mungu anaangalia moyo na sio mavazi, kinachotakiwa ni kuwa na moyo msafi mbele zake.
wewe nenda kanisani na timiza ajenda yako. Kila mtu anaenda hapo na ajenda yake. Hao akina dada nao wana ajenda yao. Wewe jali ya kwako tu na wala usijali wao wanavaaje. Just leave them alone.
Wana JF kuna jambo limekuwa likinisumbua sana kwa siku nyingi. Kila niendapo kanisani huwa najaribu kuangalia dada zetu wanavyovaa na huwa najiuuliza maswali mengi sana. Nashindwa kuelewa kama wanaenda kuuza sura kanisani au wanaenda kusali. Mfano mzuri ni kanisa la chuo kikuu cha Dsm. Hapa kuna mabinti wanaovaa vimini na wanakaa viti vya mbele. Wanapofika huwa wanajitahidi kubana miguu na kuvutavuta vijimini vyao lakini kipindi kinafika wanachia waziii wananika mapaja na viskintight vyao na wengine skintight hazionekani kwa maana watakuwa wameva bikini. Sasa naomba wenye uwezo wa kutoa onyo kwa hawa kina dada watusaidie. Nafikiri makanisa yote yangeweka sheria kwamba ni marufuku mwanamke kuingia kanisani na nguo zinazovuka magoti. Hebu angalia kina mama wa kiislamu wanapoenda msikitini wanajifunga mahijabu na makanga mengi tu. Kwa nini wakristu wasiwe na kanuni na taratibu za mavazi ya kuvaa siku za ibada. Waache kuwatia Ibilisi wachungaji na mapadre kwa kupanua mapaja yao kwenye viti vya mbele. Naomba tusaidiane kupambana na hili. Thanks in advance. May Almighty Father guide you and bless you so that you can come up with good and reasonable ideas on how to handle this damned matter.

Ni kweli maneno yako, naongezea hapo... Ukitazama na kutamani, umezini...!
Lakini vipi yule mwenye kumtamanisha mwingine... mpaka yule mtazamaji akajikuta akitamani kwa kule kutamanishwa na mtamanishaji!?
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
1Tim 2:9
Hakuna anayemtamanisha mwenzake, kiini cha tamaa kipo na hutoka ndani ya atamaniye. tamaa huletwa na fikra na hisia na malengo ya mtu. Wapo wanaume wengine ambao huwatamani wanawake wa kiislamu kwa mavazi yao ya baibui. Mwanamume anajenga hisi kwa kuutazama mwonekano wa mwanamke mwenye kuvaa baibui na kufikiria atakachokuwa anakiona wakati anapoitoa hiyo baibui. Fikra zake zinamwelekeza kuwa kitu kilichofichwa ndani ya hilo vazi jeusi lazima kitakuwa kizuri na chenye thamani kubwa. Baada ya hapo anapata matamanio na kuweka lengo la kumtafuta na kumnasa mhusika.
Lakini ikiwa wakati unatoka nyumbani kwako mawazo na fikra zako umezielekeza na kuzikita kwenye Ibada ya Misa. Utakapokuwa ndani ya Kanisa au nyumba nyingine ya Ibada hutaviona vimini, Skintaiti, bikini wala mapaja. Hebu fikiria watu wanavyoweza kuwa na mawazo kiasi cha kutojuwa kuwa anavuka barabara au mtu unamsalimia lakini hakusikii. Vivyo hivyo tukizamisha fikra zetu kwenye kuwasiliana na mungu hatutakwazika kamwe

Hapana, husiwaombee laana kwa MUNGU ila waombee wabadilike na kufanya yale yaliyo mema kwa MUNGU na binadamu wenzaoMola awalaani wale wote wanaokwenda kwenye nyumba za ibada kwa nia ya kutamanisha wenzao kishetani
Rejea vitabu vya Dini. Aliyeeza kushinda matamanio ni Nabii Yusuf alipotamaniwa na mke wa Mfalme.
sasa tujiulize kuna akina Yusuf angapi hivi sasa? watu hawapigiwi wanacheza.
QUOTE]
Blue: Aisee sidhani kama siku hizi kuna akina Yusuph
Red: Teh teh teh teh teh teh! Watu wanadundika tu, kazi kweli kweli
wewe ndo una-set standards za nidhamu? kama mkware mkware tu. nani kasema kuangalia mapaja kanisani ni dhambi zaidi ya kuangalia barabarani au kwenye daladala au darasani in that matter?Suala siyo makwazo tu ya huo uvaaji. Suala hapa ni kwamba uvaaji wa namna hiyo haustahili Kanisani kwa sababu Kanisa ni NYUMBA ya Mungu. Watu wanaoenda hapo lazima waende kwa ADABU na UCHAJI WA MUNGU kwani kanisa ni nyumba takatifu ya Mungu. Siyo kilabu cha pombe au ukumbi wa senema. Kumbe mtu anayeingia kaniasani kavaa ovyo anamkosea Mungu kwa nafasi ya kwanza kabisa.
Kwa nafasi ya pili, labda ndiyo yanakuja hayo makwazo kwa watu wenye kuangaza macho kwa mabinti, jambo ambalo naona wengi mmemkaba koo mleta mada.
Kumbe tuwe tunawaangalia au hatuwaangalii hao wadada waliovaa vibaya, ijulikane kuwa wanafanya utovu wa nidhamu mbele ya Mungu. Kuvaa nguo fupi kanisani ni machukizo kwa Mungu aliye mtakatifu. Please, tuiheshimu nyumba yake.